Thursday, August 7, 2014

WEZI WA KAZI ZA WASANII KUKIONA,KAMATA KAMATA YAANZA RASMI


 Kampuni ya Msama Promotions Ltd,kwa kushirikiana na Wizara ya habari vijana,utamaduni na michezo  imetangaza neema kwa wasanii kuanza zoezi la kuwakamata watu wanaouza nakala feki  za wasanii hapa nchini.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Bwana  Alex Msama  amesema hayo jijini dar ,kuwa zoezi hilo limekwishaanza, na mpaka  sasa wamekamatwa vijana wane katika mkoa wa Dodoma na watatu jijini Mwanza.

‘’Kuna kazi mbalimbali ambazo zinaibiwa kila kukicha huku wamiliki wa kazi hizo wakiendelea  kushuka kiuchumi  na kutoona faida  yoyote ya kazi hizo,huu ni wakati kwa wasanii kuneemeka na kazi zao.Hivyo tutahakikisha
tunafika kila mahali hata sehemu zisizofikika kirahisi na yote hii ni kuonyesha kuwa tunajali na tunathamini kazi za wasanii wetu’’,alisema Msama kwa msisitizo.

Alisema, nakala zote zitakuwa na stika za TRA  kuhakikisha hakuna wizi
wowote unaofanyika  na unaotokea katika kazi mbalimbali za wasanii.Stika hizo zimewekwa ili kuwabaini wale wote wenye hulka hiyo ya kuiba kazi za wasanii .Operesheni  hiyo itafanyika  bila kujali wadhifa wake ama cheo chake,akaongeza kusema kuwa zoezi hilo ni salamu kwa wale wote wanoatumia kazi za wasanii bila kufuata  utaratibu wa sheria zilizopo.

Pia amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika changamoto,na pia wamekuwa wakishirikiana  nao kuhakikisha  zoezi hilo linakuwa endelevu na kuzunguka kila mkoa kuhakikisha  kazi za wasanii zinaheshimiwa na zinalindwa kwa kila namna.

No comments:

Post a Comment