Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 18, 2018

MABONDIA WAJIANDAA KUZIPIGA DESEMBA 31 KINESI SHEKILANGO


Msimamizi wa mazoezi Abdallah Seif 'Kamanyani' kushoto akimsimamia bondia Ramadhani Shauri kupiga beg wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Azizi Uliza katika mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki Picha na Super D Boxing News'
Na Mwandishi Wetu

BONDIA Ramadhani Shauri amendelea kujifua kwa ajili ya mpambano wake wa kufunga mwaka na kufungua mwaka utakaofanyika Desemba 31 katika uwanja wa kinesi shekilango maeneo ya urafiki Dar es salaam akimkabili Azizi Uliza katika mpambano wake wa raundi kumi

akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika kambi yake iliyopo mabibo mwembeni amesema kuwa yupo fiti kwa asilimia mia hivyo sasa anasubili mpambano tu yana natamani iwe ata leo tupate kumalizana mana nitampa kipigo ambacho si chakawaida alisema Shauri

aliongeza kwa kusema mashabiki wake wajitokeze kwa wingi waje kumwangalia kwani sasa anapigana ngumi za moto hatari kwani mpinzani wake atofika raundi ya sita hivyo nawaomba mashabiki wawai kuingia uwanjani mapema kabla mpambano aujaisha


nae Promota wa mpambano uho Josepher Nyilawila kutoka kampuni ya Ijuka Sports  amesema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali 

 Hussein Itaba atazipiga na Kanda Kabongo na Tonny Rashidi atazipiga na Nassoro Madimba kutoka Bagamoyo maeneo ya Kiwangwa na Rolen Japhert atazikunja na Mohamedi Kashinde 'Simba wa Mbagala' nae Baina Mazola ataoneshana umwamba na Faraji Sayuni


siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...