Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi
nchini akimwelekeza bondia Lulu Kayage jinsi ya kukupa ngumi wakati wa
mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu mpambano
utakaofanyika September 27 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es
salaam picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage kulia akielekezwa
jinsi ya kupiga makomde mazito na Kocha Habibu Kinyogoli 'Masta' wakati
wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu Septermber 27
katika ukumbi wa frends Corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Juma Biglee kushoto akioneshana
umwamba na Lulu Kayage wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya
Ilala Amana Dar es salaam Lulu anajiandaa na mpambano wake na Fatuma
Yazidu utakaofanyika Septermber 27 katika ukumbi wa Frends Corner
Manzese Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana
na Juma Biglee wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma
Yazidu september 27 Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage kushoto akifanya
mazoezi ya kuimalisha misuli ya tumbo wakati wa mazoezi yake ya
kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu september 27 katika ukumbi wa
frends corene manzese Dar es salaam kushoto ni Titus Jonson Picha na SUPER D BLOG
Na Mwandishi Wetu
lulu kayage |
akizungumza wakati akiwa mazoezini
katika kambi ya ilala amana Dar es salaam amemtahadhalisha mpinzani wake
kufanya mazoezi ya kutosha kwani yeye kwa sasa yupo fiti kupita kiasi
na akuna bondia wa kike kwa Tanzania hii mwenye uzito wake anaeweza
kumsumbua kwa sasa kwani ana uzoefu mkubwa na wakutosha
aliongeza kwa kusema kuwa jinsi
anavyosimamiwa mazoezi na jopo la makocha wake wanao ongozwa na kocha
mkongwe nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kocha wa kimataifa wa mchezo wa
masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro ambao
wanamuhimiza kila wakati kufanya mazoezi ya kutosha na ndio wana
muongeza moyo zaidi kwa ajili ya kufanya mazoezi
Lulu aliongeza kuwa mchezo wa masumbwi
nchini wasichana wanaojitokeza ni wachache sana hivyo kukosa msisimko
wa kila wakati kucheza wasichana kwa wasichana hivyo kuomba wasichana
mbalimbali wajitokeze kufanya mazoezi na kucheza mchezo kwa ajili ya
afya pia ni kwa ajili ya ajira kumbuka mchezo wa ngumi ni ajira kama una
uwezo wa kufanya vizuri
siku hiyo pia kutakuwa na mpambano
mkali utakao wakutanisha Nassibu Ramadhani na Mohamed Matumla mwingine
ni Sadiki Momba na Adam Ngange, Issa Omari na Juma Fundi
No comments:
Post a Comment