Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akikata utepe
kuzindua msaada wa vyoo na mfumo wa maji safi kwenye shule ya Msingi
Kipampa, Kigoma. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya Posta Tawi la
Kigoma, Fidelis Ndahani.
Naibu Mstahiki Meya wa Kigoma, Mh. Ruhomvya Rashid Ruhomvya,
akisikiliza hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania
(TPB), Sabasaba Moshingi, wakati wa sherehe ya makabidhiano ya msaada wa
Vyoo na mfumo wa maji kwenye shule ya Msingi Kipampa. Wengine kutoka
kulia ni Meneja Mahusiano wa TPB, Noves Moses na Meneja wa TPB, Tawi la
Kigoma, Fidelis Ndahani.
Naibu
Mstahiki Meya wa Kigoma, Mh. Ruhomvya Rashid Ruhomvya akifungua bomba la
maji kwenye mojawapo wa vyoo vilivyokarabatiwa na Benki ya Posta kwenye
Shule ya Msingi Kipampa, Kigoma. Wanaotazama ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
TPB Sabasaba Moshingi Mkuu wa shule ya Kipampa.
Ofisi Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kipampa baada ya
kuwakabidhi vyoo vipya pamoja na mfumo wa maji safi.
No comments:
Post a Comment