Mkurugenzi
Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Bw. Mike Seo akiwahutubia na
waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ufunguzi rasmi kituo
kikubwa cha bidhaa za Samsung mjini Arusha.
Meneja wa Usambazaji wa Samsung Electronics Tanzania, Bw Sylvester Manyara akitoa maelezo kwa waandishi wa habari na umma.
Meneja
wa huduma wa Samsung Electronics Tanzania, Bw. Mubarak Mikidad
akiwahutubia wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari katika hafla
ya ufunguzi rasmi kituo kikubwa cha bidhaa za Samsung mjini Arusha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania, Bw. Mike Seo akiongea na
wateja katika ufunguzi rasmi wa kituo kikubwa cha bidhaa za Samsung
mjini Arusha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Bw. Mike Seo na Bw Nawaz
Ladha, Mkurugenzi wa Freedom Electronics, mmoja wa wasambazaji wakuu wa
Samsung Electronics Tanzania wakikata utepe kufungua rasmi kituo
kikubwa cha bidhaa za Samsung mjini Arusha.
KAMPUNI YA
VIFAA VYA KIELEKTRONIKI SAMSUNG YALENGA KUKUZA UCHUMI WA JIJI LA ARUSHA
Arusha, 19 Septemba 2014. Kampuni ya Samsung
inazindua rasmi duka kubwa na kituo chake
cha huduma kwa wateja lililopo barabara ya Sokoine mjini Arusha siku ya leo.
Uzinduzi huo utawawezesha wateja wake wote mkoani Arusha kupata huduma stahiki
na bidhaa halisi za Samsung. Kituo hiki ni cha kwanza kuzinduliwa mkoani Arusha
na kampuni hii yenye idadi kubwa ya watumiaji na vifaa bora vya kielektroniki
ulimwenguni.
“Mtazamo wa maisha ya wateja hubadilika
kwa kasi kubwa na kuwafanya kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma bora. Kama
kampuni kubwa inayoongoza kuwa na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni, Samsung
imefanya juhudi kubwa kuhakikisha inatimiza mahitaji ya wateja wake wote Afrika.
Mkoa wa Arusha hutegemea sana biashara kwani una wakaazi toka jamii
mchanganyiko. Hivyo katika Afrika Mashariki, Arusha ni kitovu cha wageni toka
nchi mbalimbali ulimwenguni. Kampuni ya Samsung ina imani kubwa kwamba kituo
cha huduma kwa wateja kitatoa ushirikiano mzuri na kuboresha uhusiano kwa wateja
wake mkoani Arusha. Kwasababu Arusha ni kituo kikuu cha safari nchini
Tanzania”, haya yamesemwa na
Mkurugenzi mkuuwa kampuni hii nchini Tanzania, Bw. Seo
Mbali
na kuuza simu za mkononi na bidhaa za kielektroniki, duka hili jipya la Samsung
litatoa huduma za ziada kwa wateja wake. Hii ni pamoja na kuwapa wateja wake
watakaojisajili na uduma ya e-warranty
(dhamana) usaidizi wa kiufundi bila malipo kwa kipindi cha miaka miwili.
Mpango
huu utawanufaisha wateja wa Samsung watakaosajili bidhaa zao kupitia Simu. Huu
ni mchakato utakaofanyika kwa kutuma namba ya IMEI kwenda 15685. Baada ya
kufanya hivyo wateja watanufaika na msaada wa kifundi kwa kipindi cha miaka
miwili sambamba na kujipatia nafasi ya kushinda bidhaa mbalimbali za Samsung.
Katika
kusherehekea uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinawasogezea
wateja wake huduma karibu, kampuni hii kubwa duniani inawaletea habari njema
wakaazi wa Arusha kwa kutoa punguzo kubwa la bei za bidhaa zake. Kwenye kipindi
hiki cha ufunguzi bidhaa zitakazokuwa na punguzo la bei ni pamoja na; Luninga, feni,
majokofu na vifaa vya nyumbani. Bila kuwasahau wateja wake wa simu, vifurushi
vya intaneti na zawadi za T-shirts zitatolewa kwaajili ya wanunuzi wa simu aina
ya Galaxy Trendlite.
Kwa sasa nchini Tanzania
kampuni ya Samsung ina maduka na vituo vya huduma kwa wateja katika mikoa ya
Mwanza na Dar es Salaam na ina mipango kabambe kuongeza huduma zake mikoa
mingine.
Duka hili na kituo chake
cha huduma kwa wateja vitatoa huduma siku za wiki yaani Jumatatu-Ijumaa kuanzia
saa 9.30 asubuhi hadi 5.00 jioni kwa Jumamosi ni kuanzia saa 9.30asubuhi hadi
1.00 mchana, litafungwa siku za Jumapili na Siku kuu.
Kuhusu Vifaa vya kielektroniki
vya Samsung
Teknolojia ya Samsung inatumiwa
na watu takribani 236,000 katika nchi 79, inaleta mabadiliko na kuiwezesha
dunia kuingia kwenye teknolojia mpya na matumizi ya smart phone, luninga,
air-conditioner, vifaa vya nyumbani vya kieletroniki, kamera, na vifaa vya
maofisini kama kompyuta na printers ambavyo vina teknolojia ya hali ya juu
kukidhi mahitaji ya wateja. Kujifunza mengi zaidi, tembelea www.samsung.com na www.facebook.com/SamsungMobileTanzania
Kwa taarifa Zaidi wasiliana na:
James Laidoson – Spearhead
Africa Ltd
Simu: 0754 252 256
Email: james@spearheadafrica.com
No comments:
Post a Comment