Mkuu
wa Kitengo cha Kudhibiti Hali Hatarishi wa Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC), Nicholaus Paul (wa nne kushoto) akikata utepe kuashiria
makabidhiano ya msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3
yaliyotolewa na wafanyakazi wa kitengo cha mikopo ya makampuni cha
benki hiyo kwa Shule ya Msingi Maweni. Hafla ya makabidhiano ilifanyika
shuleni hapo, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.
Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Maweni, Sylvester Roche,
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Martha Silavwe, Mwalimu Mkuu,
Zuhura Mwaliko na baadhi ya wafanyakazi wa NBC.
Meneja
wa Kitengo cha Mikopo ya Makampuni wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC,
Beatrice Musira (kulia) akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya
Msingi Maweni, Msafiri Habakuki, wakati wa hafla hiyo shuleni hapo jana.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maweni, Zuhura Mwaliko (katikati) akimshukuru Mkuu
wa Idara ya Mikopo Mikubwa ya Makampuni wa Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC), Salehe Mohamedi, baada ya kupokea msaada huo. Kulia ni Mkuu wa
Usaidizi wa Biashara na Ukusanyaji wa Mikopo wa NBC, Faith Majiwa.
Mmoja
wa wafanyakazi wa enki ya NBC, Noela Ishebabi (kulia) akiwapa
viburudisho wanafunzi wa shule hiyo wakati wa hafla ya makabidhiano ya
madawati shuleni hapo jana.
Baadhi
ya wanafunzi waShule ya Msingi Maweni wakiimba kwa furaha wakati
wakipokea msaada wa madawati kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC),
shulenihapo, Kigamboni, Dar es Salaam jana.
Baadhi
ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha na mmoja wa wanafunzi wa shule
hiyo mara baada ya kuwasili shuleni hapo, Kigamboni nje kidogo ya Jiji
la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment