Monday, September 15, 2014

Sikinde sasa kuzindua Jinamizi lao Oktoba


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVMgN3FGO5qcoaY0CIIFySEfXr5697SV_JUFFofouD78ftB1VINzF_oPJdD1H5aavb5_5LBW019C9Flzz5NttSWM-YJB8FM2kHHFjh8TCt9xcUyrHZRKXj-PyejM5EvsbeM2IoA-micrA/s1600/sikinde.JPGBENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Sikinde' inatarajia kuzindua albamu  yake mpya ya 'Jinamizi la Talaka' mwishoni mwa Oktoba baada ya kushindwa kufanya hivyo  mwezi uliopita.
Aidha bendi hiyo inatarajiwa kufanya ziara ya kimuziki katika mikoa ya Morogoro na Dodoma  wiki ijayo kwa ajili ya kuzitambulisha nyimbo zao mpya za albamu hiyo kwa mashabiki wa mikoa  hiyo.
Msemaji Msaidizi wa Sikinde, Emmanuel Ndege aliiambia MICHARAZO kuwa baada ya kukwama  kufanya uzinduzi wao Agosti kama ilivyokuwa imetangazwa, Sikinde sasa inatarajiwa kuzindua  albamu yao mpya katika maadhimisho ya miaka 38 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
Ndege alisema kwa sasa wanaendelea kufanya mchakato wa wadhamini kabla ya kutangaza rasmi  tarehe ya jambo hilo, japo alisisitiza itakuwa mwishoni mwa Oktoba.
"Uzinduzi wa albamu yetu mpya utafanyika Oktoba sambamba na maadhimisho ya miaka 38  tangu kuanzishwa kwa Sikinde," alisema Ndege.
Pia aligusia juu ya ziara ya kimuziki wanaotarajia kuifanya wiki ijayo katika mikoa ya Morogoro na  Dodoma ili kutambulisha nyimbo zao mpya kwa mashabiki wa bendi hiyo wa mikoa husika.
"Tupo katika maandalizi ya kwenda kuzitambulisha nyimbo za albamu yetu mpya katika mikoa ya  Dodoma na Morogoro, tukiwa huko pia tutakumbushia nyimbo za zamani za bendi hiyo zilizoipa  Ubingwa wa Muziki wa Dansi Tanzania," alisema Ndege

No comments:

Post a Comment