Monday, August 30, 2021

BONDIA IBRAHIMU CLASS AMTAMBIA NASSIBU RAMADHANI KUWA SEPTEMBA 24 ATAMPIGA KWA K,O

 


 

NA MWANDISHI WETU

 

BONDIA Ibrahimu Class ‘king Class Mawe’ amesema kuelekea katika mpambano wake na Nasibu Ramadhani Septemba 24 atokuwa na msalie mtume kutokana na Nasibu kuwa na maneno sana hivyo baasi anataka akate ngebe kwa kumpiga K.O mbaya sana ambayo aijawai kutokea

 

Katika maisha ya ngumi kwani ndio itakuwa mwisho wake wa kucheza mchezo wa masumbwi nchini hivyo basi naomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje kuangalia mpambano wa kihistoria nitakaopambana na nasibu mana nimepania kucheza mchezo mzuri ambao utawafurahisha na kuwaburudisha wapenzi wa mchezo wa masumbwi nchini

 

Alijimwambafai Class ata hivyo mpambano uho wa raindi kumi unaosubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa ngumi nchini umekuwa ukoingelewa kila kukicha na wapenzi mbalimbali wa mchezo huo wa masumbwi

Nae bondia Nassibu Ramadhani alijibumapigo kwa kusema kuwa kwa sasa Class atoboi kwani mpambano wa mara ya kwanza alibebwa na majaji hivyo kwa sasa nimemuandalia kipigo kitakatifu ambacho ato kisaau maishani mwake

 

Na mimi uwaga kwangu ni vitendo tu sinaga mambo mengi katika mchezo wa  ngumi mimi ndio sinaga mda wa kuongea ongea kumaliza maneno na kubwabwaja hovyo

 

Nae promota wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’ kutoka katika kampuni Tanzu ya Kizalendo ya Super D Boxing Promotion wamejipanga kuwaletea mapambano yenye tija kwa mabondia na yenye upinzani mkubwa ili wapenzi wa mchezo wa masumbwi wapate burudani

 

Aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo wameandaa mapambano saba yatakayopigwa siku hiyo uku tukiwa tumesha wasainisha mabondia Juma Choki atakaezipiga na Issa Nampepecvh mpambano wa raundi nane

 

Na tatali wamesha wasainisha mabondia vicent mbalinyi atakaezipiga na Shedrack Ignas wakati Waziri Rosta atakuwa akizipiga na Anuary Mlawa na Albano Clement atazipiga na Ramadhani Migwede na kwa upande wa kina dada bondia Agnes Kayange atazichapa na Lulu Kayage mpambano wa raundi siti na bondia Daudi Mwita atakuwa akizipiga na Saidi Ndilimo

No comments:

Post a Comment