BONDIA CHIEDZA HOMAKOMA 'NIKITA' MALAWI LULU KAYAGE TANZANIA |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Lulu Kayage yupo katika mazoezi
mazito na makali kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake wa kimataifa
na Chiedza Homakoma 'Nikita' Malawi mpambano utakaofanyika mei 14 katika
uwanja wa ndani wa Taifa
akizungumza wakati wa mazoezi yake
anayofanya kinondoni msisiri amesema anajiandaa vizuri tu kwa ajili ya
kumkabili mmalawi huyo atakaepigana nae
aliongeza kwa kusema unajuarekodi yangu imearibika kidogo kwa kuwa nilipigwa kwa point mpambano wangu wa mwisho
hivyo sasa nimejipanga vizuri
kuakikisha nafanya vema katika mpambano uho wa kimataifa nawa aidi
mashabiki wagu kuwa siku hiyo nitakuwa radhi nifie uringoni ili ushindi
ubaki Tanzania na siwezi kupigwa hapa nchini na nikatia aibu Taifa langu
siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi nchini
ambapobondia Thomas Mashali atakumbana na Sajjad Mehrab kutoka 'Irani' ubingwa wa Dunia mkanda wa U.B.O
mapambano mengine ya kimataifa
yatawakuanisha bondia Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa
Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya na
Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya na Fransic Miyeyusho
atavaana na Frank Kiwalabye wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na
Edwrd Kakembo wa Uganda
mapambano mengini ni kati ya Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola
mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga
siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi
siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa
zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa
masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa
ngumi pamoja na kutamba shiria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa
kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo
No comments:
Post a Comment