Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari
Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa
ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko
hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume
cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura
ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
---
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA.
Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa
Harambee unaowapatia elimu watoto wao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi
kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao
walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni
mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji
kijijini hapo.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman
alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada
na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia
mradi huo.
Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao
300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole
(kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki
aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa
kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi,
Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza
kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni
mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi.
Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.
Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi
waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma
masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
Mkazi wa kwanza wa kijiji cha Chole
wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu,
Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence
Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya
Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za
kupata elimu ya juu.
---
Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa
elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli
mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma
mwamko wa elimu.
"Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni ya Chole Conservation &
Development inayosimamia na kutunza magofu ya Kijerumani, ametusaidia
sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko mkubwa wa elimu," alisema
Kingi.
Alisema kuwa mwekezaji huyo aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo
ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka
2007 na umekuwa ukizidi kupanda kadri miaka inavyokwenda.
Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari
wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja na
mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi.
Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis
Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika upande wa
elimu akiwa na katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).
No comments:
Post a Comment