Wednesday, April 24, 2019

BONDIA RAMADHANMI MBEGU HAPANIA KUMPIGA HASSANI MGAYA KWA K,O APRIL 27 CHANIKA


Na Mwandishi Wetu

BONDIA ramadhani Mbegu 'Migwede' baada ya kumsambalatisha bila huruma mpinzani wake waliyokutana nae katika mpambano wa Pasaka Bilali Rashidi kwa K.O ya raundi ya pili sasa Mbegu atakabiliana na Hassani Mgaya katika mpambano wake wa Aperl 27 utakaofanyika katika ukumbu wa Manka Pub uliopo Chanika Magenge

akizungumza kuhusu mpambano uho Promota wa mchezo wa masumbwi nchini ambapo kiataalamu ni Kocha wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa maandalizi ya mpambano huo yamekamilika na sasa wana hesabu masaa kufikia mpambano uho mabonduia hawo watakuwa wakisindikiza pambano kubwa kati ya Saidi Mbelwa na Selemani Galili 'TOLL'   aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na mundu ambapo Juma Bilo atakabiliana na Magambo Christopher na Shukuru Samata ataoneshana kazi na Juma Ramasdhani na Mbwana Chinenda atamkabili Mohamed Muhunzi wakati Ismahil Kharidi atakumbana uso kwa uso na Salehe Ubuguyu Anamu Ngange 'Mnyama' atacheza na Saadi Kuchi wakati Abdul Zugo atazipiga na Lumeme Hussein na Idd Mbaruku atazikunja na Mohamed Mshamu

Super D amesema kuwa mapambano yote haya ni kwa ajili ya mabondia kupata ushindani kila wakati na wanatakiwa wawe bize na mazoezi kwa ajili ya mechi mbali mbali zitakazo wakabili ameseka kuwa uzito watapima siku ya ijumaa katika ukumbi uho huo na watacheza siku ya jumamosi ya April 27

Mpambano huu unategemea kufanyika kabla ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo kampuni ya kuinuwa vipaji vya mchezo wa masumbwi nchini ya Super D Boxing Promotion itakuwa likizo kwa mda kwa kuandaa mapambano ya masumbwi hata hivyo Super D ametoa wito kwa mabondia kuendelea na mazoezi kwa kipindi choto cha Ramadhani kwani kuna mapambano mengi ya ngumi yatandaliwa na Kampuni yake kwa ajili ya kukuza kuendeleza na kuinua vipaji vipya vya masum,bwi nchini Super D Mbali ya kuandaa mapambano ya ngumi pia anajihusisha moja kwa moja kuuza vifaa vya mchezo huo pamoja na kutoa mafunzo ya ngumi katika GYM yake iliyopo Kariakoo Dar es salaam

2 comments: