Andrew Chale (kulia) akiteta jambo na 'Mwenyekiti' Maggid Mjengwa wa Mjengwa Blog.
..Ni vya 'Who Is Andrew Chale', 'Nimnukuu Nani?' na ''Mimi ni Historia',
Na Mwandishi Wetu
Mwandishi wa Habari nchini Tanzania,
Andrew Chale anayeandikia magazeti ya Tanzania Daima na Sayari
yanayotolewa na kampuni ya Free Media ya jijini Dar es Salaam, ambaye
pia mwandishi 'msaada' wa blog za habari mbalimbali za hapa nchini na
nje ya Tanzania ameanza mchakato rasmi wa kuandika vitabu vitatu (3)
vitakavyokuwa vikielezea juu ya Maisha yake.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa
vyombo vya habari leo Novemba 19, Andrew Chale alibainisha juu ya
kusudio hilo la kutoa Vitabu vya kuelezea Maisha yake ni ndoto
aliyonayo kwa miaka mingi na kwa sasa imetimia.
"Wengi watajiuliza sasa nimepata
wapi ujasiri wa kufanya jambo hili kubwa la kuelezea Maisha yangu?.Ni
rahisi sana, Unapokuwa na Mungu kila jambo linawezekana hivyo vitabu
hivi vitakuwa ni muongozo kwa Vijana wote hapa Duniani kuelewa kuwa yale
yote wanayopitia si ya kuyakatia tamaa, bali kuangalia wapi wataweza
kujikomboa na hata kuendana na hali iliyopo kwa kujithamini, kujielewa,
uvumilivu na kufikia malengo stahiki ya maisha" alifafanua Andrew Chale.
Alivitaja vitabu hivyo kuwa ni: "Who
Is Andrew Chale?" Sehemu ya Kwanza), 'Who Is Andrew Chale 2?"-
'Nimnukuu Nani?' (Sehemu ya Pili) na Kitabu cha mwisho
kitakachojulikana kama "Mimi ni Historia".
Akifafanua vitabu hivyo vya 'Who Is
Andrew Chale' cha kwanza na kile cha pili cha 'Who Is Andrew Chale 2-
'Nimnukuu Nani?', alibainisha kuwa vitaelezea kwa kina Historia yake
tokea kuzaliwa hadi alipofikia sasa huku cha Pili cha 'Who Is Andrew
Chale 2-'Nimnukuu Nani' kikielezea yale mambo yote yaliyojificha nyuma
ya pazia na ukakasi wa maisha aliyopambana nayo kutoka kwa walimwengu na
mwishowe anauliza "Nimnukuu Nani?".
Aidha,kwa upande wa kitabu cha :
"Mimi ni Historia" ameweza kuelezea ujumbe juu ya Vijana kutokata tamaa
na baadala yake wasonge mbele kwa magumu yote waliyopitia, ikiwemo yeye.
"Mimi ni Historia", mimi mwenyewe
naogopa sana, kwanza kuanzia jina la Kitabu, Nakumbuka nilimuuliza Mama
yangu Mzazi juu ya jambo fulani la kifamilia baina yake na Baba, lakini
jibu alilonipa ndilo lililonifanya nishike neno hili 'Mimi ni
Historia'. Kikubwa kwenye kitabu hichi nitafafanua mambo mbalimbali ya
kihistoria bila shaka hata atakayesoma ambaye alipitia mambo kama yangu
naye itakuwa ni Historia" alimalizia Andrew Chale.
Vitabu hivyo vyote vitajaa Historia
ya kweli, itakayotoa mafunzo kwa kila mmoja atakayebahatika kuvisoma Pia
vitakuwa ni kama mafunzo, mfano wa kuigwa, na kukuacha ki mdomo wazi na
hata kububujikwa machozi.
Aidha, Andrew Chale, aliomba
ushirikiano kwa wadau kujitokeza kumsapoti ilikufanikisha juhudi za
vitabu hivyo ikiwemo gharama za kuandaa Mswada, mapitio na uchapaji.
"Kwa sasa nipo katika andalio la
Simulizi, na lengo kuu nije nichapishe Mkuki na Nyota.Kwa sasa natafuta
watu watakao kuwa msaada wa awali wa kufanikisha dhumuni langu hili
Ikiwemo ushahuri, msaada wa kifedha, mchango wa kimawazo na mengineo.
Tuwasiliane kupitia 0719076376 au 0767076376 au 0688076376 au chalefamily@yahoo.com" alimalizia Andrew Chale.
Andrew Chale, ambaye kwa sasa
anaishi Bagamoyo, Mkoani Pwani akifanya shughuli zake hizo za Uandishi
wa Habari, Pia ni Mwanaharakati wa Haki za Watoto nchini, msanii wa
masuala ya Vichekesho, Mtunzi wa filamu, maigizo na mshahuri kwenye
matamasha ya sanaa na Muziki, mbali hayo pia ni Mjasiriamali katika
Sanaa na Utamaduni ikiwemo kukuza Sanaa na Utamaduni kwa Mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment