BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine feb 26 akizipiga na Michael Camellion kutoka Philippinesa mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
Kimweri mpaka sasa amepanda
uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa
ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
bondia huyo mtanzania anaefanya
shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya
mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo uho
atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA
kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana
na akishinda mchezo uho
itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa
wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na
mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii
ya feb 26
Kimweri alitoa shukrani za
kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka
sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni
Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli ,
Rajabu Mhamila 'Super D'
Kocha wa Tanzania Prison Remmy
Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa
pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge
Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga
ambao amekuwa chachu katika
mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama
anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake
ndipo kilipozikiwa
|
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto) akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi kocha wa Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini |
Friday, January 29, 2016
BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA UWANJANI FEB 26 AUSTRALIA
MABONDIA KUTWANGANA DAR LIVE MARCH 12
Mabondia Iddi Mnyeke kushoto na Mohamed Kashinde wakiangaliana kwa usongo wakati wa utambuklisho wa mpambano wao utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA mbalimbali watazitwanga march
12 katika ukumbi wa Dar live mbagala akizungumza mbele ya waandishi wa
habari mratibu wa mpambano uho
Rajabu Mhamila 'Super D' amewasainisha
mabondia mbalimbali kuzipiga siku hiyo ambapo bondia Ibrahimu Maokola
'Simba wa Mbagala' atazipiga na Joseph Sinkala kutoka Mbeya mpambano wa
ubingwa raundi kumi kg 74 utakaosimamiwa na kamisheni ya ngumi za
kulipwa 'TPBC' kinachongozwa na Rais Chaurembo Palasa
aliendelea kwa kusema siku hiyo bondia
Iddi Mnyeke kg 61 atamenyana na Mohamed Kashinde wakati Pius Kazaula
kutoka Morogoro atakumbana na Karage Suba katika uzito wa kg 66
wakati Shabani Kaoneka atakumbana na
Said Seleman mpambano wa raundi sita kg 72 na Ambokile Chusa atavaana na
Seleman Galile katika mpambano wa raundi sita kg 74
pia kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayo sindikiza mpambano uho
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo mpya
za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd
mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd
Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
Monday, January 25, 2016
DARAJA LA KIGAMBONI KUANZA KUTUMIKA RASMI MACHI MOSI
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph
Nyamhanga (wa nne kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi na Meneja Mkuu wa
mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa Hifadhi ya jamii
(N.S.S.F) Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara ya kushtukiza
iliyofanywa na Katibu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Msimamizi
na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa
Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo, akimuonesha Katibu Mkuu Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (wa
kwanza kulia) sehemu ya kipande cha km
1.5 kilichopo upande wa Kigamboni kwa ajili ya upanuzi wa daraja hilo.
Mwonekano
wa Ofisi za Daraja la Kigamboni zitakazotumiwa na wasimamizi wa daraja hilo
linalotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka huu.
Lango
la kuingilia daraja la Kigamboni linavyoonekana, pembeni ni ofisi za huduma
mbalimbali zitakazokuwa zinatolewa darajani hapo.
Sehemu
ya juu ya daraja la Kigamboni, likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
DARAJA
LA KIGAMBONI KUANZA KUTUMIKA MACHI MOSI
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano sehemu ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amesema daraja la Kigamboni
litaanza kutumika kuanzia Machi mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kukagua hatua
za ujenzi wa daraja hilo Eng. Nyamhanga amemtaka msimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha
hatua ya ujenzi iliyobaki inakamilika katikati ya mwezi februari na kuanza kazi
mwanzoni mwa mwezi Machi.
“Hakikisheni Machi mosi magari yaanze
kupita rasmi kwenye daraja hili na hivyo kufungua ukurasa mpya kwa wakazi wa Kigamboni
ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na msongamano katika eneo la Magogoni”,
amesema Eng. Nyamhanga.
Eng. Nyamhanga amesisitiza kuwa Serikali
inaangalia uwezekano wa kuunganisha daraja la Kigamboni na barabara ya Charambe,Mlandizi
hadi Chalinze ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji.
Amemtaka meneja wa mradi wa ujenzi wa
daraja hilo toka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. John Msemo kuhakikisha
anatafuta Wakala makini atakayesimamia na kuendesha mradi huo.
Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita
680, unasimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano linatarajiwa kuishi
zaidi ya miaka 100 na kuwa na uwezo wa kupitisha mizigo ya tani 56
zinazokubalika katika nchi za jumuiya ya madola.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
Wauzaji bidhaa holela soko la Buguruni wapigwa marufuku
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala yapiga marufuku uuzwaji holela wa bidhaa katika
soko la Buguruni unaochafua mazingira ya soko na kuhatarisha afya za
walaji.
Hayo
yamesemwa leo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala David
Langa wakati akifafanua kuhusu kero ya wauzaji holela wanaopanga bidhaa
chini katika soko la Buguruni.
“Bidhaa
zinazopangwa chini katika soko la Buguruni sio rasmi na hakuna
utaratibu unaoruhusu wauzaji kufanya biashara hiyo, hivyo natoa
tahadhari kwa wale wote wenye tabia hiyo kuwa ni marufuku kufanya
biashara ya kupanga bidhaa chini na sio kwa soko la Buguruni tu ila
katika masoko yote yaliyopo katika manispaa yetu” Alisema Langa
Afisa
langa amesema kuwa wapo maaskari wanaolinda na kuthibiti uuzwaji holela
wa bidhaa katika soko hilo ila wauzaji wamekuwa wakifanya mchezo wa
kuwavizia maaskari pindi wanapoondoka ndipo wanapanga bidhaa zao.
Ameongeza
kuwa suala hili limekuwa sugu katika masoko mengi na njia ya
kukabiliana na changamoto hii ni kuongeza askari wengi watakaokaa muda
wote ili waweze kukabiliana na wauzaji holela.
Aidha
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Maafisa Afya
inafatilia kwa karibu masoko yote ili kufatilia kama wauzaji
wanazingatia kanuni za afya kwa kuweka mazingira safi ili kuokoa afya za
walaji.
WAKAZI WA KATA YA NAMAYUNI WAPONGEZA MTANDAO WA SIMU ZA MKONONI WA HALOTEL.
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Halotel ndio mtandao pekee unaotoa huduma za
mawasiliano kwa njia ya Simu za mkononi katika kata ya Namayuni iliyopo
Kilwa Masoko Mkoani Lindi.
Mtandao
huu ndio unawasaidia wakazi wa kata ya Namayuni kuweza kuwasiliana na
ndugu na jamaa wa maeneo hayo na sehemu nyingine kwa njia ya simu ya
mkononi kwa kuwa wamejengewa mnara unao wawezesha kuwasiliana kwa njia
simu za mkononi.
Diwani
wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura
amepongeza mtandao wa simu za mkononi wa Halotel na kusema kuwa
umeisaidia sana jamii ya wakazi wa kata ya Namayuni mkoani humo kutokana
na hapo awali kutokuwepo na mtandao wowote wa simu.
"
Tunawashukuru sana Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kukumbuka kama
kunaviumbe huku na kutuwekea mnara katika kata yetu kwakua kabla ya
mtandao huu tulisafiri na kupanda juu ya vilima ili kutafuta
mtandao(network) ili tuweze kuwasiliana na watu wengine kwa njia ya
simu."
Nao
wakazi wa Kijiji cha Namayuni wamesema kuwa Mtandao huu wa Halotel
"umetusaidi sana katika huduma mbalimbali hasa kutufichia siri katika
mawasiliano kwani tulikuwa tunaenda umbali mrefu kwenda kutafuta
mtandao, kwa sasa tunakaa ndani tuu na tunawasiliana na ndugu na jamaa
bila mtu yoyote kujua kama tumewasilana na nani".
Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.
Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.
Wanafunzi
wakisoma kupitia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti ya spidi kubwa
walizopewa na kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel katika shule ya
sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mtaalamu
wa masuala ya mtandao wa kampuni ya Halotel, Kilwa Masoko Mkoani
Lindi, Sebastian Inocent akifafanua changamoto mbalimbali zinazo wapata
wakazi wa kijiji cha Namayuni.
Afisa
habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank
Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata
ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa
kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.
Wakazi wa Kijiji cha Namayuni wakipata maelekezo walipo tembelea kibanda cha kusajili laini jijini hapo.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata mkoani Pwani, Abdala
Sakasa akizungumza wakati wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi ya
Halotel walipotembea katika shule hiyo kujionea jinsi wanafunzi
wanavyotumia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti yenye spidi ya kazi
ili kusaidia wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Lugoba hasa wa kidato
cha tano na cha sita kwa kusoma na kuongeza uwezo wao katika masoma
kutokana na wanafunzi hao kukosa baadhi ya vitabu. Wanafunzi wa shule
hiyo wamefurahia uwepo wa mtandao wa Halotel kwani ndio mtandao pekee
uliochelewa kufika hapa nchini na kuweza kutoa kompyuta 19
zilizounganishwa na intaneti katika shule hiyo.
Mwalimu
wa somo la Kompyuta na maswala ya mawasiliano(ICT), Emmanuel Mhizi
akifafanua jambo mbele ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya
Halotel walipotembelea shuleni hapo mkoani Pwani. Mwalimu wa Kulia ni
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba, Benjamini Nyamatwema.
Mhizi
amesema kuwa wanachangamoto kubwa katika kupanga zamu za wanafunzi wa
shule hiyo kwani shule hiyo inawanafunzi 1391 na kompyuta zenye intaneti
ni 19 tuu, kwa mujibu wa ratiba ya wanafunzi kuingia kwenye chumba
hicho wanaingia wanafunzi 30 kwa kila kipindi ili kila mwanafunzi aweze
kuingia katika chumba cha kompyuta.
Wanafunzi
wakiwa katika Darasa la kompyuta ambalo Kampuni ya Halotel walijitolea
kwa kuwapa kompyuta hizo pamoja na kuwaunganishia Intaneti spidi kubwa
ya bure kwa miaka mitatu mfurulizo iki kuweza kuwasaidia wanafunzi hao
katika kujisomea machapisho mbalimbali yaliyopo kwenye mitandao
mbalimbali.
Mwalimu
wa somo la Kompyuta na maswala ya mawasiliano(ICT), Emmanuel Mhizi
akiwakagua wanafunzi kwa uangalifu katika darasa hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lugoba akiendelea kujisomea somo alilolifungua walipotembelewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Halotel mkoani humo.
Walimu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani wakijadiliana jambo wakati wanatembea.
Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa kijiji cha Namayuni mkoani humo walipotembelewa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel ambayo ndio mtandao pekee uliowafikia wananchi na wakazi wa kata hiyo.
Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa kijiji cha Namayuni mkoani humo walipotembelewa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel ambayo ndio mtandao pekee uliowafikia wananchi na wakazi wa kata hiyo.
Wakazi wa kata ya Namayuni na wanakijiji cha Namanyuni wakimsikiliza Diwani
wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura
mara baada ya kutemelewa na wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi yz
Halotel mkoani humo.
Mkazi
wa Kijiji cha Namayuni akizungumza na simu wakati amekaa akitumia
mtandao wa simu wa Halotel akiwasiliana na mtu aliyepo Zanzibar bila
kwenda kupanda kwenye kilima kama zamani.
Aidha
mzee huyo alielezea furaha yake kwa ujio wa mtandao wa Halotel
unavyowasaidia na kuwafichia siri zao, kwani mwanzoni kila mtu alijua
kuwa ndio anaenda kuongea na simu na mpaka kusababisha kuaga na kwenda
umbali furani kwaajili ya kutafuta netiweki ili aweze kuzungumza na mtu
ambaye anamtafuta.
Mwenyekiti
wa Kijini cha Namayuni, Ally Mtumbwe akizungumza na waandishi wa habari
Kilwa Masoko Mkoani Lindi kata ya ya Namayuni kijijini cha namayuni
mara baada ya wafanyakazi wa mtandao wa Halotel kutembelea kijijini
hapo.
Mkazi
wa Kijiji cha Namayuni akielezea jinsi mtandao huo ulivyorahisisha
biashara kutokana na kujengewa mtandao wa Halotel amesema kuwa mtandao
huo umewasaidia kwa kuagiza bidhaa anazozihitaji ukitofautisha na zamani
ambapo ilibidi kuzifuata hata kama hajui kama bidhaa anayoitaka ipo au
haipo, hata hivyo amesema kuwa Halotel imewasaidia kuokoa muda sana.
Mkazi wa kijiji cha Namayuni akiuliza swali kuhusiana na mtandao huo kuhusiana na kama unaweza kutuma pesa au kupokea pesa.
Watoto wa Kijijini cha Namayuni wakipata picha na mwandishi wa gazeti la The Citizen kijijini hapo.
Afisa
masoko wa kampuni ya Halotel , Charle anayepiga picha kwa simu akiwa na
baadhi ya waandishi wa habari katika kijini cha Namayuni, Klwa Masoko
mkoani Lindi.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
MATUKIO MBALIMBALI BUNGENI MJINI DODOMA.
Waziri
Mkuu, Kassim Majalaliwa akisalimiana na Mbunge wa Nkansi Ally Kessy
kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majalaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbozi Magharibi,
David Silinde kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016.
Katikati ni Mbunge wa Nkansi, Ally Kessy.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo
kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee kutoka jimbo la
Chemba Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Januari 25,2016. Kushoto kwake
ni Mbunge wa Chemba Juma Nkamia.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BONDIA FRANSIC CHEKA ATUA NCHINI NA KUMPIGIA MIKWALA MSERBIA GEARD AJOTOVIC
Bondia
Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani
juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo aliweka kambi nchi ya
Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia
Geard Ajetovic kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa
habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo
aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia
Geard Ajetovic kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi
wetu
Dar es
Salaam. Bondia Francis Cheka amerejea nchini kutoka Zambia na kusema Mserbia
Geard Ajetovic aiandae kupokea kipigo kikali katika pambano lao la mabara la
uzito wa super middle la Shirikisho la
Masumbwi ya Kulipwa Duniani (WBF).
Cheka na
Ajetovic watapambana kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 katika pambano
lililoandaliwa na kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion.
Akizungumza
jana, Cheka alimpongeza meneja wake,
Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited kwa kumwezesha kuweka
kambi nje ya nchi ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo kwa
upande wake.
Alisema kuwa
Ndambile na kampuni yake imeonyesha kuwa wanajali na wanamalengo makubwa ya
kumwendeleza kutokana na ukweli kuwa amekaa katika kambi ya kisasa yenye
mabondia na makocha wazuri nchini Zambia.
“Kwanza
naishukuru kampuni ya Advanced Security Limited kwa kufanikisha kambi hii,
nimejifua vya kutosha nchini Zambia, mazoezi yalikuwa magumu na yalihitaji uvulivu
mkubwa, kwa kutambua lengo langu ni nini, nilifanya kwa juhudu zote na sasa
nipo tayari kwa pambano, hata kesho (leo) nipo tayari kwa bondia yoyote
duniani,” alisema Cheka.
Alisema kuwa
kutokana na siku kuwa nyingi, ataendelea na mazoezi hapa hapa nchini huku
akisubiri mipango mengine ya meneja wake kwa upande wa maandalizi.
Meneja wa
Cheka, Juma Ndambile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced
Security Limited alisema kuwa lengo la
kampuni yao ni kufanya mapinduzi na kuleta maendeleo katika mchezo wa ngumi za
kulipwa hapa nchini.
Ndambile
alisema kuwa Cheka ni bondia mwenye kipaji na hakuwa tayari kuona kipaji hicho
kinapotea na kuchukua jukumu la kumwendeleza. “Mimi na kampuni yangu tuna
mipango ya kuwamiliki mabondia wengi hapa nchini, kama ilivyo kwa Cheka, nao
watapata fursa ya kufanya mazoezi nje ya nchi na kupata mapambano ya kimataifa
ya ubingwa ili kuiletea sifa taifa,” alisema Ndambile.
Alisema kuwa
wanataka kutumia vizuri fursa waliyopewa na WBF ambayo inamtaka Cheka ashinde
pambano hilo ili aweze kuwania ubingwa wa Dunia hapa hapa nchini.
|
Sunday, January 24, 2016
BONDIA VICENT MBILINYI AENDELEA KUJIFUA NA KUTAFUTA WAPINZANI
VICENT MBILINYI KG 63 TANZANIA 2016 |
Bondia Vicent Mbilinyi akielekezwa jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake yakawaida Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea
kujifua baada ya kumchakaza bondia mkongwe wa siku nyingi Deo Njiku sasa
anaendelea na mazoezi ya nguvu kwa aji ya kuwasambalatisha mabondia
wengine watakaopita mbele yake
bondia huyo mpaka sasa ameshacheza
michezo tisa na kushinda 7 kupoteza na droo 1 ambapo imemuweka katika
rekodi nzuri ya mchezo uho kwa mwaka jana
akizungumza na mwandishi wa habari
hizo Mbilinyi amesema kwa sasa yupo fiti kucheza na mtu yoyote kwa
keshaiva kikamilifu baada ya kupata mazoezi ya aina mbalimbali yanayo
mjengea kujiamini katika mchezo wa masumbwi akiwa chini ya kocha wa
kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D'
aliendelea kwa kusema kuwa nilingia
katika ngumi za kulipwa kama najitolea lakini siku zinavyozidi kwenda
ndio najijengea mashabiki na kujulikana zaidi katika mchezo niupendao
hivyo na ahidi sito waangusha na wala sito lewa sifa wanazonipa
nitaendelea kujifua ili niendelee kupambana zaidi katika mchezo
nae kocha anaemnowa bondia huyo Super D
amesema kuwa Mbilinyi ana moyo wa kufika mbali hivyo ameonesha nia ya
kucheza mchezo uhu katika mazingila magumu hivyo kwa mwaka 2016 ni wake
wa kutoka katika mchezo wa ngumi
na naisi katika uzito wake kwa sasa
akuna wa kumsumbua kwa sababu amekutana na mabondia wa lika zote ambao
wanatamba na waliotamba
Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
sasa anawasimamia mabondia wake akiwemo Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
Shabani Kaoneka, Shomari Milundi, Vicent Mbilinyi Mwenyewe na mwanadada
Lulu Kayage ambao wote wapo chini ya Super D Boxing Promotio ambayo
kazi yake kubwa ni kuwafundisha na kuwatafutia mipambano mbalimbali ya
nje na ndani
MABONDIA ABDALLAH PAZI NA GORGER DIMOSO WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 BAGAMOYO MKOA WA PWANI
Bondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya kutia saini za makubaliano ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Geoger Dimoso akisaini mkataba wa kuzipiga na Abdallah Pazi wa pili kushoto kulia ni mlatibu wa mpambano huo Pembe Ndava na kushoto ni kocha Mbaruku Heri |
Mabondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani katikati ni mratibu wa mpambano uho Pembe Ndava Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Abdallah Pazzi na Gerger Dimoso wamesaini mkataba wa kuzipiga Bagamoyo mkoa wa Pwani March 5 katika uzito wa kg 74
akizungumza wakati wa kutiliana saini
Promota wa mpambano uho Muhusin Sharif amesema kuwa wameamua kupeleka
mpambano uho Bagamoyo kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa pwani wapate
burudani ya masumbwi siku hiyo
aliongeza kwa kusema kuwa anaomba
makampuni mbalimbali kutoa sapoti kwa ajili ya udhamini wa mapambano
hayo kwa kuwa Bagamoyo mchezo huo unapendwa na ndio unachipukia hivyo
anaomba sapoti kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia mchezo uho
ili uendelee kukua hapa nchini
ambapo kwa Bagamoyo atuna jukwaa
'ring' la ngumi ata moja mpaka tukodishe kutoka Dar es salaam yaje hapa
ndio vijana wapate kucheza hivyo naomba wadau mbalimbali wajitokeze
kuchangia upatikanaji wa jukwaa hiro kwa ajili ya mchezo wa ngumi ili
zisonge mbele
siku hiyo mbali na mpambano uho
kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Sadiq
Momba atakumbana na Baina Mazola katika uzito wa kg 59 na Adam Yahaya
atakumbana na Selemani Bagaiza katika uzito wa kg 49 na Juma Khan
atapambana na Bruno Vivuaviwili na Abdallah Zamba atakumbana na Twalibu
Tuwa
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
Wednesday, January 20, 2016
MABONDIA SADIQ MOMBA NA BAINA M,AZOLA WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 TASUBA BAGAMOYO
Mabondia Sadiq Momba kushoto wakitambiana na Baina Mazola baada ya kutia saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani katikati ni promota Muhusin Sharif Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Promota wa mchezo wa masumbwi Muhusin Shsharif katikati akiwa pamoja na mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola mara baada ya mabondia hawo kutiliana saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS |
KIONGOZI TOKA SHIRIKISHO LA MASUMBWI PST PEMBE NDAVA KATIKATI AKISAINI MKATABA WA KUKUBALI KUPIGANA BONDIA BAINA MAZOLA KUSHOTO NA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU |
Promota
wa masumbwi nchini Muhusini Sharif Katyikati akiwainuwa mikono juu
mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola wakati wa kutambulisha
mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa
Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS BONDIA SADIQ MOBA AKITIA SAIN YA KUZIPIGA NA BAINA MAZOLA MARCH 5 KATIKA UKUMBI WA TASUBA BAGAMOYO MKOA WA PWANI WANAOSHUDIA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU NA KIONGOZI TOKA SHIRIKISHO LA MASUMBWI PST PEMBE NDAVA Na Mwandishi Wetu MABONDIA Sadiq Momba na Baina Mazola jana wamesaini mkataba wa kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa Pwani uzito kwa kg 59 akizungumza wakati wa kutiliana saini kwa ajili ya mpambano huo promota Muhusini Sharif amesema ameamua kuwapambanisha mabondia hawo wanaotamba kwa sasa kwenye uzito uho kwa ajili ya kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini unajua Sadiq Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa anafanya vizuri awapo nje ata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand amepigwa kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kurudi nyumbani hivyo anacho itaji ni ushindi na kupigana na mtu mwenye point za kutosha kumrudisha kileleni na Baina Mazola katika uzito wake yeye ni namba tatu katika boxrec nchini hivyo nae anataka kuwa zaidi ya bondia Momba na ndio anatishia amani katika uzito uho kwa sasa nae bondia Momba amesema baada ya kupoteza mpambano wake nje ya nchi sasa wadogo zake wanamtaka kucheza nae kwani inaonekana kiwango changu kimepungua na kudiliki watoto wadogo kunitaka mimi ata ivyo nashukuru uhu mchezo mimi ni kazi yangu naitegemea ivyo nitaakikisha simpi nafasi ata chembe kwa kumpiga kipigo kibaya sana ambacho ajawai kupigwa tanga aanze mchezo wa masumbwi nchini nae bondia Mazola amesema kwa sasa yupo vizuri sana na anawaomba mashabiki zake kuwa na moli ya kwenda bagamoyo ambapo promota kafanya vizuri sana klupereka mpambao huu uko sisi mabondia wote wawili tuna umarufu mkubwa sana maeneo ya manzese na vitongoji vyake ata hivyo nita akikisha nampiga Momba kama begi kwa kuwa sasa ana jipya nimeona stail zake zote anazotumia kupigana sijaona jipya hivyo ajiandae kwa kipigo tu
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengipia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha |