Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 12, 2016

SUPER D ATOA SADAKA WA NIABA YA BONDIA OMARI KIMWERI WA AUSTRALIA


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Deer Park, Victoria, Australia  mtoto Mohamed Mussa wa Madrasatul _Noor Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33  Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS



  Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akitoa sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Australia kwa mtoto Kauthar Seif wa Madrasatul Nool Hudaa iliyopo mtaa wa mafia Dar es Salaam Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akigawa sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Australia  kwa watoto wa
Madrasatul _Noor Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33  Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA  mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia  
amewakumbuka ndugu zake kwa kutoa sadaka kwa watoto wa Madrasatul _Noor-Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33
akizungumza baada ya kutoa msaada uho kwa niaba ya Kimweri Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mfano uhu ni wakuigwa kwa mabondia mbalimbali 
kukumbuka kutoa sadaka japo kidogo kwa kipato wanachokipata kupitia mchezo wa masumbwi   
aliongeza kwa kusema kuna mabondia wengi nchini wanapata pesa nyingi kupitia mchezo wa ngumi lakini awawakumbuki watu wenye mahitaji mbalimbali
 Kimweri anatalajia kucheza mpambano wake mwingine  feb 26 akizipiga na  Michael Camellion kutoka Philippines mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title  utakaopigwa katika ukumbi wa


The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
 
Kimweri mpaka sasa amepanda uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
 
bondia huyo mtanzania anaefanya shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo uho 
 
atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA 
 
kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana 
 
na akishinda mchezo uho itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii ya feb 26
 
Kimweri alitoa shukrani za kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila 'Super D' 
 
Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga 
 
ambao amekuwa chachu katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake ndipo kilipozikiwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...