Patrick Phiri (kushoto) aliyetimuliwa Simba wiki kadhaa baada ya Yanga kumtimua Marcio Maximo |
Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunovic |
Simba imemfukuza kocha huyo kutokana na kutoridhishwa na matokeo iliyopata timu yao katika msimu huu ikiwamo kipigo cha bao 1-0 ilichopewa na Kagera Sugar mwishoni mwa wiki.
Kocha huyo aliyemrithi Zdravkov Logarusic aliyetimuliwa mapema amekuwa hana matokeo mazuri tangu ajiunge na timu hiyo August mwaka huu.
Hii ni mara ya tatu kwa Phiri kuifundisha Simba tangu ajiunge na timu hiyo August mwaka huu ameiongoza katika michezo 22 na kushinda nane, kati ya hizo ni moja tu ya Ligi Kuu na moja ya Nani Mtani Jembe.
Aidha taarifa zinasema kuwa Mserbia Goran Kopunovic kutoka Polisi Rwanda ndiye atakayeinoa Simba na kocha huyo atawasili kesho Jumatano.
Kocha huyo mpya aliyewahi kuzinoa timu za APR atakuja na msaidizi wake Mnyarwanda Jean Marie Ntagawabila na kumaanisha kuwa hata kocha msaidizi wa Simba aliyekuwa na Phiri, Suleiman Matola naye ameenda na maji katika maamuzi yaliyofikiwa na uongozi wa juu wa Simba.
Simba na Yanga kwa muda mrefu sasa zimekuwa na utamaduni wa kutimua na kuajiri makocha wapya kila mara bila kujali vipindi wanavyokuwa na timu zao, jambo ambalo linadaiwa limekuwa likiwachanganya wachezaji kwa kushindwa kunasa mafunzo ya makocha wanaoletwa na kabla ya kuzoeana nao hutimuliwa.
Bahati mbaya ni kwamba klabu hizo zimekuwa zikitimua makocha hata wakati timu zao zikiwa katika nafasi nzuri tofauti na inavyoshuhudiwa Ulaya klabu zikiwatimua makocha kutokana na timu kufanya vibaya
No comments:
Post a Comment