Marquee
tangazo
Tuesday, August 10, 2010
ZAIN YATANGAZA PUNGUZO KUBWA KATIKA VIWANGO VYA MALIPO YA INTERNET
Meneja Masoko wa Kampuni ya Zain Tanzania Bw. Costantine Magavilla (kulia) na Meneja Uhusiano Bw. Muganyizi Mutta wakizindua huduma ya vifurushi vyamalipo ya Intarnet vilivyopunguzwa garama, Dares salaam
KAMPUNI ya simu ya Zain imetangaza /toa punguzo la zaidi ya asilimia 10 katika viwango vya malipo ya huduma ya intaneti ili kuwanufaisha wateja wake.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Meneja Masoko Zain, Bw.Contantine Magavilla wakati akitangaza punguzo hilo kuwa, zaidi ya wateja milioni tano watatumia huduma hiyo kwa viwango nafuu.
"Tunatambua kuwa wateja wetu wanahitaji kupata huduma ya interneti popote walipo kwa haraka na nafuu, kwa viwango hivi vipya vya malipo tunawahakikishia kuwa viwango bora zaidi vitaendelea kutolewa kwa malipo ya kabla na awali," alisema Bw.Magavilla
Alisema watumiaji wa huduma hiyo watashuhudia kasi ya mawasiliano ambayo itachangia katika maendeleo mbalimbali ya kiuchumi.
Aliongeza kuwa huduma hiyo itakuwa na viwango tofauti vya malipo kutokana na hitaji la mteja ambpo kwa siku (datasiku ) itakuwa shilingi 500 na fulldata ambayo itakuwa ya mwezi mmoja italipiwa shilingi 70,000.
"Huduma hii inampa nafasi mtumiaji wa zain kutumia intaneti kupitia katika simu yake ya mkononi au kutumia modem katika kompyuta yoyote na mahalipopote nchini," alisema Bw.Magavilla
Alisema ili kutumia huduma hiyo mteja atatakiwa kutuma ujumbe kwa maandishi kwenda namba 15444 kulingana na viwango vya malipo mteja anavyohitaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment