Friday, October 19, 2018

ISSA NAMPEPECHE NA HASHIMU CHISOLA WAPIMA UZITO KUZIPIGA OCTOBAR 20 CCM MWIJUMA MWANANYAMALA


Na Mwandishi wetu


BONDIA Issa Nampepeche na Hashimu Chisola wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa raundi kumi utakaofanyika jumamosi ya Octobar 20 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala akizungumza wakati wa upimaji  mratibu Ibrahimu Kamwe 'BigRaght' 

amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kukata na shoka kwani wamejipanga kuinua mchezo wa masumbwi katika kitongoji cha mwananyamala na viunga vyake

mbali na pambano hili siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka kati ya Shabani Madilu atakaezipiga na Selemani Bangaiza na bondia machachari anaekuja kwa kasi ya ali ya juu Hamisi Maya atazipiga na Zumba Kukwe kutoka Kibaha Mkoa wa Pwani  mpambano mwingine utawakutanisha Mbena Rajabu atakae oneshana umwamba na Fredy Masinde na Josephe Mbowe atazikunja na Mwinyi Mzengela 


aliongeza kwa kusema BigRight Sports and Arts Promotion imejizatiti kuinua vipaji vya mabondia chipkizi na kuwaendeleza wale walio katika chati ya juu kwa kuwandalia mapambano mbalimbali yakiwemo ya ubingwa wa taifa na yale ya ubingwa wa kimataifa

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine

2 comments: