Thursday, January 22, 2015

OFISI YA BUNGE YAKABIDHIWA MSAADA WA VIFAA VYA TEHEMA NA SERIKALI YA CHINA


 Mkurugenzi wa Mipango na Tehama wa Ofisi ya Bunge Sigfred Kuwite akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.
 Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akieleza vifaa vilivyokabidhiwa na Serikali ya China kupitia Ubalozi wake wa hapa nchini kwa ajili ya kusaidia Bunge kutekeleza majukumu yake. Vifaa hivyo vinathamani ya Dola za Kimarekani 100,000/=
 Balozi wa China hapa Nchini  Mhe. Dkt. LU Youquing akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vya TEHAMA kwa Ofisi ya Bunge.
 Mazungumzo yakiendelea.
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge Balozi wa China hapa Nchini  Mhe. Dkt. LU Youquing mara baada ya hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea kutoka kwa Balozi wa China hapa Nchini  Mhe. Dkt. LU Youquing baadhi ya Vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa serikali ya China kwa ajili ya kusaidia shughuli za Bunge. Vifaa hivyo vyenye thamani ya Dola za Kimarekani laki moja vimekabidhiwia leo katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Spika jijini Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Balozi wa China hapa Nchini  Mhe. Dkt. LU Youquing na viongozi wengine wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA. Picha na Owen  Mwandumbya.

No comments:

Post a Comment