Saturday, November 28, 2015

KOCHA SUPER D AMNOWA BONDIA IBRAHIMU CLASS KING CLASS MAWE


Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimfanyisha mazoezi ya nguvu  na kujenga misuli bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro desemba 25 Picha na SUPER DBOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akifundishwa jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'UpCat' wakati wa mazoezi ya bondia huyo kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro Picha na SUPER DBOXING NEWS



Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' juu akimfanyisha mazoezi ya misuli ya shingo kupandisha na kushusha shingo uku akiwa juu ya bondia  Ibrahimu Class 'King class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano ya kitaifa na kimataifa ya bondia huyo Picha na SUPER DBOXING NEWS 
Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amendelea kuwamwagia sumu mabondia Ibrahimu Class 'king Class Mawe' na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro


wakati Class akimvaa Twaha Kassimu bondia vicent Mbilinyi atavaana na bondia mkongwe kabisa Deo Njiku wa Morogoro


akizungumzia mazoezi ambayo anampa bondia bigwa wa mikanda miwili ya U.B.O na WPBF Afrika Ibrahimu Class ambapo kwa sasa anamfanyisha mazoezi ya kumjengea nguvu pamoja na akili kwa ajili ya mchezo wake ujao


ambapo amekuwa akimfanyisha mazoezi mbalimbali ya nguvu yakiwemo ya kujenga misuli ya tumbo pamoja na shingo ambapo bondia huyo kwa sasa anafanya mazoezi mara tatu kwa siku na kusimamiwa vizuri


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment