Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki (kulia)
akizungumza na waandishi (hawapo pichani) Dar es Salaam kuhusu malipo ya
sasa ya gharama za Umeme nchini.Mwengine ni Kaimu Meneja Mawasiliano na
Uhusiano kwa Wateja,Leila Muhaji.
Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Wateja,Leila Muhaji.akiwakaribisha waandishi kwenye mkutano.
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki
(katikati) akizungumza.Wengine ni Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano
kwa Wateja,Leila Muhaji (kushoto) na Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji,Pius
Gaspar.
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki(kushoto)
akizungumza na waandishi.Mwengine ni Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji,Pius
Gaspar.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kazini.
KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA VUNJO,MREMA AKUBALI YAISHE
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE
wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia (TLP) ameshinda kesi ya kupinga matokeo
ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo
kupitia chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustine Lyatonga Mrema .
Mbatia
ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa mlalamikaji (Mrema) kuamua
kufuta shauri hilo kwa hati maalumu iliyowasilishwa katika mahakama kuu
ya Tanzania Kanda ya Moshi huku akikiri kumtambua Mbatia kama mbunge
halali wa jimbo hilo.
Mbali
na utambuzi huo Mrema pia amekanusha maelezo pamoja na ushahidi wake
aliowasilisha mahakamani hapo dhidi ya Mbatia,wananchi wa jimbo la Vunjo
pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini ambazo zilitajwa
mahakamani hapo wakati wa ushahidi wake.
Ukiwasilisha
hoja mahakamani hapo mbele ya Jaji wa mahakama kuu Lugano Mwandambo ,
upande wa mlalamikaji ukiongozwa na wakili January Mkobogho ulieleza
kuwa pande mbili katika shauri hilo wamefikia makubaliano nje ya
mahakama.
Wakili
Mkobogho aliiomba mahakama kuona makubaliano hayo ambayo yako katika
maandishi kama alama kwa mujibu wa makubalinao waliyoafikiana baada ya
kuingizwa na kupokelewa mahakamani hapo kama madai.
Alisema
kwa kuwa kesi hiyo ya uchaguzi ikiwa na maslahi mapana ya umma na kwa
kuwa mlalamikiwa wa pili na watatu waliunganishwa kwenye shauri hili kwa
mujibu wa sheria aliomba kila upande ubebe gharama zao.
Wakili
Mkobogho alieleza kuwa kutokana na pande zilizokuwa zinakwaruzana
wameamua kukaa na kumalizana wenyewe na kwamba haoni sababu za
mlalamikiwa wa pili na watatu kutokubeba gharama zao wenyewe.
Jopo
la mawakili sita wa upande wa utetezi ukiongozwa na wakili , Mohamed
Tibanyendera uliileza mahakama hiyo kwamba wanaungana na mtoa maombi kwa
maslahi ya umma na kwamba wanakubali kila upande kubeba gharama zake.
Wakili
mkuu wa serikali Mark Muluambo akisaidiana na wakili wa serikali
Grayson Orcado , alisema wamesikia pande zote na wameafiki kuhusiana na
uamuzi huo kutokana na kesi hiyo kuwa na maslahi kwa umma.
Alisema
upande wao hauna pingamizi na maamuzi hayo na kwamba wamekili kupokea
nakala na wataisoma na kuipitia vizuri, na kutokana na mlalamikiwa wa
pili na watatu walitumia gharama katika kesi hiyo waliiomba
mahakama walipwe nusu ya gharama hizo.
Baada
ya kusikiliza maelezo ya pande hizo mbili Jaji Mwandambo alieleza
kupata maelezo kuwa mlalamikaji amekiri kwamba kesi hiyo hainafaida
yeyote kwa wana Vunjo na kwamba amekubali kuwa tuhuma zake zote
alizokuwa nazo juu Mbatia na watu wote aliokuwa anawahusisha na kesi
hiyo kuwa amezitengua .
Jaji
Mwandambo alieleza kuwa mlalamikaji pamoja na yote aliyoyasema pia
amekiri kuwa mbunge wa sasa wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia alichaguliwa
kwa kura halali na alipata kura nyingi dhidi yake.
Nje
ya mahakama Wakili Tibanyendera alisema haikuwa kazi rahisi kufikia
maridhiano haya na kwamba ushawishi mkubwa umefanyika baada ya Wakili
anyemtetea Mrema kumueleza ukweli mwenendo wa shauri hilo.
“Tumefanya
kazi ya kuwashawishi wateja wetu ,Mrema amekiri katika maandishi
yaliyosajiliwa leo mahakamani baada ya kuona kwamba kesi hii haina faida
kwa wana vunjo,amekiri na kutengua tuhuma zake zote alizotoa dhidi ya
Mbatia,wafuasi wake na taasisi nyingine.”alisema Tibanyendera.
“Hoja
kubwa ilikuwa ni kupinga matokeo ya Ubunge,Mrema kwa maandishi amekiri
kwamba Mbatia alichaguliwa kihalali na akapata kura nyingi kihalali,hayo
yamo katika amri wa mahakama,”alisema Tibanyendera.
Akizungumza
mara baada ya kufikiwa kwa uamuzi huo Mbunge wa jimbo la Vunjo,James
Mbatia alisema Chama chake kina aamini katika itikadi za utu na kwamba
amemsamehe na hata dai gharama za kesi hiyo.
“Tungeweza
kumdai Mrema gharama kubwa,tangu kuletwa kwa kesi hiyo mahakamani,mimi
sitamdai Mrema hata senti moja,nimemsamehe Mrema kwa sababu ni mpiga
kura wa jimbo la Vunjo,nisingependa kuona anadidimia zaidi lazima ni
mlee vizuri mzee wngu Mrema,”alisema Mbatia.
“Gharama
za mawakili talipia asilimia 50 za mawakili wa upande wetu,Mrema
amekubali kulipa sehemu ndogo ya malipo ya mawakili wetu, tungeendelea
tungeweza kuuza hata nyumba zake, sasa atalipa Milioni 40 na tayari kwa
hatua ya kwanza mawakili watapewa Mil 15 ambazo tayari ziko
mahakamani,mwezi ujao atalipa Mil 15 na kabla ya mwezzi wa sita atalipa
Mil 10 “aliongeza Mbatia.
Mbatia
aliyekuwa amengozana na mawakili wake pamoja na baadhi ya wafuasi wa
chama cha NCCR-Mageuzi alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa
jimbo la Vunjo waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo .
“Niwashukuru
wananchi wa jimbo la Vunjo kwa ushirikiano na muda mwingi uliopotea
kwa ajili ya kufuatilia kesi hii ,yapo mengi ambayo tulitakiwa kuanza
kuyafanya lakini muda mwingi tulitumia katika kushughulikia shauri hili
“alisema Mbatia.
Upande
wa utetezi katika shauri hilo ulikuwa ukiongozwa na Mawakili Mohamed
Tibanyendra, Faith Sadala ,Youngsevior Msuya na Mike Kavala huku
Mawakili wa serikali wakiwa ni Mark Mluambo Helen Mwajage na Lilian
Machange.
Katika
uchaguzi huo Mbatia alitangazwa mshindi kwa kupata kura 60,187 huku
Mrema akiambulia kura 6,416, na mgombea wa CCM, Innocent Shirima, kura
16,097.
BOSS WA RT AULA KIMATAIFA
Rais
wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) Lord Sebastian Coe (kushoto)
akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony
Mtaka.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKISHO la
mchezo wa Riadha Duniani (IAAF) limemteua Rais wa Shirikisho la Riadha nchini
(RT) Anthony Mtaka kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda kundi la ushauri wa
mikakati ya mawasiliano la shirikisho hilo.
Rais wa IAAAF ,Lord
Sebastian Coe alitangaza uteuzi huo hivi karibuni ambapo wajumbe wengine ni Abrahamson
Alan wa Marekani, Rodan Joe Junior ,Sierra Calixto
,,Karamarinov Dobromir kutoka Bulgaria na Rochdi Souad wa Ufaransa.
Akizungumza kuhusu
uteuzi huo Mtaka ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu alisema amepokea uteuzi
huo kwa furaha kutokana na kuwa ni nafasi ya juu katika sekta maarufu ya michezo katika
ngazi ya kimataifa.
“Nimefurahishwa na
uteuzi huu hasa ukizingatia nimeteuliwa nikiwa rais wa shirikisho la riadha mwenye
umri mdogo kuliko wote kwa sasa takuwa na fursa ya kujifunza mambo mengi
mazuri.”alisema Mtaka.
Alisema uteuzi huo
ni faida kubwa kwa maendeleo ya michezo katika taifa letu, hasa kipindi hiki
ambapo serikali ya awamu ya tano inapoandaa mkakati wa kuiweka sekta ya michezo
kuwa sehemu kubwa ya ajira.
Mtaka alisema Tanzania
itapata nafasi pana zaidi ya kuwakilishwa katika mikutano mikubwa ya mchezo wa
riadha duniani (Decision Making) eneo ambalo linatoa fursa kubwa kwa maandalizi
ya mashindano makubwa yajayo baada ya mashindano ya Olyimpiki yatakayofanyika
katika jiji la Rio de Jeneiro mwaka huu.
“Taifa litarajie
uwakilishi wenye tija, sababu mimi nimeteuliwa kati ya wajumbe nane ambao kila mmoja wao anawakilisha eneo kubwa,
hivyo kama nimepewa dhamana ya kuiwakilisha bara zima la Africa, kwa vyovyote
nitaweka maslahi ya nchi yangu mbele bila kuathiri utendaji wa jukumu
nililopewa.”alisema Mtaka.
“ Uteuzi wangu ni
sifa kwa taifa zima, sifa ambayo itafufua mtazamo mwema ulioonyeshwa na
wanariadha wakongwe walioiletea taifa sifa kama Filbert Bayi, Suleiman Nyambui,
Gidamis Shahanga, Juma Ikangaa bila kumsahau Mzee John Stephen Akhwari
aliyeshiriki Mexico City Games 1968.”aliongeza Mtaka.
Aidha Mtaka
alisema uteuzi huo umeongeza hamasa ya kuwekeza maradufu katika kambi ya timu
ya taifa ya riadha iliyopo katika hosteli ya Chuo cha misitu cha FITI kilichopo
West Kilimanjaro wilayani Siha na Arusha.
FAHAMU MAMBO TISA KUHUSU UKATILI KWA WATOTO
|
Kutoka
kushoto ni Emmanuel Buttorn, Rose Minja (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Watoto) na Christopher Mushi wote kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo
hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni
ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka
redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. . |
Mratibu wa kipindi cha Walinde watoto Neema Kimaro na Kimela Billa mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto wakizungumza na waandishi wa habari.katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. |
Tabu Salum kutoka redio ya Sauti ya Quran akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. |
Waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto wakijadiliana mara baada ya mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. |
Mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu Ukatili kwa watoto
Tatizo
la Ukatili dhidi ya watoto, linaongezeka siku hadi siku, na kuleta
athari mbalimbali za kimwili, kiakili, (kisaikologia) na kiafya kwa
watoto. Watoto wanaumizwa, kubakwa, kunajisiwa, kutelekezwa,
kusafirishwa kibiashara na kufanyishwa kazi za hatari zinazoathiri afya
zao. Matendo haya ya kikatili hayakubaliki kabisa.
Yafuatayo ni mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu ukatili kwa watoto:
1. Aina za ukatili
Ukatili dhidi ya watoto upo wa aina nyingi. Ukatili wa Kijinsia, ni
vitendo au maneno yanayoweza kusababisha madhara kwa mtu au kundi la
watu kutokana na maumbile yao. (Mf: kuguswa bila ridhaa, jaribio la
kubaka/kubaka, kulazimisha kufanya ngono n.k). Ukatili wa Kimwili ni kama kupigwa, kusukumwa, au kutishiwa kuuwawa kwa silaha. (Mf: kuonyeshwa kwamba hutakiwi, vipigo vya mara kwa mara) na Ukatili wa Kiakili/Kisaikolojia, kutelekezwa, kubaguliwa, kutishwa. (Mf: kuitwa majina mabaya, kunyimwa huduma za msingi, kufanyishwa kazi ngumu n.k)
2. Wahusika wa Ukatili dhidi ya watoto
Utafiti
wa Ukatili dhidi ya Watoto Tanzania ulifanyika mwaka 2009 na uliongozwa
na Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta mbalimbali za Serikali, Asasi za
Kiraia na Wadau wa Maendeleo. Katika utafiti huo ilionekana kuwa
ndugu wa karibu kama mjomba, baba, walezi na walimu ndio wanaosababisha
ukatili dhidi ya watoto. Kwa kuona hivyo, Serikali kwa kushirikiana na
wadau wengine wakaona umuhimu wa kuanzisha mpango wa kuelimisha jamii
kuzuia ukatili dhidi ya watoto.
3. Nini kifanyike kupunguza ukatili kwa watoto
Wananchi
wote kwa ujumla wana jukumu la kuhakikisha kwamba wanawalinda watoto.
Wazazi / walezi wanapaswa kujua watoto wao walipo na wanachokifanya kila
wakati na kuhakikisha usalama wa mahali watoto wanapopenda kutembea
mara kwa mara. Watoto wapewe moyo kuripoti vitendo mbalimbali vya
ukatili.
4. Umuhimu wa kituo cha huduma ya simu kwa mtoto - namba 116
Kituo
cha huduma ya simu kwa mtoto ni muhimu katika mifumo ya ulinzi wa mtoto
nchini. Ni sehemu pekee ambayo mtoto au Mzazi/Mlezi anaweza kupiga simu
na kutoa taarifa za ukatili kwa siri na kupata huduma ya ushauri nasaha
na rufaa kwa msaada zaidi kwa mujibu wa tatizo lolote linalohusu
ukatili dhidi ya watoto. PIGA SIMU BURE kwenda namba 116 kutoa taarifa
za ukatili dhidi ya watoto.
5. Uchumi na Familia
Familia
zikiwa na hali ngumu ya kiuchumi husababisha ugomvi kati ya wanafamilia
na hii huweza kupelekea kutelekezwa kwa watoto au kuwatenga watoto na
familia, jambo ambalo litaongeza hatari ya ukatili na unyanyasaji wa
watoto. Vilevile ugumu wa maisha ni kisababishi cha watoto wanaofanya
kazi katika umri mdogo, kuchuuza /kufanya biashara ya watoto, mimba
zisizotarajiwa na ndoa za utotoni. Hivyo basi ni muhimu wazazi/walezi
kujishughulisha na kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa wanachama wa
vikundi ili waweze kuzalisha mapato ya kusaidia mahitaji ya familia.
6. Madhara ya adhabu kwa watoto
Kuna
madhara mengi sana ambayo yanaweza kuwapata watoto kutokana na kupewa
adhabu mbalimbali. Adhabu huleta hasira na chuki ambayo haisaidii kuleta
mabadiliko ya tabia. Kadri adhabu inapokuwa kali zaidi ndivyo
inavyopelekea mtoto kuwa na matatizo ya kutojithamini, kuwa mhalifu,
kupata magonjwa ya akili na kuwa na tabia ya ukatili. Adhabu mara nyingi
haitoi mchango chanya kwa maendeleo ya mtoto
7. Ishara ambazo huonyeshwa na watoto waliofanyiwa ukatili
Ni
muhimu kwa wazazi/ walezi kutambua ishara mbalimbali zinazoonyeshwa na
mtoto aliyefanyiwa ukatili. Ishara hizo ni kama vile mtoto kutojiamini
hata kama anafanya kitu sahihi anakua na hofu kwa sababu tu anahisi
anaweza kupigwa. Mtoto kukataa kwenda sehemu ambazo amezoea mf. shule,
ukifuatilia kwa ukaribu utakuta kuna mtu anamfanyia ukatili huko au
njiani.
8. Wasikilize kwa makini
Ni
muhimu kujijengea mazingira ya kumsikiliza mtoto kwa makini. Unapofanya
hivyo ni muhimu ajue kuwa unamsikiliza, aidha kwa kutumia ishara bila
maneno; kama vile kuashiria kwa kichwa. Mtazame mara kwa mara kwa
mtazamo wa kirafiki. Unaweza pia kurudia aliyokwambia kwa maneno
mengine.
9. Umuhimu wa vyombo vya habari kupambana na ukatili
Kwa mujibu wa mwongozo wa vyombo vya habari wa kuandika habari za watoto uliochapishwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT),
“Watoto wanahitaji uangalizi maalum wa kuwajali na kuwalinda. Wakati wa
kuandika habari za watoto, vyombo vya habari vinapaswa kujenga taswira
sahihi kwa watoto ili kuwaepusha katika hatari ya kuadhibiwa au
kunyanyapaliwa. Watoto ni binadamu wanaohitaji kutambuliwa, kupewa
hadhi, utu, heshima na zaidi ya yote kulindwa. Kutokana na ukweli huo,
uelewa, umakini na weledi wa uandishi wa habari zinazowahusu wao kwa
kuzingatia hali yao na mahitaji yao ni muhimu. Kimsingi vyombo vya
habari vinatakiwa kuboresha uandikaji wa habari za watoto na wakati huo
huo kulinda usalama wao kimwili na kihisia/jaziba. “
Mambo
haya yameibuka katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya
mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro.
Mafunzo
hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni
ya True Vision Production yamehudhuriwa na waandishi wa habari kutoka
redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
Redio
hizo ni pamoja na Kitulo FM, Radio Maria, Radio Faraja, Boma Hai Radio,
Uplands FM, Radio Sauti ya Quran, Kwizera FM na Country FM.
Nyingine
ni Bomba FM, Zenji FM, ZBC, Radio Huruma, Ice FM, Radio Jamii Kilosa,
TBC Taifa, Dodoma FM, Fadeco Radio, Radio Victoria na Best FM.
Waandishi
wa habari wametakiwa kushirikiana na serikali na wadau wengine
kuhakikisha kuwa haki za watoto zinatekelezwa hapa nchini.
Ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kuwa anawalinda watoto na kuwasadia kukua na kufikia ndoto zao katika jami
Monday, April 4, 2016
NAIBU WAZIRI WA AFYA MAENDELEOYA JAMII JINSIA ,WAZEE NA WATOTO DKT. NASSOR KIGWANGWALLA AZINDUA JENGO LA OFISI ZA T-MARK TANZANIA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla (katikati) akikata utepe wakati wa kuzindua jengo la
ofisi la kampuni ya T-Mark Tanzania, Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa
T-Mark Tanzania,Diana Kisaka na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Kampuni ya T Mark, Charles Singili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla (katikati) akifungua rasmi jengo la ofisi ya T- Mark
Tanzania
Mkurugenzi mtendaji wa T-Mark Tanzania,Diana Kisaka(kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo
la Ofisi pamoja ja jengo la kuhifadhia mali za kampuni ya T-Mark
Tanzania, Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T Mark, Charles
Singili(katikati)
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T Mark, Charles Singili(katikati)
akizungumza na waandishi wa habari wakatinwa hafla ya uzinduzi wa jengo
la ofisi pamoja na ghala la kuhifadhia mali za kampuni.
Meneja Mradi wa asasi ya T-Mark Tanzania, Doris Chalambo akizungumza na
waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa
majrngo ya kapuni ya T-Mark Tanzania
Kikundi cha burudani kikiendelea kutoa burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya kampuni ya T-Mark Tanzania
Mkurugenzi mtendaji wa T-Mark Tanzania, Diana Kisaka(katikati) akitoa
ufafanuzi kuhusu shughuli wanazozifanya katika kampuni ya T-Mark
Tanzania mara baada ya kuwasili kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla
(kulia) na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T Mark, Charles
Singili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa T-Mark
Tanzania alipotembelea mabanda ya kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa
majengo ya kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kumaliza kufanya uzinduzi wa majengo ya kampuni ya T-Mark Tanzania
Wafanyakazi wa Kampuni ya T-Mark Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi
Wafanyakaiz wa T-MArk Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa majengo mawili kumalizika
Geofrey Adroph
BLOGGER
P.O.BOX 24793,
Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965,
Email: pamojapure@gmail.com.
Blog: http://www.pamoja.co.tz/
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Friday, April 1, 2016
JESHI LA POLISI LAONGEZA MUDA WA KUHAKIKI SILAHA SASA NI MIEZI KITATU NCHI NZIMA
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao
Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya (kulia), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mchakato
wa kuhakiki silaha ambapo jeshi hilo limeongeza muda wa miezi mitatu
kwa nchi nzima kuanzia leo.
Msemaji wa Jeshi Nchini, Advera Bukumbi (kulia), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya kuzungumza na waandishi.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.
Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.
Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na kuzisajili na kufanya malipo katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri.
Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa
"Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi" alisema Mssanzya.
Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.
Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.
"Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa," alisema.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.
Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.
Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na kuzisajili na kufanya malipo katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri.
Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa
"Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi" alisema Mssanzya.
Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.
Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.
"Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa," alisema.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Thursday, March 31, 2016
KAMATI YA BUNGE, MALIASILI, UTALILI, ARDHI NA MAZINGIRA WAMTAKA WAZIRI LUKUVI KUFUTA HATI MILIKI YA ECO ENERGY
Wajumbe wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii wakiingia kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadani jana |
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii Atashasta Justus Nditiye akitoa maazimio ya kamati hiyo mara baada ya kuitembelea hifadhi ya Taifa ya Sadani wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo,Marry Chatanda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Injia Ramo Makani akizungumza wakati wa ziara hiyo |
Kaimu Mkurugenzi wa (TANAPA),Ibrahim Mussa akizungumza wakati za ziara ya kamati ya Bunge Maliasili,Utalii na Ardhi Mazingira ilipotembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Meja Jenerali Gaudance Milanzi akizungumza wakati za ziara ya siku moja ya Kamati ya Bunge ya Maliasili,Utalii na Ardhi |
Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Tanapa,Mtango Mtaniko akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya Bunge Maliasili,Utalii na Ardhi walipofanya ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani
Mjumbe wa Kamati ya Bunge Maliasili,Utalii,Ardhi na Mazingira,Pauline Gekule akiulizwa swali wakati ziara hiyo |
MJUMBE wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii,Shabani Shekilindi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga akiuliza swali wakati wa ziara hiyo |
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini,Marry Chatanda ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo akichangia hoja kwenye ziara hiyo |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudance Milanzi kulia akiteta jambo na Meneja wa Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakati kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utalii walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani Picha kwa Hisani ya Tanga Raha Blog
No comments:
Post a Comment