Monday, March 2, 2015

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' ANYAKUWA UBINGWA WA U.B.O AFRICA KWA KUMTWANGA COSMAS CHEKA

 

 

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O Africa mpambano uliofanyika jumamosi ya jana Class alinyakuwa ubingwa huo kwa kushinda kwa Point na sasa Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Africa W.P.B.F na U.B.O Africa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' askiwa na mikanda yake ya ubingwa wa Africa wa U.B.O na WPBF
Bondia Fadhili Majiha kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Majiha alishinda mpambano huo kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O Africa mpambano uliofanyika jumamosi ya jana Class alinyakuwa ubingwa huo kwa kushinda kwa Point na sasa Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Africa W.P.B.F na U.B.O Africa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Cosmas Cheka akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O AFRICA
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akishangilia ushindi na mashabiki wake baada ya mpambano wake na Cosmas Cheka na kufanikiwa kumdunda kwa point


Na Mwandishi Wetu

BONDIA machachali wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ametwaa ubingwa wa U.B.O Africa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kumtwanga bondia Cosmas Cheka wa Morogoro kwa point mpambano wa raundi kumi lililofanyika katika uwanja wa ndani wa taifa Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita

katika mpambano uho ulioanza kwa mashambilizi kwa kila bondia kumtupia makonde mwenzie kwa ufundi wa  ali ya juu na ulikuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande baada kila mmoja kujiandaa kwa mda mrefu ata hivyo class alibuka mbabe baada ya raundi kumi kwisha

katika mipambano mingine iliyopigwa siku hiyo bondia Fadhili Majiha alimsambalatisha Fransic Miyeyusho kwa point mpambano mwingine uliowakutanisha bondia chipkizi Vicent Mbilinyi aliyepambana na Epson John wa Morogoro mpambano uliomalizika kwa sale

wakati bondia Shedrack Ignas alimpiga bila ya huruma bondia Husein Mbonde kwa K,O ya raundi ya nne ya mpambano wao nae Saidi Mundi akimpiga kwa point bondia Ramadhani Shauri

aidha wadau wa mchezo wa ngumi waliofulika kuona mpambano huo wa kistoria wameomba kuwa mapambano hayo yanatakiwa kuanza mapema kuondoa hadha ya usumbufu wa usafili wakati wa kutoka na kwenda majumbani kwao kwani wapenzi wa mchezo wengi wa masumbwi wanategemea daladala kwa usafiri wa kurudi makwao ambapo ikifika zaidi ya saa sita daladala zinatoweka barabarani

No comments:

Post a Comment