Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma .
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo
na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa
katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne,
alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi
alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha
na Jumanne Juma .
NA MWANDISHI WETU
MISS
Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo,
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, jana ilitoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha
Kulea Yatima cha Extrem kilichopo Tandare kwa Bi Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar
es Salaam.
Mrembo
huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti inayojihusisha na masuala ya
urembo, alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya
kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na wengineo
wanaioshi nawazazi wao.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na kituo hicho
ambacho huwa hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo.
“Nimefika
hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya watoto kama
hawa, lakini pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya
jamii ya Watanzania,” alisema.
Kidoti
alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi
mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani
nao wana haki ya kuishi na ufurahia maisha kama wengine.
Msaada
aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell, ni mchele, unga wa
sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti.
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa
pongezi kwa Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia
makundi maalum.
Akielezea
changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo wa
kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za
matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji.
No comments:
Post a Comment