Monday, March 25, 2019

BONDIA IBRAHIMU CLASS AFUDHU VIPIMO SASA RASMI KUPIGANA U.S.A MACHI 30


Bondia Mtanzania Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akifanyiwa vipimo nchini Marekani kwa ajili ya mpambano wake wa march 30 katika ukumbi wa  Fantasy Springs Casino, Iliyo nchini Marekani.

Bondia Mtanzania Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akifanyiwa vipimo nchini Marekani kwa ajili ya mpambano wake wa march 30 katika ukumbi wa  Fantasy Springs Casino, Iliyo nchini Marekani.

Bondia Mtanzania Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akifanyiwa vipimo nchini Marekani kwa ajili ya mpambano wake wa march 30 katika ukumbi wa  Fantasy Springs Casino, Iliyo nchini Marekani.

Na MWANDISHI WETU
 Bondia Mtanzania  Ibrahim Class (King Class Mawe)  ambaye yupo nchini Marekani kwa ajili ya mchezo wa masumbwi amefanyiwa vipimo kwa mara ya pili kwa ajili ya  kupanda ulingoni kuwania ubingwa wa dunia wa Baraza la Ngumi (WBC) kwa vijana 
Class atazichapa na bingwa mtetezi, Eduardo Hernandez, Machi 30 pambano la raundi 12 la uzani wa super feather litakalopigwa kwenye ukumbi wa Fantasy Springs Casino, Iliyo nchini Marekani.


Akizungumza moja kwa moja kutoka Marekani, Class alisema baada ya kuhitimisha vipimo kwa mara ya pili na kuthibitika yuko fiti anachosubiri ni siku ya mpambano uhu tu
"Nashukuru vipimo vimeenda vizuri, niko fiti, sina tatizo lolote na kinachosubiriwa ni kupanda ulingoni," alisema Class.
Alisema hana hofu na mpinzani wake ambaye hana rekodi ya kupigwa.


"Mimi ndio na kwenda kuvunja rekodi hiyo, nimemsoma mpinzani wangu kupitia video za mapambano yake ni Bondia wa kawaida sana kwangu tofauti na wanavyomzungumzia watanzania ambao awanielewi


Class kwa nchini Tanzania alikuwa akinolewa na kocha mkongwa wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' pamoja na kocha wa kimataifa wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye alikuwa anasimamia mapambano yake yote yaliyokuwa yakifanyika nchini mpaka kufikia levo ya kimataifa

Class amewahaidi watanzania kuwa wasiwe na wasiwasi nae kwani kwa sasa amepata ujuzi zaidi wa mchezo wa masumbwi baada ya kufanya mazoezi uko Marekani na makocha wa kizungu na kugundua mbinu mbali mbali watumiazo wenzetu

aliongeza kwa kusema kuwa mchezo wa ngumi kwake upo kwenye damu na yeye anakuwa mtanzania wa kwanza kucheza ndani ya U.S.A katika kipindi kirefu kilichopita

alisema mpambano uho umedhaminiwa na promota mkubwa Duniani Oscar Dela Hoya kupitia kampuni ya Golden boy Promotion hivyo sitopenda kuwangusha watanzania na kujiangusha mimi mwenyewe katika ulimwengu wa masumbwi naomba watanzania siku hiyo ikifika waniangalie kupitia luninga zao waone nini nakifanya katika Dunia hii

No comments:

Post a Comment