Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya
sh. Milioni 2, mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half
Marathon Ismail Juma baada ya kushinda katika mashindano hayo
yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mkoani Moshi,
katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile
Tiano pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mchezo wa Riadha Mkoa wa
Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kulia) akifurahia jambo na Kaimu
Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano wakati wa
mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja
wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
Washindi
wa kwanza mpaka wa tatu wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, kwa
upande wa wanaume, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa
Leonidaz Gama (kushoto), kulia ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za
Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama
Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage pamoja na na Mwenyekiti wa Chama
Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
Kaimu
Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili
kushoto) akisoma risala katika mashindano ya fainali ya mashindano ya
Tigo Kili Half Marathon, iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha
Ushirika Mjini Moshi, wa kwanza kushoto ni Ofisa Mawasiliano wa Tigo
John Wanyancha, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama
pamoja na Makamu Mwenyekiti wa RT William Kalage na Mwenyekiti wa KAA
Liston Metacha.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya simu ya Tigo Diego Gutierez (kushoto) akizungumza na
Kaimu wake Cecile Tiano (katikati) pamoja Mkurugenzi wa Kanda ya
Kaskazini David Charles kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half
Marathon yaliyofanyika juzi Mkoani Moshi.
Kaimu
Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili)
kushoto, akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo kabla
ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon iliyofanyika juzi
kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
Washindi
wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya
Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo
cha Ushirika Mjini Moshi.
Washindi
wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya
Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo
cha Ushirika Mjini Moshi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya
sh. 500,000 mshindi wa tatu Vicoty Chepkemei, baada ya kuibuka mshindi
katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanawake
katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha
Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya
Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama
Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa
Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya
sh. Milioni 1 mshindi wa pili wa mashindano Tigo Kili Half Marathon,
Eunice Echumba, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja
wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na
Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya
sh.500,000 mshindi wa tatu Theophil Joseph, baada ya kuibuka mshindi
katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa Wanaume,
katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha
Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya
Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama
Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
No comments:
Post a Comment