Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 27, 2010

KUMEKUCHA CUF KIDONGO CHEKUNDU


WAFUASI WA CHAMA CHA WANANCHI CUF WAKIENDA KWENYE UFUNGUZI WA KAMPENI KIDONGO CHEKUNDU LEO

ZAIN KUPIGA SIMU SMS USIKU BURE


MkurugenziMtendaji wa Zain Tanzania Sam Elangallor akiongea wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya ofa maaluma kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani ambapo wateja wa Zain sasa watapiga simu bure baada ya dakika ya kwanza ya maongezi kuanzia saa sita usiku mpaka saa 12 asubuhi.

BONDIA FRANCIS CHEKA KUCHEZA FILAM YA MAISHA YAKE YA MCHEZO





BINGWA wa masumbwi Tanzania Francis Cheka anatalajia kuonekana duniani kote kupitia filamu maalum itakayohusu historia ya maisha yake tokea utoto mpaka mafanikio katika mchezo huo hapa nchini.

Akiongea na waandishi wa habara jijini Dar es Salaam, mtayalishaji wa filamu hiyo hapa nchini kupitia kampuni ya Real Peoples Enterprises (RPE) Amon Ntevi alisema kampuni yake ipo katika hatua ya mwisho kupiga picha maeneo mbalimbali ikiwa ni sambamba na kuingiza matukio aliyofanya ndani nje ya Tanzania kwenye masumbwi.

“Filamu hii itakua ya pekee na ya kwanza kutengenezwa kwa hapa nchini ambapo itaonyesha uhalisia wa bondia Cheka tokea alipokua kijana mdogo na maisha aliyopitia hadi mafanikio katika mchezoo wa ngumi hapa nchini’ alisema Amon.

Pia alisema kuwa watanzania na washabiki wake duniani kote watapata kumjua kwa undani kupitia filamu hiyo itakayojaa simulizi na vitendo kutoka kwa Cheka mwenyewe.

“Wengi wanamuona Cheka kama bondia lakini hawajamjua kwa undani zaidi hivyo kupitia filamu hiyo wataweza kumjua kwa undani ni pamoja na kuingiza matukio ambayo washabiki hawakuwai kuyaona.

Kampuni ya RPE, inayojishuhurisha na matangazo, uchapishaji na utengenezaji wa ‘video documentary’ mbalimbali, kwa filamu hiyo itakuwa ni ya kipekee hapa nchini na watu watafurahia.

Aidha, alisema kuwa filamu hiyo inatalajiwa kuzinduliwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro siku ya Idd Pili ambapo Cheka atakua na pambano kali dhidi ya bondia wa Uganda Sebyala Med.


KUTOKA http://othmanmichuzi.blogspot.com

WALEMAVU WAPEWA SOMO KUUSU UCHAGUZI MKUU WA 2010



Baadhi ya watu wenye ulemavu wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa elimu ya mpiga kula kwa walemavu Dar es salaam jana iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuulika na mpango wa Maendeleo UNDP kutoka kushoto ni Mwenyekiti SHIVYAWATA Bw.Samwel Onesmo Katibu Bi.Eunice Urasa na Mwenyekiti wa Kamati Taifa ya usalama barabararani kwa watu wente ulemavu Bw.Jutoram Kabatella

UTALII WAZIDI KUIMALIKA NCHINI



Msanii wa michoro Bw. Lukas Mwainyekunde kulia akiwaonesha michoro mbalimbali watalii kutoka ujerumani kushoto ni Bw.Pascal Miller na Bw. Michael Schindt. mtaa wa zanaki Dar es salaam

Thursday, August 26, 2010


MISS TANZANIA WATEMBELEA MUNDULI


Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wasichana Maasai iliyopo Monduli Mkoani Arusha wakati wa rembo hao walipotembelea shule hiyo jana wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Paulina Lowasa dada wa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowasa, akiwapa mkono wa kuwatakia heri Warembo wa Vodacom Miss Tanzania alipokutana nao Wilayani Monduli mkoni Arusha jana na kuwapa zawadi ya vikoi vya kimaasai warembo wote 30. Warembo hao wanatembelea Kanda ya Kaskazini kuangalia vivutio vya Utalii nchini.

ROCK CITY MARATHON KUFANYIKA SEPTEMBA 26


Msemaji katika mkuzano na wandishi wa habari Mawazo Waziri akifafanuwa jambo
KAMPUNI ya Capital-Plus International (CPI) imeandaa mashindano ya riadha ya kilomita 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2010’ yatakayofanyika Septemba 26 mwaka huu Jijini Mwanza.

Tunafanya mashindano haya kwa mara ya pili ambapo ya kwanza yalifanyika mwaka jana na kwamba tunatarajia mbio hizo zitaanzia uwanja wa CCM Kirumba kuelekea njia tofauti za Jiji la Mwanza na kumalizia katika uwanja huo.

Kama ilivyokuwa katika mashindano yaliyopita tunatarajia wanariadha kutoka sehemu mbalimbali mchini pamoja na nchi jirani watashiriki katika mashindano hayo ya aina yake katika ukanda huo wa Ziwa.

Mialiko kwa ajili ya ushiriki itatumwa baada ya kutoa tarifa hizi kupitia vyama vya michezo husika ambavyo ni Jamhuri ya watu wa Congo (DRC), Rwanda, Burundi, Kenya,Uganda na Zambia.

Mashindano haya pamoja na mbio hizo ndefu pia yatahusisha matukio mengine kadhaa ambayo ni mbio za kilomita 5 kwa wote , mbio za kilomita 3 kwa wazee wa kati ya umri wa miaka 55 na zaidi, mbio za kilomita 3 kwa watu wenye ulemavu na mbio za kilomita 2 kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 7 -10.

Ada za ushiriki kwa mashindano haya ni sh. 500/= kwa mbio ndefu za kilomita 21, sh.300/= mbio za kilomita 5 na 3 wakati mbio zitakazohusisha watoto ni bure.

Tumeamua kupanua wigo wa ushiriki mwaka huu kutokana na kutambua umuhimu wa michezo kwa rika mbalimnbali lakini muhimu zaidi ni mapendekezo tofauti tuliyopokea kupitia wadau mbalimbali baada ya kumalizika kwa mashindano ya mwaka jana.

Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL),Mfuko wa Pensheni wa Taifa (PPF), Hoteli ya New Africa, NSSF Clouds FM na Isamilo Lodge ya Mwanza.

Fomu kwa ajili ya kujisajili zinapatikana Isamilo Lodge Mwanza, Ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, Ofisi za Capital- Plus International Limited- DSM, Makao Makuu ya Chama cha Riadha Tanzania (RT) Dar es Salaama, Ofisi za RT Mwanza. Pia washiriki wanaweza kupata fomu hiyo katika www.capitalplus.co.tz / rockcitymarathon.com

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi kuhusiana na mashindano haya unaweza kutuandikia kupitia info@capitalplus.co.tz.
Raymond Kanyambo
+255 786 107991, 0712 340149, 0754 027892
Katibu Mkuu wa chama cha Ridhaa Tanzania, Seleiman Nyambui (kushoto)akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuusu mashindano ya Rock City Marathon yatakayofanyika sept 26 kulia ni Mkurugenzi wa masoko bodi ya utalii Tanzania. Amant Macha katikati ni Mratibu wa mashindano hayo. Ratmond Kanyambo

Wednesday, August 25, 2010

TIMU YA TAIFA YA POOL YAINGIA KAMBINI KWA UDHAMINI WA BIA YA SAFARI




MCHEZAJI WA TIMU YA tAIFA gODFREY mUHANDO AKIPIGA MPIRA WAKATI WA MAZOEZI
TIMU ya Taifa ya mchezo wa Pool imeanza kambi kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya Dunia ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Ufaransa Novemba 8 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Tanzania (TAPA), Amos Kafwinga alisema kambi hiyo itajumuisha wachezaji 8 chini ya Kocha wao Mkuu Denis Lungu kutoka Zambia.

Kafwinga alisema wachezaji hao watakuwa wanafanya mazoezi mara mbili kwa wiki katika baa ya Blackpoint iliyopo Makumbusho, Dar es Salaam.

“Maandalizi yanayofanywa yataisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano hayo ya kuitangaza nchi kupitia mchezo huo unaodhaminiwa na bia ya Safari Lager,” alisema Kafwinga.

Wachezaji wanaounda timu hiyo ni Felix Athanas, Abuu Shabani, Godfrey SWai, Mohamed Idd, Omary Akida, Godfrey Mhando, Aliakber A Akberali na Arjuan Lavinja.

Nae kocha wa mchezo Lungu alipo ulizwa kuusu maendeleo ya kambi hiyo alisema wachezaji wote wapo katika hili nzuri ya mchezo na watahakikisha wanaitangaza vema bendera ya Tanzania kimataifa


Kocha wa Timu ya taifa ya mchezo wa pool. Denis Lungu (katikati) akiwapa maelezo wachezaji wa timu hiyo kwenye kitabu wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika makumbusho Dar es salaam

MISS TANZANIA WAFANYA ZIARA ZIWA MANYARA


Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watalii waliotoka Chuo Kikuu cha Calfonia Los Angels Marekani waliotembelea Hifadhi ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya warembo wanao shiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimsikiliza mmoja wa waongoza watalii (hayupo pichani) katika Hifadhi ya Ziwa Manyara alipokuwa akiwapa maelezo juu ya hifadhi hiyo.

BIA YA KILIMANJARO YAINGIA MKATABA WA MIAKA MITATU YA UDHAMINI WA BONGO STAR SEACH


Mkurugenzi wa BenchMark Production,Madame Ritha Paulsen akiongea leo katika ukumbi wa hoteli ya Paradise uliopo ndani ya jengo la Benjamin Mkapa wakati wa utambulisho wa mdhamini mkuu mpya wa Bongo Star Search ambaye ni kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chak cha Kilimanjaro premium lager.kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na kulia ni Afisa masoko na mafunzo wa TBL,Edith Bebwa.

Bongo star search ni moja ya kipindi kinacho rushwa na television hapa nchini Tanzania ambacho kime fanikiwa kwa kiwango kikubwa kabisa kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa mwaka jana kampuni ya kutengeneza bia hapa nchini TBL kwa kupitia kinywaji chake kinachojihusisha na maswala ya muziki Kilimanjaro premium lager. Ilishiriki kama mmoja wa wadhamini wa shindano hilo.

Uhusiano huu mkubwa wa kampuni hizi mbili umetokana na sababu kuu kwamba BSS inahusika kutafuta na kuinua vipaji vya wanamuziki hasa vijana wa umri wowote ambapo Kilimanjaro premium lager kufuatia kauli mbiu yake ya Kufikisha Muziki wa Tanzania Kilele cha mafanikio kwa upande mwingine ina husika na muziki wa vijana wa Kitanzania.

Kilimanjaro premium lager imekua ikunga mkono juhudi za kuendeleza Muziki hapa Tanzania kwa kiwango cha juu.. Ikiwa mdhamini mkubwa kwenye zoezi la kutoa Tunzo za Muziki Tanzania kila mwaka,Tunzo zinazojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Ndio maana Kilimanjaro premium lager imeona hakuna sababu ya wao kutoshirikiana na BSS 2010 katika kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.

Kilimanjaro premium lager imeandikisha mkataba wa kuwa mdhamini wa Bongo star search kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo ni BSS 2010, BSS 2011, BSS 2012.

Washiriki wa BSS watashirikishwa katika mambo mbali mbali yakiwemo mashindano yatakayo kua yanafanyika siku hadi siku katika jumba la BSS KILI HOUSE 2010.

BSS 2010 itakuwa ikirusha hewani kila jumapili saa tatu na robo usiku (3:15) kupitia television ya ITV ikishirikiana na Radio one na magazeti ya The Guardian ,Nipashe.
unatakia kufuatilia shindano hilo bila kukosa na pia ni muhimu kupiga kura yako ili kuweza kuwachagua watakao weza kushiriki mpaka mwisho .

shiriki nasi ili kuweza kukamilisha ndoto za wanamuziki wetu.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akitangaza udhamini miaka mitatu wa shindano la Bongo Star Search katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Paradise jijini Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni Mkurugenzi wa Benchmark Production, Ritta Paulsen.

Tuesday, August 24, 2010

MILIONI 800 ZATUMIKA KUTANGAZA UTALII LIGI YA UINGEREZA


Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Tengeneza akifafanuwa jambo kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Aloyce Nzuki
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Aloyce Nzuki akizungumza na waandishi wa habari leo kulia ni Meneja Masoko wa bodi hiyo Geofrey Meena

Bodi ya Utalii Tanzania imeendelea kutumia mbinu mbalimbali za kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi, kadiri uwezo wa kifedha unavyoruhusu.

Kwa mara nyingine tena, Bodi ya Utalii imetumia michezo kutangaza vivutio vya utalii. Tofauti na huko nyuma ambako tulikuwa na timu za mpira kutoka nje ya nchi ambazo zilicheza hapa nyumbani, kwa mara ya kwanza sasa tumetumia michezo inayoendeshwa nje ya nchi kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia baadhi ya mashirika yake (hususani TANAPA na Ngorongoro), kwa uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania, tumenunua nafasi ya kutangaza kwenye viwanja vya nyumbani vya timu sita (6) zilizopo kwenye ligi kuu ya Uingereza, iliyoanza tarehe 14 Agosti, 2010 na itakamilika tarehe 22 mei, 2011.kwa galama ya milioni 800

Tanzania inakuwa ni nchi ya kwanza Afrika kuweka matangazo yake kwenye viwanja vya mpira katika ligi hii ya Uingereza.

Viwanja ambavyo Tanzania imeweka matangazo yake ni vile viwanja vya nyumbani vya timu sita zifuatazo:-


Kama ambavyo wengine mnafahamu, zipo timu 20 zinazocheza hii ligi kuu ya Uingereza, na kwamba kila timu inacheza na nyingine, nyumbani na ugenini. Sisi tumeweka matangazo yetu kwenye viwanja hivyo sita vya nyumbani, maana yake tutakuwa na jumla ya mechi 114, tangu kuanza kwa ligi hii tarehe 14 Agosti, 2010 hadi tarehe 22 Mei, 2011.

Tarehe 14 Agosti, 2010 siku ya kwanza ya ligi, timu tatu zilicheza kwenye viwanja vya nyumbani na matangazo yetu yalionekana. Timu hizo ni Blackburn Rovers, Sunderland, na Wolves.

Matangazo haya ni ya teknolojia ya “digital video” (yaani LED Perimeter Advertising) ambayo yataonekana kwenye kuta za kuzunguka uwanja. Matangazo haya ni ya sekunde 30 kila linaporushwa, na katika mechi moja tangazo hilo litarushwa si chini ya mara sita, kwa jumla ya dakika tatu kila mechi.

Kwa sekunde hizi 30, tumeandaa matangazo mafupi, hususan kuonesha vivutio vyetu maarufu, lakini mwisho wa kila tangazo kuna tovuti iayoitwa www.visit-tanzania.go.tz

KAMPUNI YA ZAIN YAFUTULISHA WATOTO YATIMA TANGA


Zain yafuturisha yatima Tanga

Kampuni ya simu za mkononi ya Zain kupitia mradi wake wa Build Our Nation, imetoa futari katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Orphanage Trust Team cha Tanga mjini kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani.

Futari hiyo ambayo ilitolewa na Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tunu Kavishe iliambatana na misaada mingine kama vile vyandarua 90 pamoja na vyakula vikiwemo mchele, Unga, Sabuni na Mafuta ya kupikia vilivyotolewa za Zain pia.

Akiongea wakati wa hafla hiyo Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tunu Kavishe alisema kuwa Zain wameamua kutoa msaada huo kama sehemu yake ya kujali jamii kupitia mradi wake wa Build Our Nation.

“Siku ya leo, tumeamua kufuturu pamoja na watoto yatima wanaotunzwa na kituo cha watoto yatima cha Orphanage Trust Team kilichopo cha hapa Tanga, hii ni sehemu muhimu kwetu katika kusaidia Jamii na pia kama ishara ya mshikamano unaonyeshwa na Zain kwa jamii na wateja wake, haswa wakati wa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani”, alisema Tunu Kavishe, Meneja Huduma za Jamii wa Zain.

Akizungumzia msaada huo, Msimamizi wa kituo cha Orphanage Trust Team, Sheikh Hassani Waziri, alisema kuwa wamefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Zain kwa ajili ya kuwakumbuka watoto yatima katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani.

“Tunawashukuru sana Zain kwa kuwakumbuka watoto hawa yatima katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na naomba msaada huu uwe endelevu ili watoto hawa nao wapate fursa ya kufurahia maisha yao”.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini Dr. Ibrahimu Msengi ambaye aliyehudhuria hafla hiyo aliishukuru kampuni ya Zain kwa kuonyesha moyo wa kusaidia watoto yatima katika kituo hicho.

Kwa mujibu wa Kavishe, mikoa mingine ambayo kutafanyika hafla za kufuturisha kutoka zain ni Dar es Salaam, Pemba, Songea, na Mbeya, Morogoro, Tabora, Kigoma na Kagera.

Kavishe alisema kuwa zaidi ya miaka mitano, mbali na juhudi za kusaidia jamii kwa namna mbalimbali hapa nchini, hususan katika sekta ya elimu, kampuni ya simu ya Zain imejiwekea utaratibu wa kuwa inafuturisha wadau mbalimbali katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Monday, August 23, 2010

Mndorwa aibuka mshindi gofu Lugalo


Na Mwandishi wetu

Eddy Mndorwa amefanikiwa kuibuka mshindi katika mashindano ya mchezo wa gofu yaliyofanyika juzi katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kupata pointi 38.

Mndorwa aliyekuwa akichuana vikali na Simon Sayore alifanikiwa kumpiku kwa tofauti ya pointi 4 baada ya mpinzani wake kujipatia pointi 34.Ushindi huo ulimpatia Mndorwa zawadi mbalimbali kutoka Zain ikiwemo seti ya vyombo vya ndani.

Akiongea baada ya kukabidhiwa zawadi Mndorwa alisema akuamini wala akutarajia kama angekuwa mshindi kwasababu mchezo ulikuwa mgumu na kwamba alipata upinzani mkali kutoka kwa wachezaji wengine lakina hatimaye akaibuka mshindi.

“Siamini kama nimeshinda kwani mchezo kwangu ulikuwa mgumu sana na mpinzani wangu alikuwa mkali kweli lakini nimetumia vyema mashimo namba tisa na kumi ambayo yamenipa ushindi,” alisema Mndorwa

Mndorwa ambaye ni mchezaji mkongwe alisema yeye kumshinda Sayore ni furaha kubwa sana, kwakuwa alikuwa akisikia kuwa Sayore ni mchezaji mkongwe na mwenye uwezo mkubwa katika uchezaji wa mchezo wa gofu.

Mbali na Mndorwa washindi wengine ni Ally Mufuruki, Simon Sayore,Hassan Nkya na Bradray Mitchell Washindi hawa pia walijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo miavuli, vyombo vya nyumbani pamoja vyote kutoka Zain.

Michuano hiyo ambayo imekuwa ikifanyika kila mwisho wa wiki chini ya udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zain itaendelea wiki ijayo katika viwanja hivyo kwa kuwashirikisha wachezaji wa rika mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

ZANTEL YAPUNGUZA BEI VIFURUSHI VYA INTANET


Gari la Zantel la huduma kwa wateja likiwa limeegeshwa mjini tayari kuwahudumia wateja wa intaneti wa Zantel pamoja na kutoa huduma zingine kama kusajili namba za simu.
Vijana wa Zantel wakiwa kwenye pikipiki yenye kasi kuashiria jinsi intaneti ya Zantel ilivyo na kasi wakipita barabara za mji wa Dar es Salaam wakigawa vipeperushi vya vifurushi vipya intaneti.

KUMBUKUMBU YA MZEE SULEIMAN KAUBANIKA


Familia ya Halima S. Kaubanika ya Ilala Dar es salaam, wanakumbuka kifo cha baba yao Mzazi Mzee Suleiman M. Kaubanika kilichotokea
24/8/2009 Kigogo Dar es salaam. Sasa ni mwaka mmoja tangu ututoke wake zako, watoto,marafiki zako na majirani wanakukumbuka sana hasa kwa ucheshi na mawazo uliokuwa nayo Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi- Amin

Hits Tanzania kuzinduliwa Januari 2011 kutingisha mitandao mingine


mwenyekiti wa Excellentcom Tanzania Ltd, Mhe. Abdullah Mwinyi

Mwenyekiti wa Excellentcom Tanzania Ltd, Bw.Abdullah Mwinyi (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Bw. David Charles wakipongezana baada ya kuzindua nembo ya “hits” Dar es salaam jana itakayoanza kutoa huduma za mtandao wa simu mwanzoni mwa 2011
Kampuni ya ExcellentCom inayoendesha shughuli zake kama Hits Tanzania imefanya uzinduzi wa chapa na nembo yake ya “hits”
jijini Dar es Salaam jana. Hits Tanzania ni kampuni inayoendesha mtandao wa mawasiliano ya simu ambayo imepewa leseni ya kutoa huduma za Sauti, ujumbe mfupi na huduma za Mtandao (Data).

Wakati wa uzinduzi wa nembo yake, mwenyekiti wa Excellentcom Tanzania Ltd, Mhe. Abdullah Mwinyi alisema “Hits Tanzania sasa imeanza rasmi shughuli zake na iko kwenye hatua za mwisho kuwasha mitambo yake, kwa hiyo wataanza ujenzi na upanuzi wa mtandao ili kuwa na uwezo wa kutoa huduma nchi nzima mapema mwakani".

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mtendaji Mkuu wa ExcellentCom, David Charles alisema kwamba kwa mujibu wa taarifa ya TCRA (Tanzania Communications Regulatory Authority) ya Machi 2010, soko la huduma za simu za mkononi kwa sasa zinapatikana kwa kuwafikia zaidi ya asilimia 40 ya wananchi wa Tanzania. Aliongeza kwamba na kwa mujibu wa taarifa ya BMI (British Market Index) ya awamu ya pili ya mwaka 2010, matarajio ni kwamba huduma hizo zitawafikia zaidi ya asilimia 60 ya wananchi ifikapo 2012.

Bw. Charles alisema kwamba tayari kuna uwekezaji endelevu wa miundombinu kadhaa ya mawasiliano ambayo inashawishi kuwapo kwa mikakati ya ubia endelevu. “Kusema kweli, imeonekana dhahiri kwamba hakuna wakati muafaka kwa kampuni ya Hits Tanzania kusambaza mtandao wake kama sasa,” alisema.
Kampuni itaendelea na harakati za kuwekeana mikataba na wabia muhimu ambao wataiwezesha kampuni hiyo kuwapa wateja wa Hits na wateja wa wabia huduma maalum hapo ifikapo mwakani. Kwa mtazamo huo, kampeni hiyo itaitwa "a life time subscription" ambayo itatoa thamani na ubora kwa wabia wa Hits pamoja na wateja wake.

Hits Tanzania itazindua kampeni ya kutenga namba ya simu baadae mwaka huu, ambapo wateja wataweza kutengewa namba zao kupitia kianzishi namba cha Hits, ambacho ni 0741 mpaka 8.

Sunday, August 22, 2010

MASHINDANO YA WAZI YA GOFU YANAYODHAMINIWA NA BANK YA KCB KUMALIZIKA LEO





Mchezaji wa gofu,Katembo Maftah akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya wazi ya mchezo huo yaliyomalizika Dar es salaam jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya KCB Tanzania
Wafanyakazi wa KCBA Tanzania wakiwa katika viwanja wa gofu leo

Mchezaji wa gofu, Munir Ailyissa akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya wazi ya mchezo huo yaliyomalizika Dar es salaam leo. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya KCB Tanzania
Mchezaji wa gofu, Suleiman Kessy akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya wazi ya mchezo huo yaliyomalizika Dar es salaam leo. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya KCB Tanzania

KAMATI YA UTENDAJI TASWA YAKUTANA KWA MARA YA KWANZA


Wajumbe mbalimbali wa chama hicho wakiwa katika kikao kilichofanyika jana jijini Dar es salaam picha na blog ya fullshangwe

Friday, August 20, 2010

REDD'S MISS TANZANIA 2010 HUYU !!


Warembo washiriki wa Miss Tanzania 2010 wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa bia ya Redd's mara baada ya mkutano wa kumsaka balozi wa Redd's kumalizika leo katika hotel ya Gerrafe,mbezi beach.

WASANII WATAPELIWA MKURANGA


WASANII WALIOUZIWA VIWANJA MKURANGA WAMETAPELIWA

Asasi moja inayojitambulisha kuwa inashughulikia wasanii,inadaiwa kutapeliwa mashamba waliyodai kuyanunua katika kijiji cha Mwanzega,wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa ajili ya Waandishi wa habari na wasanii.

Uongozi wa Serikali ya ya wilaya ya Mkuranga,umetoa maelezo kuwa,wale wote waliouziwa mashamba hayo wametapeliwa,kwani si mamlaka za wilaya wala Halmashauri zilizohusika kwa namna yoyote ile katika mchakato huo.Mkuu wa wilaya hiyo,Henry Clemence,amesema tayari jeshi la polisi wilayani humo limeingilia kati na kuwashikilia kwa muda Mwenyekiti wa Kijiji hicho pamoja na viongozi wa asasi hiyo (jina tunalo).

Alisema kuwa hadi sasa,Mtendaji wa kijiji hicho hajulikani alipo baada ya kutoroka,kwa kujua kuwa anasakwa na vyombo vya dola.

Clemence alitoa maelezo hayo wakati akizungumza na Nipashe,baada ya watu waliochukuliwa fedha kupitia taasisi hiyo kutua wilayani humo kwa lengo la kukabidhiwa ‘MAENEO YAO’. “Wilaya ya Mkuranga haina ardhi kama hiyo,wilaya hii ipo karibu na jiji la dare s salaam..inapaswa kupangwa vizuri ili ilete manufaa kwa watu wa Mkuranga.

Kwa wanaotaka kuja huku (Mkuranga),nawashauri wafuate taratibu,wasivunje amani iliyopo…wanaotaka ardhi wapitie Halmashauri,wasipitie katika asasi wala kwa mtu yeyote kwa sababu taratibu za kumiliki aradhi hazielekezi hivyo,”alisema mkuu huyo.

nestle-tanzania-taarifa-kwa-vyombo-vya



Dar es Salaam: Mamlaka ya chakula Tanzania (TFDA) iliitarifu Nestlé kwamba Tanzania imeamua kuyazuia makopo 2261 tofauti ya maziwa ya watoto na vyakula vingine kutoka sehemu mbalimbali. Baadhi ya makopo hayo ni bidhaa ya Nestlé ambayo ni maziwa ya watoto ya NAN 2 yanayotoka nchini Afrika ya kusini. TFDA imeyatambua makopo 26 ya NAN 2 ambayo hayafai.

Tawi la Nestlé la nchini Tanzania limepatiwa taarifa hiyo na mamlaka ya chakula Tanzania (TFDA) kwamba maziwa haya ya NAN2 yanauzwa nchini Tanzania. Nestlé imeamua kulichukulia suala hili kwa umakini na wameamua kutoa ushirikiano wa hali ya juu na TFDA na mamlaka nyingine za serikali ili kutatua tatizo hili haraka iwezekanavyo

Nestlé imejidhatiti katika kutoa maziwa yenye kiwango cha hali ya juu kwa wateja wake na inapenda kuwakumbusha watumiaji wote vielelezo muhimu vya maziwa ya Nestlé yanayouzwa nchini Tanzania

.

Maziwa ya watoto ya NAN na LACTOGEN yanayoingia nchini Tanzania yanatoka ulaya.Uhalisi wa bidhaa hii umeonyeshwa kwenye kopo.

· NAN 2, LACTOGEN 1 Na LACTOGEN 2 yanatengenezwa Na Nestlé ya nchini Ufaransa

· NAN 1 inatengenezwa na Nestlé ya nchini Netherlands

Na bidhaa zote zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili na kuna nembo ya ndege weupe watatu

Nestlé inapenda kuwashauri watumiaji wa bidhaa zake na umma wa watanzania kwa ujumla kuhakikisha wananunua bidhaa zetu kufuatana na vielelezo tulivyovitaja hapo juu.
Share |

MAKAI MORINGA ENTERPRISES YAONESHA BIDHAA


Mkurugenzi Mtendaji wa MAKAI MORINGA (MLONGE) ENTERPRISES Bi. Eileen Kasubi akionesha bidhaa mbalimbali wanazouza ofisini kwake leo
DAWA YA MAKAI MORINGA (MLONGE) ENTERPRISES

FM ACADEMIA KUZINDUA ALBAM MPYA IDDI MOSI


Rais wa bendi ya FM Academia Nyoshi el Sadaat akizungumza na waandishi kuusu uzinduzi uho leo

Thursday, August 19, 2010

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI YA KUTEMBELEA MIRADIILIYOFADHILIWA NA HEIFER PROJECT INTERNATIONAL-HAPA NI UFUGAJI WA NGAMIA WA KIKUNDI CHA KAPASHE -SAME


Viongozi wa HEIFER na waandishi wa habari wakitambulishana na wanakikundi wa Kapashe wa Wilayani Same
Mchungaji wa Ngania Geofrey Shegere akiwaongoza Ngamia kwenda kuchota maji ikiwa ni moja ya kazi ambazo mnyama huyo hufanya.

PILIKAPILIKA ZA KURUDISHA FOMU MANSPAA YA KINONDONI LEO



Mgombea nafasi ya Ubunge wa jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA Bw. Jonh Mnyika akirudisha fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam kupitia Chama cha National Reconstuction Alliance Allance (NRA).kwa Msimamizi Msaidizi wa jimbo hilo Bi Sion Nnk



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe Bi.Halima Jams Mdee akirudisha fomu yake ya kugombania ubunge wa jimbo hilo kwa Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi Bw. Onesmo Kweyamba

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe Bi.Angela Kizigha akirudisha fomu kwa Msaidizi wa uchaguzi Jimbo la Kawe Bw. Onesmo Kweyamba



Mwandishi wa Habari wa gazeti la Dar Leo linalochapishwa na Kampuni ya Business Times Limited (BTL),Ni. Rachel Balama, akirudisha fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam kupitia Chama cha National Reconstuction Alliance Allance (NRA).kwa Msimamizi Msaidizi wa jimbo hilo Bi Sion Nnko

Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia chama cha Wananchi CUF Bw. Julius Miatiro akirudisha fomu kwa Msimamizi Msaidizi Bi. Sion Nnko Dar es salaam leo kwa ajili ya kugombea

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe Bw. James Mbatia akipunga mkono wafuasi wake waliokuwa wakimsindikiza kurudisha fomu Dar es salaam leo kwa ajili ya kugombea

Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia chama cha CCM, Idd Azani (kulia) akirudisha fomu kwa Msimamizi Msaidizi Bw. Burton Mahenge Dar es salaam leo kwa ajili ya kugombea
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...