Kiungo
wa timu ya Simba SC, Jonas Gerald Mkude (katikati) akisani mkataba mpya
mbele ya Rais wa Simba , Evans Aveva (kulia), Zachalia Hans Pope
(kushoto)
Jonas
Gerald Mkude (katikati) akiweka saini ya dole gumba katika mkataba mpya
mbele ya Rais wa Simba , Evans Aveva (kulia), Zachalia Hans Pope
(kushoto).
KIUNGO
wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude amesaini mkataba wa miaka miwili
kuendelea kuichezea Simba SC na kusema bado nipo sana Msimbazi.
Akizungumza
baada ya kusaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi
wa Silver Pippe, Kawe, Dar es Salaam Mkude amesema kwamba amesaini
klabu hiyo baada ya kufikia kiwango cha fedha alichotaka.
Mkude
mwenyewe hakusema ni kiasi gani amepewa, lakini habari ambazo mtandao
huu mezipata zinasema kiungo huyo amepewa Sh. Milioni 60, ingawa
mwenyewe alianzia Milioni 80.
No comments:
Post a Comment