Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akizindua rasmi Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 jana jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa(Kushoto) akitoa
ufafanuzi wa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa iliyofanywa na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyotumia tafiti za taifa zilizofanyika kwa
kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.Kulia ni Waziri wa Fedha Mh. Saada
Salum Mkuya.
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servicius Likwelile
chapisho la lenye Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka
wa kizio wa 2007 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa takwimu hizo leo
jijini Dar es salaam.
::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.Dar es salaam
Serikali imesema kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2007 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 26.8 ikilinganishwa
na trilioni 20.9 za mwaka 2001, ambapo wastani wa pato la mwananchi
mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi milioni1,186,200/= mwaka 2001
hadi shilingi milioni 1, 561,050/= mwaka 2013.
Akizindua usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum ameeleza kuwa matokeo hayo ni sawa na ongezeko la ukubwa wa Pato la Taifa kwa asilimia 27.8.
Amesema ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi za Serikali kuweka mazingira mazuri na kutengeneza fursa za kuwawezesha wananchi kufanya kazi za kujiajiri na hatimaye kupata kipato halali kwa kazi wanazofanya.
Mh.
Mkuya amesema kuwa kukua kwa uchumi wa Tanzania kumechangiwa na
kujumuishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo Sayansi na Teknolojia
ambako kumetoa fursa kwa wananchi kujiongezea kipato hususan matumizi ya
simu za kiganjani ambazo zimerahisisha mawasiliano na utafutaji wa
masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi.
Amezitaja shughuli nyingine kuwa ni ukamilishaji wa miamala mbalimbali ya kibenki na mikopo ambazo zimekuzwa na sekta ya mawasiliano , kuongeza ajira na kupunguza muda wa kusubiri huduma za malipo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha,
amefafanua kuwa kuongezeka kwa thamani ya Pato la Taifa kunaiongezea
Serikali uwezo kimapato kupitia kodi na kuiwezesha kugharamia ujenzi wa
miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
“Serikali
imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama,
utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya Binafsi ya mwaka 2012 unaonyesha
asilimia 60 ya kaya zote nchini zinapata maji safi na salama hasa
hususan maeneo ya mijini,zaidi ya asilimia 20 ya kaya zote nchini
zinatumia nishati umeme haya ni mafanikio makubwa ya matokeo ya ukuaji
wa uchumi nchini” Amesisitiza Mh. Mkuya.
Akizungumzia
mchango wa Sekta Binafsi katika kukua kwa pato la taifa nchini amesema
kuwa ajira zipatazo laki nne kati ya laki sita katika sekta iliyo rasmi zimepatikana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa imetumia Tafiti za Taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.
Amezitaja
tafiti hizo kuwa ni pamoja na utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya wa
mwaka 2007, Sensa ya Kilimo iliyofanyika mwaka 2008 na Takwimu nyingine
za utawala kutoka katika Wizara na Idara za Serikali.
Aidha,
amefafanua kuwa ukokotoaji wa takwimu hizo umefuata mfumo wa Umoja wa
Mataifa wa kutayarisha takwimu za Pato la Taifa wa mwaka 1993 na 2008
kwa lengo la kuhakikisha kuwa takwimu hizo zinalinganishwa na takwimu
nyingine duniani.
No comments:
Post a Comment