Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 20, 2010

nestle-tanzania-taarifa-kwa-vyombo-vya



Dar es Salaam: Mamlaka ya chakula Tanzania (TFDA) iliitarifu Nestlé kwamba Tanzania imeamua kuyazuia makopo 2261 tofauti ya maziwa ya watoto na vyakula vingine kutoka sehemu mbalimbali. Baadhi ya makopo hayo ni bidhaa ya Nestlé ambayo ni maziwa ya watoto ya NAN 2 yanayotoka nchini Afrika ya kusini. TFDA imeyatambua makopo 26 ya NAN 2 ambayo hayafai.

Tawi la Nestlé la nchini Tanzania limepatiwa taarifa hiyo na mamlaka ya chakula Tanzania (TFDA) kwamba maziwa haya ya NAN2 yanauzwa nchini Tanzania. Nestlé imeamua kulichukulia suala hili kwa umakini na wameamua kutoa ushirikiano wa hali ya juu na TFDA na mamlaka nyingine za serikali ili kutatua tatizo hili haraka iwezekanavyo

Nestlé imejidhatiti katika kutoa maziwa yenye kiwango cha hali ya juu kwa wateja wake na inapenda kuwakumbusha watumiaji wote vielelezo muhimu vya maziwa ya Nestlé yanayouzwa nchini Tanzania

.

Maziwa ya watoto ya NAN na LACTOGEN yanayoingia nchini Tanzania yanatoka ulaya.Uhalisi wa bidhaa hii umeonyeshwa kwenye kopo.

· NAN 2, LACTOGEN 1 Na LACTOGEN 2 yanatengenezwa Na Nestlé ya nchini Ufaransa

· NAN 1 inatengenezwa na Nestlé ya nchini Netherlands

Na bidhaa zote zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili na kuna nembo ya ndege weupe watatu

Nestlé inapenda kuwashauri watumiaji wa bidhaa zake na umma wa watanzania kwa ujumla kuhakikisha wananunua bidhaa zetu kufuatana na vielelezo tulivyovitaja hapo juu.
Share |

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...