Na
Mwandishi Wetu
MABONDIA kutokwa kwa Super D Coach
Uhuru GYM Sunday Kiwale 'Moro Best' na Ibrahimu Makubi wapo mkoani
morogoro kwa ajili ya mpambano yanayo wakabili ambapo Sunday Kiwale
'Moro Best' atamkabili Said Chalachim kutoka Ifakara wakati Ibrahimu
Makumbi atazipiga na Charles Chilala nae kutoka Ifakara
akizungumza baada ya kupima uzito
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
amesema kuwa mabondia wake wapo vitani hivyo awatofanya ajizi wala kuwa
na msalia Mtume kwani kazi waliyotumwa na mashasbiki zao kutoka Dar es
Salaam si yakitoto na awatotaka kuwangusha kwa kuwa wao ni watu wa kazi
kazi
nae bondia kiwale anaetamba katika
uzito wake amesema kuwa mabondia wengi nchini wanamuogopa ndio mana
amekuja kucheza Mkoani ili kuendeleza kipaji chake kisije kikapotea bule
kwa sababvu ya kuogopewa na mabondia wa Dar es salaam katika uzito wake
kwani kazi yangu wanaijua na kuitambuwa niwapo ulingoni
na bondia Makubi alisema kuwa yeye ni
bondia mchanga sana katika ngumi za kulipwa ila ni motto mkali katika
masumbwi hivyo nawaomba wapenzi wa mchezo wa ngumi waje kwa wingu
kushudia kazi atakayo ifanya
Mabondia hawo wote watakuwa
wakisindikiza mpambano wa ubingwa kati ya Twaha Kiduku wa Morogoro na
Mada Maugo watakaozipiga raundi kumi kugombea ubingwa wa Taifa nchini
Promota wa mpambano uho kaike Siraju
alieleza kwa kusema kuwa ameandaa mapambano mengi sana nchini ususani
Morogoro sasa baada ya kumuibua Fransic Cheka sasa ameibuwa mabondia
wengine mbalimbali kutoka moro pamoja na vitongoji vyake hivyo kazi kwao
mashabiki kutoa sapoti
aliongeza kwa kusema mbali na
mapambano hayo kutakuwa na mitanange mingine ya kukata na shoka ambapo
bondia Epson John atazipiga na Adamu Ngange na Cosmasi Cheka
atakabiliana na Amani Bariki na kingilio katika mapambano yote hayo ni
tsh 7000 na V.I.P 15000 na nyote mnakaribishwa
No comments:
Post a Comment