Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu muendelezo na msimamo wa mradi wa Airtel
FURSA msimu wa 2 katika ofisi za Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam ili
kuendelea kuwezesha vijana wengi nchini.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Airtel FURSA kutumia Simu kuwafikia vijana nchi nzima
AWAMU ya pili ya mpango wa Airtel FURSA imezidi kujimarisha nchini
baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kujipanga kutoa mafunzo ya
ujasiriamali na kutumia mtandao wa Airtel kuwafikia vijana nchi nzima kwa njia
ya simu.
Akizungumza jijini hapa mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa
mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano, alisema mafunzo yajayo ya semina
zinazoendelea kwa vijana wajasiriamali yatafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam,
Dodoma na Lindi.
“Pia wakati wowote kuanzia sasa Airtel FURSA tutaweka wazi mfumo
wa mafunzo kwa njia mpya ya kiubunifu zaidi kwa njia ya simu za mkononi
ili kuwafikia vijana wengi zaidi wanaokabiliwa na changamoto za ajira,” alisema
Bi, Singano.
Alisema walengwa wa mpango huo ni vijana wenye kati ya umri wa
miaka 18 na 24 na kwamba tangu mradi huo uanze mwaka jana na kudumu kwa miezi
sita, takribani vijana 2,500 nchini wamekwishafaidika na sasa wanamiliki
biashara na miradi mbalimbali.
Mkurugenzi huyo wa Airte Bi, Beatrice Singano aliwaomba
wadau na serikali kujitokeza na kushirikiana na Airtel kuwawezesha vijana ili
nao waweze kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka.
“Katika msimu huu wa pili wa Airtel FURSA, tutawafikia vijana
wengi zaidi na kuwapa mafunzo na semina, ushawishi na kuwainua kwa misaada ya
vitendea kazi.
“Tayari tumefika na kutoa mafunzo katika mikoa ya Manyara na
Morogoro, sasa tunaingia Dodoma, kisha vijana wa Lindi na Dar es Saalam
wajiandae,” alisema.
Alisema uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa njia ya simu utawezesha
hata wale wasio na nafasi ya kuhudhuria mafunzo na semina, wataweza kufanya
hivyo popote walipo.
“Tunaamini kuwa msimu huu utakuwa na mafanikio zaidi kwani wengi
watawezeshwa kupitia programu hii,” alisema
Mpango wa Airtel FURSA ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi
nzima kwa kuwapatia vifaa, mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kwa njia
tofauti waweze kufikia malengo yao.
Pia mpango huu unawawezesha vijana kuongeza mitaji au kupanua
biashara zao za ujasiriamali kwa kuwapa msaada wenye thamani ya hadi Sh.
milioni 10 kwa kila mmoja.
Ili kijana kufaidika na msaada huo, anatakiwa kutuma maombi kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 15626 akiwa jina kamili, umri wake, aina ya biashara anayoifanya, mahali alipo na namba za simu, au kupitia airtelfursa@tz.airtel.com au kujaza fomukutoka kwenye tovuti www.airtel.com.
No comments:
Post a Comment