Monday, March 9, 2015

Floyd Mayweather vs Manny Pacquiao



Floyd Mayweather vs Manny Pacquiao






 Pambano la ngumi linalosubiriwa kwa hamu

Bingwa kulamba Euro mil 160

 Pambano kupigwa Mei 2


LOS VEGAS, Marekani

MCHEZO wa ngumi ni kati ya michezo ambayo inapendwa sana ulimwenguni kutokana  na kuwa uhalisia kwa kiasi kikubwa.

Ni mchezo wa hatari ambao umeshawapa vilema vya baadhi ya viungo wachezaji wa mchezo huo kutokana na kutokuwa makini.

Kwa sasa pambano ambalo ndio limekuwa gumzo kwa mashabiki wa ngumi ulimwenguni, ni kati ya Floyd Mayweather, Jr dhidi ya Manny Paquiao.

Pambano hilo na uzito wa middle linatarajiwa kufanyika Mei 2 mwaka huu katika Ukumbi wa MGM Grand ndani ya Los Vegas.

Kwa kiasi kikubwa mashabiki wa mchezo wa ngumi wanalisubiria kwa hamu pambano hilo kutokana na rekodi zilizopo kati ya mabondia hao.

Ukiangalia kwa upande wa Mayweather ameshapigana mapambano 47 na kushinda yote na kati ya hayo 26 ameshinda kwa KO.

Kwa upande wa Paquiano, ameshacheza mapambano 64 na kushinda 57, K) 38 ambapo amepoteza matano na kutoa sare mawili.

Katika pambano la mwaka huu, lilianza kuadaliwa tangu mwezi Januari baada ya masupastaa hao kukutana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu Miami na kuamua kukaa pembeni kwa ajili ya kuongelea mpambano huo mkali.

Baadaye walikubaliana kwa kubalilishana namba za simu ambapo pia baadaye ilifahamika kuwa wamefikia muafaka.

Pamoja na kuwa walifikia muafaka lakini awali Mayweather hakuwa tayari kulizungumzia pambano hilo kutokana na kuamua kuweka siri, lakini baadaye ilibainika kuwa wameshainishana na kupanga siku ya pambano ambapo waliamua kuanza kuitangaza katika vyombo mbalimbali vya Habari.

Pambano hilo ambalo ndilo litakalokata ngebe za mabondia hao linatarajiwa kuhudhuriwa na umati wa mashabiki ambapo mpaka sasa tiketi zimeshaanza kuuzwa.

Pambano hilo limegubikwa na utata ambapo awali walikuwa wazipige mabondia hao lakini pambano liliahirishwa baada ya Pacquiao kukataa kupima matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu.

Hata hivyo kwa sasa Pacquiao ametamka mwenyewe kuwa anatarajia kumlipa faini ya pauni milioni 3.2 kwa Mayweather kama yeye atashindwa kufaulu katika kipimo hicho safari hii.

Mkataba waliongia kati ya mabondia hao ni pamoja na bingwa kuondoka na dau la Euro milioni 160.

Hata hivyo kwa sasa kumekuwa na tambo za hapa na pale kwa mabondia hao kwa kila mtu kudai kuwa atafanya vizuri, lakini cha msingi ni kusubiria Februari 2 kwa ajili kuona uhondo.

No comments:

Post a Comment