Licha
ya majukumu mbalimbali yanayowakabili viongozi wetu wakuu wa nchi
lakini kuwatembelea wapiga kura wao na kujua yanayowakabili ni jambo
muhimu sana ambalo mbali na kuwapa faraja wananchi hao wa eneo husika
lakini inaleta matumiani kuwa kiongozi wao yupo na anawajibika.
Mara
kwa mara baadhi ya wabunge hudhani kuwa bila ya kuwa na kitu huwezi
enda Jimboni labda hadi uwe na mifuko ya saruji, bati au jezi na mipira
ya kuwagawia wapiga kura wake.
Jana
Naibu Waziri wa Fedha, na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Mchemba
alitembelea Jimboni kwake ili kufuatilia Utekelezaji wa miradi ya
Maendeleo na Kusikiliza Maoni,Matatizo na Maombi ya Wananchi.
kundi la burudani likitumbuiza.
Mbunge akipokea zawadi mbalimbali na kuzipa baraka.
Michango ya kijamii ilifanyika kwaajili ya maendeleo.
Mwigulu akiwaaga wapiga kura wake.
No comments:
Post a Comment