Bondia Shabani Kaoneka akipima uzito kwa ajili ya mp[ambano wake kesho
NA MWANDISHI wetu
MABONDI fransic Cheka na Geard Ajetovic wamepima uzito kwa ajili ya pambano
lao la mabara la uzito wa super middle la Shirikisho la Masumbwi ya
Kulipwa Duniani (WBF) ambapo waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye, atawaongoza Watanzania kwenye Viwanja vya Leaders
Club, Kinondoni, kushuhudia pambano la ubingwa wa Mabara wa WBF
Intercontinental kati ya Francis Cheka na Geard Ajetovic. Cheka
anamkaribisha Ajetovic, Mwingereza mwenye asili ya Serbia, katika
pambano hilo la raundi 12 uzito wa Super Middle, linalotazamwa kama
marudiano ya mtifuano baina ya wawili hao waliowahi kuchapana jijini
Manchester, Uingereza mwaka 2008. na Cheka kupoteza mpambano uho kwa
point Wawili hao wametambiana vya kutosha, kila mmoja akijinasibu kuwa
yu tayari kumuadabisha mwenzake, Cheka akienda mbali zaidi kwa kusema
hatarajii kuwaangusha Watanzania, hususani anapopigana katika ardhi ya
nyumbani. Pambano hilo limeratibiwa na Kampuni za Advance Security kwa
kushirikiana na Hall of Fame Boxing and Promotions zote za Dar es
Salaam, ambalo litatanguliwa na mapambano mengine manne, ikiwamo
burudani ya muziki kutoka kwa Bendi ya Twanga Pepeta. Akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa upimaji uzito, Mkurugenzi wa Advance
Security, Juma Ndambile, alisema maandalizi yote ya pambano hilo
yamekamilika na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kumsapoti
Cheka. Ndambile, alisema viingilio vimegawanyika makundi mawili, ambako
kiingilio cha juu kitakuwa ni Sh. 50,000 kwa Jukwaa la VIP, wakati cha
chini ni Sh. 15,000 kwa viti vya kawaida. Aliyataja mapambano ya
utangulizi kuwa kati ya Mohammed Matumla dhidi ya Mustapha Dotto (uzito
wa Light raundi nane), Mohammed Bakari na Cosmas Cheka (Feather raundi
nane) na lile la Lulu Kayage dhidi ya Mwanne Haji (Fly Raundi sita)a
ajili ya
mpambano wake
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo
vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia
watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na
kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
|
No comments:
Post a Comment