Dar es Salaam
– Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village
umeshiriki maonyesho ya nyumba yalioyofanyika jijini Dar es Salaam inategemea
umeanza hivi karibuni.
Wakati Meneja Masoko
na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village akiongea alisema “Kwa sasa
ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zitakuwa tayari ifikapo
Januari 2015. Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika
kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama
hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni.
Mrudi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni
hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko
300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment
zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.
Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wa kazi hawatahitaji
kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha
polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika
No comments:
Post a Comment