Friday, September 27, 2019

BONDIA JUMA CHOKI SASA AWAZIA UBINGWA WA TAIFA BAADA YA KUWA KING OF THE RING


NA MWANDISHI WETU

BONDIA Juma Choki Baada ya kumgalagaza bila ya huruma Emanuel Mwakyembe na kuchukua ubingwa wa King Of The Ring 2019 katika uzito wa KG 58 amesema ato bweteka kwa kuwachua ubingwa huo 

ambapo alipewa zawadi ya pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano amesisitiza ato bweteka kwa kuwa bingwa wa mashindano hayo ata hivyo ameomba kuwa andaliwe ubingwa wa taifa ndio matarajio yake kwa sasa akichukuwa ubingwa wa taifa kisha ataenda juu kuchukuwa ubingwa wa Afrika arafu ubingwa wa Dunia

Bondia huyo mwenye ndoto ya kuwa bingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini Tanzania kwa kuchukuwa mikanda nje ya nchi na kuletea sifa Tanzania 

Akizungumza kocha wake ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa choki ni bondia mzuri na malengo yake ni kufika mbali na kweli atafika anapo pataka kwani kwenye nia pana njia

ikumbukwe kuwa mimi ndio nimewatoa mabondia mabingwa wa dunia ambao wamepita katika mikono yangu kama vile Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Idd Mkwela Vicent Mbilinyi Sunday Kiwale Ibrahimu makubi ambaye kwa sasa yupo mazoezini akijiandaa na mpambano wake na abdallah kingolwira wa morogoro pambano litakalofanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 mwenge pale jeshini

hivyo nina uwakika na mabondia wangu wote ninaowafundisha na siku zoto sinaga kazi mbovu

1 comment: