Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 10, 2018

VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA KWENYE KUPIMA UZITO PALE SOKO LA VETENAL LILIOPO TAZARA KUKUTANA KATIKA MASUMBWI SEPTEMBA 15 TAIFA




FRED SAYUNI
Na Mwandishi Wetu 

Haidari Mchanjo
Katika ali isiyokuwa  ya kawaida kwa mashabiki wa michezo baada ya kucheza mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama Ndondo Cup sasa timu za Goms United na Keko Furniture zinakutana katika masumbwi ambapo Goms united inawakilishwa na bondia Haidari Mchanjo na Keko Furniture anatoka Fred Sayuni 
mashabiki wa mabondia hawo wamepanga kuanza shangwe zao siku ya ijumaa wakati wa kupima uzito kwenye soko la vetenal lililopo maeneo ya Tazara Dar es Salaam kuanzia saa nne na watacheza jumamosi katika uwanja wa ndani wa Taifa 'Indoor Stadium'

Mabondia pamoja na kambi zao watapima uzito ijumaa na watacheza siku ya jumamosi

ambapo kwa sasa yameshafanyikamaandalizi ya kutosha kwa mabondia wote kilichobaki ni mpambano tu kufanyika


Akizungumzia pambano hilo mratibu wa mapambano ya ngumi Rajabu Mhamila 'Super D'  kutoka kampuni ya kizalendo  ya Super D Boxing Promotion amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi wakati Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' atazipiga na Geoger Dimoso na Vicent Mbilinyi atavaana na Saidi Mpoma 'Kidedea' wakati Mohamedi Kashinde atakumbana na Sadiki Momba na Imani Daudi ataoneshana umwamba na Paul Kamata 

Na mpambano mwingine utawakutanisha Faraji Sayuni na Issa Nampepeche Ramadhani Shauri atakumbana na Said Amani wakati Mwinyi Mzengela atakumbana na Kassimu Rajabu 'Boxer Mnyama' Saidi Zungu na Tonny Rashidi Super D aliongeza kwa kusema kuwa mapambano hayo yote yataanza kuanzia saa 12 jioni ili zimalizike kwa wakati

mapambano hayo yameandaliwa na  kampuni ya ngumi za kulipwa ya Super D Boxing Promotion inayoendelea kuinuwa vipaji vya mabondia mbalimbali nchini ili kujikuzia kipato na kujiweka nafasi nzuri kwa mabondia kucheza kila wakati

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...