Sehemu
wa wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu
(HREDP), wakiwa katika hafla hiyo.
|
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akihutubia wakati wa hafla hiyo. |
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza wakati wa hafla
hiyo.
|
Mwenyekiti wa HREDP, Abubakar Rakesh akizungumza wakati wa hafla hiyo. |
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (kushoto), akitoa ufafanuzi
wa jambo kwa Naibu Waziri Makamba.
|
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikagua kioski
baada ya kukabidhi.
|
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwatunza pesa
wanamuziki ya walemavu ya Bendi ya Tunawajali, iliyokuwa ikitumbuiza katika
hafla hiyo.
|
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akijadiliana jambo na baadhi
ya wanachama wa HREDP.
|
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Kuwapatia vioski vya biashara na mtaji kuanzisha biashara
· Kuwawezesha
kujiinua na kuwa wajasiriamali
Katika
kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo imekabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye
ulemavu yenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali.
Sambambal
na hilo Airtel pia imewapatia mtaji wa kuanzisha biashara ili kuwawezesha
watakao nufaika na vibanda hivyo kuwa mawakala wa huduma ya Airtel money na
kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo
vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Saalam.
Akiongea
wakati wa hafla ya makabidhiano , Naibu Waziri wa mawasiliano Mh. Januari
Makamba alisema” tunapenda kuwashukuru Airtel kwa kutanua wigo na kutoa
msaada kwa watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Serikali yetu iko makini katika kuhakikisha kila mtanzania anapata haki sawa
bila kubagua makundi natoa fulsa sawa katika maeneo mbalimbali.
Sisi
kama Serikali tunaamini msaada mliopokea leo utakuwa chachu ya kuleta maendeleo
ya kiuchumi na nyenzo kwa wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo
ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu kujikwamu na tatizo la kiuchumi unaowakumba
makundi mengi kama haya katika jamii”.
Sera
ya serikali kwa walemavu inalenga kuboreshea mazingira watu wenye ulemavu na
kuwahusisha katika shughuli za uzalishaji ili kuinua uchumi na kutumia kwa
ufanisi rasilimali zilizopo katika kuboresha huduma. Naaamini kwa Airtel
kuwekeza kwenye jamii leo hakutachangia kuboresha maisha ya wengi tu bali
kutachangia kutekeleza na kutilia mkazo agenda za Serikali.
Nachukua
fulsa hii kuwaomba makampuni mengine na wadau mbalimbali kushirikiana na
serikali katika kutoa misaada ya muda mrefu na endelevu katika makundi mengine
kama haya nchini kama ilivyofanywa na Airtel leo”. Aliongeza Makamba.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bibi Beatrice Singano alisema “
kwa mara nyingine tena tumefikia jamii kupitia mpango wetu wa huduma kwa jamii
tukiamini kwa kufanya hivi tunachangia na kusaidi familia za wanachama wa
Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu ,
pamoja na kuinua uchumi kwa watu wenye ulemavu kwa ujumla. Airtel tunatoa fulsa
na kuwawezesha wale waliokuwa na ndoto za kumiliki biashara zao kuweza
kuzifikia ndoto hizo na kujikita kwenye ujasiriamali na biashara.
Tunaamini
Msaada huu haujalenga kuwapatia mtaji tu bali vifaa vya kuendesha biashara
pamoja na mafunzo ya jinsi ya kuendesha biashara endelevu. Tunauhakika
ushirikiano tulioanzisha leo utawaweza wanachama wa kikundi hiki kuwa sehemu ya
kutoa huduma zetu na hivyo kupata faida itakayowawezesha kuwa wajasiriamali
bora nchini’
Tunawaasa
wale wote watakaofaidika na msaada huu leo kutumia vibanda hivi kwa ubunifu na
kuhakikisha vinawanufaisha kufikia malengo
yao ,bado tutaendelea kushirikiana pamoja
nanyi na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha tunatimiza lengo letu la kuboresha
maisha ya watanzania kupitia huduma na bidhaa zetu za kibunifu na fursa za kibiashara’ aliongeza Singano.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi
kwa watu wenye ulemavu Bw. Abubakar Rakesh alisema” tunayofuraha kuona baadhi
ya wenzetu wakiwezeshwa kupata rasilimali muhimu za kuanzisha biashara.
Tunawashukuru
Airtel kwa msaada huo na kwa kukiwezesha kikundi hiki kuwa cha kwanza kupata
msaada kama huu . Wito wangu kwa wanachama wenzangu ni kutumia nafasi hii
vizuri, kuweka jitihada katika kazi zao ili kufanya vyema na kufanikiwa
katika biashara zao”
“Napenda
kutoa shukrani zangu za pekee kwa serikali na kwa Mh Makamba,kwa mchango wake
na kujitolewa kwake kuwasaidia watu wenye ulemavu” aliongeza Rakesh
No comments:
Post a Comment