Monday, August 30, 2021

BONDIA IBRAHIMU CLASS AMTAMBIA NASSIBU RAMADHANI KUWA SEPTEMBA 24 ATAMPIGA KWA K,O

 


 

NA MWANDISHI WETU

 

BONDIA Ibrahimu Class ‘king Class Mawe’ amesema kuelekea katika mpambano wake na Nasibu Ramadhani Septemba 24 atokuwa na msalie mtume kutokana na Nasibu kuwa na maneno sana hivyo baasi anataka akate ngebe kwa kumpiga K.O mbaya sana ambayo aijawai kutokea

 

Katika maisha ya ngumi kwani ndio itakuwa mwisho wake wa kucheza mchezo wa masumbwi nchini hivyo basi naomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje kuangalia mpambano wa kihistoria nitakaopambana na nasibu mana nimepania kucheza mchezo mzuri ambao utawafurahisha na kuwaburudisha wapenzi wa mchezo wa masumbwi nchini

 

Alijimwambafai Class ata hivyo mpambano uho wa raindi kumi unaosubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa ngumi nchini umekuwa ukoingelewa kila kukicha na wapenzi mbalimbali wa mchezo huo wa masumbwi

Nae bondia Nassibu Ramadhani alijibumapigo kwa kusema kuwa kwa sasa Class atoboi kwani mpambano wa mara ya kwanza alibebwa na majaji hivyo kwa sasa nimemuandalia kipigo kitakatifu ambacho ato kisaau maishani mwake

 

Na mimi uwaga kwangu ni vitendo tu sinaga mambo mengi katika mchezo wa  ngumi mimi ndio sinaga mda wa kuongea ongea kumaliza maneno na kubwabwaja hovyo

 

Nae promota wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’ kutoka katika kampuni Tanzu ya Kizalendo ya Super D Boxing Promotion wamejipanga kuwaletea mapambano yenye tija kwa mabondia na yenye upinzani mkubwa ili wapenzi wa mchezo wa masumbwi wapate burudani

 

Aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo wameandaa mapambano saba yatakayopigwa siku hiyo uku tukiwa tumesha wasainisha mabondia Juma Choki atakaezipiga na Issa Nampepecvh mpambano wa raundi nane

 

Na tatali wamesha wasainisha mabondia vicent mbalinyi atakaezipiga na Shedrack Ignas wakati Waziri Rosta atakuwa akizipiga na Anuary Mlawa na Albano Clement atazipiga na Ramadhani Migwede na kwa upande wa kina dada bondia Agnes Kayange atazichapa na Lulu Kayage mpambano wa raundi siti na bondia Daudi Mwita atakuwa akizipiga na Saidi Ndilimo

Tuesday, August 3, 2021

MABONDIA CLASS NA NASSIBU WAPIGWA PINI NA SUPER D BOXING PROMOTION

 


 


NA MWANDISHI WETU


PROMOTA wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amewapiga pini mabondia Ibrahimu class na Nasibu Ramadhani kwa kuingia nao Mkataba wa kuzipiga Septemba 24 jijini Dar esa Salaam 


Akizungumza baada ya kuingia mkataba na mabondia hao uliotiwa saini mbele ya rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa TPBRC Agapeter Basili zilizopo keko Dar 


Super D amesema kuwa anapenda kufungua milango kwa wafadhili mbalimbali kujitokeza kudhamili mpambano uhu kwani mpambano ulikuwa unasubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kwa kuwa hii ni dabi ambayo ina kila kitu katika mchezo wa masumbwi mana mabondia wana uwelewa wa mchezo wa ngumi pamoja na kujulikana kimataifa zaidi


aliongeza kwa kusema kuwa mchezo wa masumbwi sio uhadui kwani michezo ujenga urafiki pamoja na kujenga udugu, mabondia hawa ambao wamekuwa wakifanya kazi za uchambuzi wa mchezo wa ngumi katika TV 


ata hivyo kwa sasa wanaingia katika vita ya kutafuta heshima katika mchezo wa ngumi ambao wanaupambania kila kukicha


mbali na mabondia hao mabondia wengine waliokwisha saini mkataba kupitia kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ni Issa Nampepeche ambaye atavaana na Juma Choki katika mpambano wa kugombania ubingwa wa taifa


SUPER D AWACHONGANISHA TENA IBRAHIMU CLASS NA NASIBU RAMADHANI KUZIPIGA SEPTEMBA 24

 



Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwanyoosha mikono juu mabondia Nasibu Ramadhani kushoto na Ibrahimu Class mara baada ya kusaini mkataba wa kuzichapa Septemba 24 jijini Dar esa Salaam

 Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa kuzipiga kwa mara nyingine tena kupitia kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion mpambano unaotarajia kuzipiga septembar 24 jijini Dar es salaam akizungumza mara baada ya kuwasainisha mikataba mabondia hawo promota wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' 


Amesema kuwa mpambano uho unakwenda kuweka historia mpya ya mchezo wa masumbwi nchini Tanzania kwa kuwa viwango vya mabondia hawo ni vya kimataifa hata hivyo mabondia hawo wenye wa penzi wengi wa mchezo huo kwa kuwa na vigezo vikubwa vya kujua mchezo wa ngumi

Katika mpambano wa kwanza uliopigwa miaka kadhaa iliyopita Class alibuka na ushindi wa point na Nassibu akakubali mpambano uho ameshindwa hivyo alikuwa anaomba marudiano


ahidha kampuni hiyo imeingia mkataba wa mpambano mwingine tena kati ya Issa Nampepecha na Juma choki ikiwa pia mpambano huo ni wa marudiano


hata hivyo katika mpambano wa kwanza katika chezo uho Choki alishinda kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kuibuka na ushindi mara ya Nampepeche kupigwa na kuvuja Damu nyingi sana katika mchezo huo


ambapo mpambano uhuo ulikuwas ukichezeshwa na refarii Antoni Ruta wakigombania mkanda wa ubingwa wa P.S,T mpambano uliokuwa uchezwe kwa raundi kumi