Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph
Nyamhanga (wa nne kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi na Meneja Mkuu wa
mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa Hifadhi ya jamii
(N.S.S.F) Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara ya kushtukiza
iliyofanywa na Katibu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Msimamizi
na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa
Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo, akimuonesha Katibu Mkuu Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (wa
kwanza kulia) sehemu ya kipande cha km
1.5 kilichopo upande wa Kigamboni kwa ajili ya upanuzi wa daraja hilo.
Mwonekano
wa Ofisi za Daraja la Kigamboni zitakazotumiwa na wasimamizi wa daraja hilo
linalotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka huu.
Lango
la kuingilia daraja la Kigamboni linavyoonekana, pembeni ni ofisi za huduma
mbalimbali zitakazokuwa zinatolewa darajani hapo.
Sehemu
ya juu ya daraja la Kigamboni, likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
DARAJA
LA KIGAMBONI KUANZA KUTUMIKA MACHI MOSI
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano sehemu ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amesema daraja la Kigamboni
litaanza kutumika kuanzia Machi mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kukagua hatua
za ujenzi wa daraja hilo Eng. Nyamhanga amemtaka msimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha
hatua ya ujenzi iliyobaki inakamilika katikati ya mwezi februari na kuanza kazi
mwanzoni mwa mwezi Machi.
“Hakikisheni Machi mosi magari yaanze
kupita rasmi kwenye daraja hili na hivyo kufungua ukurasa mpya kwa wakazi wa Kigamboni
ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na msongamano katika eneo la Magogoni”,
amesema Eng. Nyamhanga.
Eng. Nyamhanga amesisitiza kuwa Serikali
inaangalia uwezekano wa kuunganisha daraja la Kigamboni na barabara ya Charambe,Mlandizi
hadi Chalinze ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji.
Amemtaka meneja wa mradi wa ujenzi wa
daraja hilo toka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. John Msemo kuhakikisha
anatafuta Wakala makini atakayesimamia na kuendesha mradi huo.
Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita
680, unasimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano linatarajiwa kuishi
zaidi ya miaka 100 na kuwa na uwezo wa kupitisha mizigo ya tani 56
zinazokubalika katika nchi za jumuiya ya madola.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
No comments:
Post a Comment