Friday, May 13, 2016

NGUMI ZA KIMATAIFA KUPIGWA KESHO JUMAMOSI MEI 14 UWANJA WA NDANI WA TAIFA


Bondia Sajjabi Ben wa Uganda akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kimataifa utakaofanyika siku ya jumamosi ya mei 14 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Chiedza Homakoma 'Nikita' wa Malawi akitunishiana misuli na Lulu Kayage baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumamosi ya mei 14 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Alan Kamote kutoka Tanga Tanzania akitunishiana misuli na Salim Chazama wa Malawi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi utakaofanyika jumamosi mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
NASSIBU RAMADHANI
RAMADHANI SHAULI





LULU KAYAGE KATIKATI AKIWA NA TEAM YAKE

LULU KAYAGE KUSHOTO NA Chiedza Homakoma 'Nikita' wa Malawi
FRANSIC MIYEYUSHO
Bondia Sajjabi Ben wa Uganda akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kimataifa utakaofanyika siku ya jumamosi ya mei 14 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

 Na Mwandishi Wetu
HOMA ya mpambano wa kimataifa umezidi kupamba moto baada ya leo kukutanishwa mabondia wote  wa Tanzania pamoja na mataifa mengine watakaocheza 
 
akiongea na wahandishi wa habari
wakati wa upimaji uzito kwa mabondia Mratibu wa mpambano uho Anton Rutta amesema kuwa mabondia wote wamepima uzito na ngumi zitapigwa kesho 'Leo' kuanzia saa kumi na nusu jioni ambapo bondia
Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' atakuwa anagombea ubingwa wa dunia kg 76 mkanda wa U.B.O na Sajjad Mehrab kutoka 'Irani'


 
Wakati mapambano mengine ya kimataifa yatawakutanisha mabondia 
 
 Mwanadada Lulu Kayage atakaezichapa na Chiedza Homakoma 'Nikita' wa Malawi na Allen Kamote atapambana na Salim Chazama wa Malawi  wengine ni Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya na Fransic Miyeyusho atavaana na Sajjabi Ben wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na Edwrd Kakembo wa Uganda
mapambano mengini ya kitaifa yatawakutanisha  Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola pambano ambalo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' atatowa zawani ya vifaa vya mchezo wa ngumi kwa mshindi kati ya Nampepeche na Mazola


mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga

siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi pia ngumi zitaanza mapema kuepusha usumbufu unaojitokezaga kwa wapenzi kuchelewa majumbani mwao kwa ajili ya mchezo wa masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba shiria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo

No comments:

Post a Comment