Wednesday, December 17, 2014

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA AKABIDHI VIFAA VYA KUZIMIA MOTO.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vya kuzima moto pamoja na makoti ya kujikinga na kemikali, kutoka kwa Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose (kulia). akikabidhi msaada wa vifaa hivyo ambavyo tayari vimeingia nchini kwenye kontena maalumu pia kuna kofia ngumu kwa ajili ya Jeshi la Polisi, pamoja na aina mbalimbali ya mabuti jeshi, suruali maalumu kwa ajili ya kupambana katika matukio mbalimbali na viatu vya kiume na kike. Kushoto ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paulo Chagonja na Kaimu Kamishna Operesheneni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Christom Manyologa ambao walikabidhiwa vifaa hivyo baada ya kupokelewa na Waziri Chikawe katika ukumbi wa wizara hiyo.   
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimshukuru Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, kwa msaada wa  vifaa mbalimbali vya kuzima moto pamoja na makoti ya kujikinga na kemikali ambayo vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kukabiliana na matukio mbalimbali nchini. Picha zote na Felix Mwagara Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment