Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
Bw. Daniel
Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar s salaam kuhusu utaratibu
wa kutoa nakala za vyeti kwa watahimiwa waliopoteza vyeti vyao ambapo utaratibu
huo unahusisha uchunguzi wa uhalali wa mwombaji. Kulia
ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi na kushoto ni Msaidizi wa Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mitihani la Tanzania Bi Glee Magemba.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mitihani Tanzania
(NECTA) na Vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuonyesha mafanikio ya Baraza hilo nchini.
**************************************
Frank- Mvungi - MAELEZO
Baraza la Mitihani la
Tanzania (NECTA) limedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa Mitihani ya
Taifa na udanganyifu wakati wa Mitihani katika ngazi mbalimbali za elimu nchini.
Mafanikio hayo
yametokana na ushirikiano uliopo kati ya NECTA na kamati za uendeshaji mitihani
katika ngazi za mikoa na wilaya ili kutatua tatizo la wizi wa mitihani ya taifa
na udanganyifu wakati wa mitihani uliokuwa ukifanywa kinyume na taratibu za
baraza la mitihani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza hilo Bw. Daniel
Mafie wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jjijini Dar es salaam uliolenga
kueleza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa.
Akifafanunua Mafie
amesema kuwa katika mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013 watahimiwa
waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 13 tu ikilinganishwa na
watahiniwa 9,736 waliobainika kufanya udanganyifu mwaka 2011.
Aidha Mafie aliongeza
kuwa katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo
kwa kufanya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa na watahimiwa 789 mwaka
2012 na 3,303 mwaka 2011.
Akieleza zaidi kuhusu
mafanikio yaliyofikiwa Mafie alisema Baraza hilo limeweza kusanifu mifumo ya
Kompyuta yenye uwezo wa kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu katika
matokeo ya mitihani ya Taifa.
Katika kukabiliana na
tatizo la watu wanaotumia vyeti vya watu wengine au kughushi vyeti wakati wa
kuomba ajira au nafasi za masomo katika shule mbalimbali ambapo kuanzia mwaka
2008/2009 Baraza hilo lilianzisha utaratibu wa kuweka picha za watahimiwa
katika vyeti vyao.
Katika utaratibu huo
vyeti hivyo viliwekewa alama za kiusalam hali ambayo imesaidia Baraza hilo kuwa
na uwezo wa kubaini kwa haraka na kuwachukulia hatua wale wanaoghushi vyeti au
kutumia vyeti vya watu wengine.
Baraza la Mitihani la
Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyochini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 21 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya
mwaka 1998 na 2002 kwa ajili ya
kuendesha mitihani ya Taifa kwa lengo la kuweka misingi ya sera ya mitihani,
kuendesha mitihani na kutunuku stashahada mbalimbali na vyeti kwa watahiniwa
wanaofuzu na kufaulu mitihani iliyo chini yake kisheria.
No comments:
Post a Comment