Sunday, November 16, 2014

REDBULL WAMLETA BINGWA WA KUPIGA MISELE NA PIKIPIKI KUTOKA AFRIKA KUSINI


MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia chombo cha moto Pikipiki  Bryan Capper yuko nchini kwa mwaliko maalum akitoka nchini kwao Afrika kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.
Akizungumza leo asubuhi  katika viwanja vya Coco Beach  Jijini Dar es Salaam ambako ndiko alikoanza kuonesha onyesho lake la kwanza  na kuonesha umahiri wake katika uendeshaji wa pikipiki  yupo nchini kwa kudhaminiwa na Kampuni ya Red Bull, atakuwa nchini kwa ziara ya  siku tatu.
Kesho  Jumapili atakuwa katika viwanja vya Mlimani City na  Jumatatu atahitimisha ziara yake katika eneo la Ubungo Tanesco.
Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini Tanzania  pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.
Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club , Blagina Mwihava alisema kwamba wamemleta  mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto.    
 “Hii itakuwa ni shoo kwa watanzania  ili waweze kuvutika kucheza mcheo huu wa aina yake .

Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans  inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini maonesho hayo yote  ni ya wazi.
KAMPUNI YA MAFUTA YA ENGEN YAADHIMISHA MIAKA 21 TANGU KUANZISHWA KWAKE Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania leo Novemba 14,2014 wameungana na wafanyakazi wenzao Barani Afrika kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo.Engeni ni Kampuni iliyojikita katika uuzaji wa Mafuta bora ndani na nje ya Tanzania,huku ikiendelea kujivunia kwa Ubora wake.Pichani ni Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo ya Engen hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo lao Kurasini jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania,Mubita Akapelwa (wa pili kulia) akikata keki wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo. Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo akichua kipande cha Keki iliyokatwa vyema na Dada Jullieth Lwato (alieshika sahani) wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.

Make Money at : http://bit.ly/adflywin

3 comments:

  1. If you are interested in generating money from your traffic with popunder ads - you can embed one of the most established networks - PopCash.

    ReplyDelete
  2. hop over to this website browse around these guys right here go to website this article my sources

    ReplyDelete