Mkurugenzi
mawasiliano na Masoko wa kampuni ya saruji la Lafarge Tanzania Allan
Chonjo akiwaeleza wananchi wa kijiji cha Mpuguso kata ya Mpuguso
wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwamba kampuni hiyo imetoa mifuko 150 ya
saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Cha Afya cha kata hiyo, kushoto ni
mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
Wakazi
wa kijiji cha Mpuguso wilayani Rungwe mkoani Mbeya wakishangilia
baada ya kupata taarifa za msaada wa saruji kutoka kampuni ya Lafarge
Tanzania.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipokea mifuko ya saruji kutoka kwa
Maofisa wa kampuni ya Lafarge Tanzania kwa ajili wa ujenzi wa Kituo
cha Afya cha kata ya Mpuguso kilichopo wilayani Rungwe mkoa wa
Mbeya,(kushoto ni Fundi Mshauri wa ujenzi wa gharama nafuu wa Lafarge
Evarist Mnyema,Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Allan Chonjo na
Meneja wa Habari na Mahusiano Straton Bahati.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akishirikiana na viongozi wa Kijiji cha
Mpuguso kubeba mfuko wa saruji kati ya mifuko 150 iliyotolewa na
kampuni ya Lafarge Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha
Kata hiyo.
No comments:
Post a Comment