Monday, August 29, 2016

MABONDIA NASIBU RAMADHANII NA IDDI ATHUMANI WASAINI KUZIPIGA NOVEMBA 9 MABIBO


Bondia Nassibu Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na Iddi Athumani 'Mchina' baada ya kutiliana saini ya kupambana novemba 9 Mabibo Dar es salaam katikati ni Promota wa mpambano uho Abdallah Kamanyani Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Nassibu Ramadhani wa pili kushoto na Iddi Athumani kulia wakiwa na promota wao Abdallah Kamanyani katikati kushoto ni kocha wa Nassibu Cristopher Mzazi na wa pili kulia ni kocha wa Athumani Yusuph Komba Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Nassibu Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na Iddi Athumani baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga novemba 9 mabibo Picha na SUPER D BOXING NEWS
IDDI ATHUMANI 'MCHINA'
NASSIBU RAMADHANI
Bondia Iddi Athumani 'Mchina' kushoto akitia saini ya kuzipiga na Nassibu Ramadhani Novemba 9 mabibo Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Nassibu Ramadhani akisaini Mkataba wa kuzipiga na Iddi Athumani 'Mchina' novemba 9 mabibo

MSONDO NGOMA WALIVYO TUMBUIZA DDC KARIAKOO MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA

 Wasanii wa bend ya msondo ngoma wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika Kariakoo mwishoni mwa wiki iliyopita kutoka kushoto ni Abdul Ridhiwani na Romani Mn'gande Picha na BURUDAN BLOG
 Waimbaji wa Msondo ngoma Music Band wakiwajibika wakati wa onesho lao la mwishoni mwa wiki iliyopita lililofanyika Kariakoo kutoka kushoto na Hassan Moshi Hamisi Kambi na Juma Katundu Picha na BURUDAN BLOG
 Wasanii wa bendi ya Msondo ngoma music Bandi wakitumbuiza kushoto ni mpiga tumba Amri Said na Ibrahimu Kandaya onesho lililofanyika DDC Kariakoo Dar es salaam mwishoni mwa wiki Picha na BURUDAN BLOG
 Waimbaji wa bend ya Msondo Music wakitumbuiza wakati wa onesho ao lililofanyika mwishoni mwa wiki kutoka kushoto ni Athumani Kambi Shabani Dede na Hassani Moshi Picha na BURUDAN BLOG
 WADAU WA MSONDO NGOMA WAKIWA KATIKA ONESHO HILO
WATANGAZAJI WA RADIO WAKIWA KATIKA TAMASHA HILI LA BENDI YA MSONDO NGOMA KUSHOTO NI MTANGAZAJI WA RADIO ONE NA KULIA NI MTANGAZAJI WA RADIO UHURU

Friday, August 26, 2016

MABONDIA IDDI MKWELA NA HASHIMU CHISORA KUGOMBANIA UBINGWA WA TAIFA WA TPBC



Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Iddi Mkwela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubngwa wa raundi kumi  KG 61 utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa agost 27 jumamosi Katikati ni kiongozi Ally Bakari 'Champion' Picha na SUPER D BOXING NEWS



Mabondia Abdallah Zamba kushoto akitunishiana misuli na Twalibu Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Iddi Mkwela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubngwa wa raundi kumi  KG 61 utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa agost 27 jumamosi  Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Mabondia wa kike Halima Bandola kushoto na Ester Kazabe wakitunishiana misuli kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa katikati ni Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa
Bondia Iddi Mkwela ajiojiwa na mtangazaji wa ITV Jimmy Tala baada ya kupima Uzito
IDDI MKWELA
Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa kushoto akizungumza na mabondia pamoja na makocha wao kufata talatibu za kumwandaa bondia pamoja na sheria zake wa pili kushoto ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Mabondia Hashimu Chisora na Iddi Mkwela wakitunishiana mishuli

PSPF YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA JESHI LA MAGEREZA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM


Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi seemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete.

 Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo.

Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini.

“Nyinyi mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,

 “Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo.

Baada ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo ya mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo.

Tuesday, August 23, 2016

BONDIA IDDI MKWELA ALIVYO MSAMBALATISHA MWINYI MZANGELA TAIFA


Mabondia Mwinyi Mzengela kushoto na Iddi Mkwela wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mkwela alishinda kwa point katika mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Iddi Mkwela kulia akipiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Upcut' uku akirudi nyuma wakati mpinzani wake akiwa kamkumbatia Mkwela alishinda kwa pointi mpambano uho wa raundi sita uliofanyika mwishoni mwa wki iliyopita katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia mahelekezo bondia Iddi Mkwela wakati wa mpambano wake na Mwinyi Mzengela Mkwela alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Refarii wa mpambano wa masumbwi nchini Pembe Ndava katikati akimnyoosha mkono juu bondia Iddi Mkwela baada ya kumshinda Mwinyi Mzengela kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
MABONDIA MWINYI MZENGELA NA IDDI MKWELA WAKIPONGEZANA BAADA YA KUMALIZIKA MPAMBANO WAO MKWELA ALISHINDA KWA POINTWA PILI KULIA NI KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' Picha na SUPER D BOXING NEWS

BONDIA IDDI MKWELA AKIWA NA MASHABIKI WAKE AKISINDIKIZWA KWA AJILI YA KUENDA KUPAMBANA NA MWINYI MZENGELA
KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' MBELE KULIA AKIMSINDIKIZA BONDIA IDDI MKWELA ALIEBEBWA JUU JUU

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA WILAYANI MLELE


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda wakati Waziri Mkuu, alipohutubia mkutano wa hadara kwenye kijiji cha Majimoto wialayani MleleAgosti 23, 2016. Wapili kulia ni Mbunge wa Kavuu, Dkt.Pundeciana Kwembe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati walipokutana katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu,   kwenye kijiji cha Majimoto wilayani Mlele Agosti 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JANET MBENE AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI SEKONDARI YA ILEJE


 Mbunge wa Ileje , Mh Janet Mbene,akiakabidhi mifuko 50 ya Saruji kwa Mkuu wa shule ya Sekondari ya Ileje Agrey Mwahihojo kwa ajaili ya ukarabati wa madarasa

 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akikagua Mabweni ya Wasichana  ya shule ya Sekondari ya Ileje
 Mbunge wa Ileje ,Janet Mbene akisalimiana na Makamu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ileje , Hamidu Mwabulanga

Saturday, August 20, 2016

MABONDIA IDDI MKWELA NA MWINYI MZENGELA WAPIMA UZITO KUWA SINDIKIZA SEGU NA MFAUME TAIFA


Mabondia Iddi MKwela kushoto na Mwinyi mzengela wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito na afya kwa ajili ya mpambano wao wa Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Iddi MKwela kushoto na Mwinyi mzengela wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito na afya kwa ajili ya mpambano wao wa Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Iddi MKwela kushoto na Mwinyi mzengela wakitamba mbele ya kamera  baada ya kupima uzito na afya kwa ajili ya mpambano wao wa Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na Mabondia Iddi Mkwela kushoto na Mwinyi Mzengela baada ya kupima uzoto kwa mabondia hawo kwa ajili ya mpambano wao wa Agost 21 uwanja wa ndani wa Taifa kusindikiza mpambano wa Mfaume Mfaume na Yonas Segu Picha na SUPER D BOXING NEWS







Bondia Mwinyi Mzengela Akipima uzito kulia ni mpinzani wake Iddi Mkwela na kushoto ni msimamizi Ibrahimu Kamwe Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Iddi Mkwela akipima uzito

daktari wa mchezo wa masumbwi, Donald Madono kulia akimpima bondia Iddi Mkwela Afya yake kabla ya mpambano wake na mwinyi Mzengela Kesho
Picha na SUPER D BOXING NEWS
daktari wa mchezo wa masumbwi, Donald Madono kulia akimpima bondia Mwinyi Mzengela  Afya yake kabla ya mpambano wake na  Iddi Mkwela Kesho
Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Iddi Mkwela na Mwinyi Mzengela wamepima uzito na afya leo kwa ajili ya mpambano wao wa raundi sita mpambano utakao fanyika jumapili ya Agost 21  katika uwanja wa ndani wa taifa mpamba ambao ni wa kuwasindikiza
 Mabondia Jonas Segu na Mfaume Mfaume watakaozipiga kwa raundi nane uzito wa kg 66

Msimamizi wa upimaji wa uzito alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya ngumi za kulipwa nchini Habibu Kinyogoli ambaye alisimamia zoezi ilo la upimaji uzito pamoja na Afya kwa wachezaji wote watakao cheza
Pia aliwakumbusha sheria mbalimbali wawapo ulingoni kwani mchezaji anapaswa kujua na kuzingatia kanuni na talatibu za mchezo wa masumbwi nchini
Aliongeza kwa kusema  kuwa mapambano ya jumapili yatanza mapema sana ili kuwapa nafasi mashabiki waluni makwao wakapumziki wakiwa wamepata burudani tosha ya mchezo wa ngumi bila ya bighuza ya aina yoyote ili
Pia ulizi utakuwa wa kutosha katika mpambano uhu kwani mandalizi yote yamesha kamilika tunasubili tu kesho kwa ajili ya mchezo kamili
Bondia mwingine anaekuja kwa kasi kwa sasa katika uzito wa kati Shabani Kaoneka atapambana na Kivu Abdi mpambano wa raundi sita 

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

Wednesday, August 10, 2016

BONDIA VICENT MBILINYI AJINOA KA AJILI YA MKENYA SEPTEMBA 17 NAIROBI KENYA




 Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimnowa bondia Vicent Mbilinyi kwa kumwelekeza kupiga ngumi zilizo nyooka wakati wa mazoezi ya bondiahuyo ya kujiandaa na mpambano wake wa septemba 17 kuzipiga na George Owano  wa Kenya mpambano utakaofanyika Carnivore Grounds, Nairobi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akinolewa na kucha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kujiandaa na mpambano wake wa septemba 17 kuzipiga na George Owano  wa Kenya mpambano utakaofanyika Carnivore Grounds, Nairobi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
 BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea amendelea kujinoa kwa ajili ya mpambano wake ujao dhidi ya
George Owano  wa Kenya mpambano utakaofanyika  katika ukumbi wa Carnivore Grounds, Nairobi
septemba 17
Mpambano uho wa kwanza kwa Mbilinyi utakaofanyika nje ya nchi na ni wakimataifa utakuwa wa raundi nane uzito wa kg 63.5
Bondia huyo anaenolewa na kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa yupo tayali kwa ajili ya mpambano uho kwana ana shaka kwa kuwa mbinu zote anazijua na siri ya ushindi wake itakuwa ni si vinginevyo 
ndio mana ameamua kuwa katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM kwa ajili ya kunolewa kwa mpambano uho ujao
nae kocha wa bondia huyo aliongeza kwa kusema kuwa Mbilinyi kwa saa yupo fiti kila idara kilichobakia kwa sasa ni mazoezi ya kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya kuondoa uoga wa macho wakati wa mchezo
aliongeza kwa kusema Super D kuwa Mbilinyi ni bondia wake mwingine anaekwenda  nje ya nchi wa kwanza alikuwa Ibrahimu Class 'King Class Mawe' alienda Zambia na kufanikiwa kushinda kwa kurudi na ubingwa wa WPBF Afrika mwingine Ni mwana Dada Lulu Kayake aliyenda Afrika ya kusini na kurudi na ushindi
Hivyo mabondia wangu wote wanapokwenda nje ya nchi wa mara ya kwanza wanarudi na ushindi ndivyo itakavyokuwa kwa Mbilinyi ni wakati wake sasa

SUPER D COACH NA BONDIA VICENT MBILINYI

BONDIA VICENT MBILINYI KULIA AKIWA NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI TANZANIA RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
BONDIA VICENT MBILINYI KULIA AKIWA NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI TANZANIA RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
BONDIA VICENT MBILINYI


 VICENT MBILINYI





SUPER D COACH NA VICENT MBILINYI