Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya
kuongeza salio kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa
mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL
top-up).
Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya
kuongeza salio kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa
mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL
top-up). Kulia ni Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla.
Kutoka kulia ni Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere, Mkuu
wa Mauzo wa TTCL, William Chamla, Ofisa Habari wa TTCL, Edwin Mashasi
wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya
kuongeza salio kwa wateja wa TTCL kupitia simu za mkononi 'Mobile
Banking'
Ofisa Habari wa TTCL, Edwin Mashasi (aliyesimama) akiwatambulisha
waandishi wa habari (hawapo pichani) maofisa wa TTCL, Kutoka kulia ni
Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere na Mkuu wa Mauzo wa
TTCL, William Chamla kabla ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa
wateja wa TTCL kupitia simu za mkononi 'Mobile Banking'.
KAMPUNI
ya Simu nchini Tanzania (TTCL) sasa imerahisisha upatikanaji wa vocha
zake baada ya kuingia makubaliano kuishirikiano na benki 13 nchini
zinazotoa huduma zake pia kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking)
ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya
mkononi (TTCL top-up).
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Mipango na
Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere alisema huduma hiyo ya kununua salio kwa
njia ya simu kupitia mabenki 13 imeanza kufanya kazi hivi sasa hivyo
mteja wa TTCL anaweza kununua salio lake popote alipo kwa kutumia simu
yake.
Alisema
TTCL imeingia makubaliano ya kiushirikiano katika uuzaji wa muda wa
maongezi kwa benki za Standard Chartered, Akiba Commercial (ACB),
Tanzania Postal Bank (TPB), Exim Bank, Dar Es Salaam Community Bank
(DCB), Mkombozi Bank, KCB Bank pamoja na Bank of Africa ambazo wateja wa
beki hizo wanaweza kununua salio kupitia simu zao popote walipo kwenye
akaunti zao.
“…Jumla ya benki 13 zimeingia ubia wa kibiashara na TTCL kwa ajili ya
kuuza vocha za TTCL kupitia benki zao…hapo juu nimetaja majina ya benki
zote ambazo zinatumika kwa ajili ya kufanya miamala mbalimbali ikiwemo
TTCL TOP-UP,” alisema Bw. Bizere.
Akifafanua
zaidi juu ya huduma hiyo Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla alisema
huduma ya TTCL TOP-UP na Mobile banking ni njia ambayo TTCL imeanzisha
kwa wateja wake kwa ajili ya kuongeza salio la muda wa maongezi kwa simu
za mezani, mkononi na kununua vifurushi vya intaneti hivyo mteja
ataweza kununua salio lake muda wowote na popote.
“…Mteja atakayenufaika na huduma hii ni yule mwenye akaunti ya benki, na
amejisajili katika huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi yaani
'mobile banking'.
Hata
hivyo alisema ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma kwa wateja wa
wao vocha za TTCL pia zinapatikana katika vituo vya Maxmalipo na Selcom
‘wireless Point’ na kwenye Ofisi za TTCL, pamoja na vituo vya huduma kwa
wateja ambako viko katika kila mkoa na wilaya.
No comments:
Post a Comment