Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, December 29, 2013

Mdau Maggid Mjengwa azindua kitabu cha Simulizi za Mzee Mandela

  

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ikolo Investment,Maggid Mjengwa akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhulia kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Kitabu cha "Simulizi za Mzee Mandela" kilichoandikwa na Maggid Mjengwa mwenyewe.hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Kwenye Uzinduzi huo,Ndugu Mobhare Matinyi akisisitiza jambo mbele ya wadau mbali mbali waliohudhulia kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Kitabu cha "Simulizi za Mzee Mandela" kilichoandikwa na Maggid Mjengwa,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wadau waliokuwepo kwenye uzinduzi huo akiuza swali.
Wadau wakinunua vitabu hivyo vya  "Simulizi za Mzee Mandela" mara baada ya uzinduzi wake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ikolo Investment,Maggid Mjengwa akisaini kwenye vitabu hivyo vilivyonunuliwa na wadau hao.

Saturday, December 28, 2013

DVD ZA NGUMI ZINAZOPENDWA NA WADAU WENGI HIZI HAPA



DVD HII YA FLOYD MAYWETHER VS ROBERT GUERRERO IKIWA NA MAPAMBANO MATATU NDANI NDIO INASHIKA CHATI KWA KUPENDWA NA WADAU WENGI
MAPAMBANO MAKALI YA NGUMI ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

DVD HII YA THIMOTHI BRADLEY VS JUAN EMANUEL MARQUEZ NI MPYA AMBAYO INATOKA WIKI END HII IMEKUWA GUMZO MIDOMONI MWA WATU BAADA YA BRADLEY KUMTWAGA MARQUEZ KWA POINT
MAPAMBANO MAKALI YA NGUMI ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
DVD HII AMBAYO INA MAPAMBANO MENGI YA WATANZANIA YAKIWEMO JAPHERT KASEBA VS MANENO OSWARD,KASEBA VS CHEKA,CHEKA VS RASHID MATUMLA, CHEKA VS HASSANI MATUMLA, JOSEPHE MARWA VS ALPHONCE MCHUMIA TUMBO NA CHEKA MPAMBANO WAKE ALIOPOTEZA UJERUMANI
MAPAMBANO MAKALI YA NGUMI ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

DVD HII INAENDEREA KUWA GUMZO KUTOKANA NA MABONDIA WALIOCHEZA KWENYE DVD HII YA MASUMBWI IKIMUHUSISHA FLOYD MAYWETHER VS MIGUEL COTTO PAMOJSA NA MAPAMBANO YA UTANGULIZI YALIOCHEZWA SIKU YA MPAMBANO
DVD HII YA FLOYD MAYWETHER VS ROBERT GUERRERO IKIWA NA MAPAMBANO MATATU NDANI NDIO INASHIKA CHATI KWA KUPENDWA NA WADAU WENGI
MAPAMBANO MAKALI YA NGUMI ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

DVD HII INAENDEREA KUWA GUMZO KUTOKANA NA MABONDIA WALIOCHEZA KWENYE DVD HII YA MASUMBWI IKIMUHUSISHA FLOYD MAYWETHER VS MIGUEL COTTO PAMOJSA NA MAPAMBANO YA UTANGULIZI YALIOCHEZWA SIKU YA MPAMBANO
MAPAMBANO MAKALI YA NGUMI ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

KALAMA NYILAWILA KUMVAA IBRAHIMU MAOKOLA DESEMBA 31 MSASANI KLABU


Msimamizi wa Mchezo wa ngumi katika kambi iliyopo sinza
makaburini, Bernald Lumbila (kushoto) akimwelekezai bondia Kalama Nyilawila jinsi ya kupiga ngumi katika mbavu Dar es saam Nyilawila anajiandaa na mpambano wake dhidi ya Ibrahimu Maokola utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu Picha nawww.superdboxing coach.blogspot.com
Kalama Nyilawila akijifua
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Kalama Nyilawila yupo katika mazoezi makali ya mwisho mwisho kabla ajamkabili mpinzani wake Ibrahimu Maokola siku ya Desemba 31  mpambano wa kufunga mwaka utakaoshirikisha mabondia mbalimbali akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kalama ameseme yeye yupo fiti wakati wowote kwa ajili ya mpambano huo kwa ana usongo wa kuonesha ngumi zinachezwaje kwa mabondia chipkizi nchini

Mpambano huo utaanza kabla ya bondia Fransic Miyeyusho kupanda jukwaani kuvaana na David Chalanga kutoka Kenya mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi

na mapambano mengine ni Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atavaana na Mohamed Kashinde uku Cosmas Cheka akioneshana ubabe na Iddy Mnyeke mpambano mwingine ni Antoni Mathias atakae menyana na Fadhili Majiha mapambano yote ya utangulizi ni ya raundi sita sita 

siku hiyo itasindikizwa na burudani za kila aina akiwemo mwana hi pop mashuhulu Kala Pina, Kimbunga Noma na wengine wengi ambao wata uanga mwaka na kukaribisha mwaka mpya kwa njia ya burudani
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Audhuria ibada Kijijini Kwake Kibaoni wilayani Mlele, Katavi



 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wazee baada ya ibada ya  Krismasi iliyofanyika kijijini kwake, Kibaoni wilayani  Mlele, Katavi, Desemba 25, 2013.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na watoto  baada ya ibada ya Krismasi iliyofanyika  kijijini kwa Waziri Mkuu, Kibaoni wilayani Mlele, Katavi Desemba 25,2013.Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI AENDA MUHIMBILI KUWAFARIJI WAGONJWA


 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.Akiwa nachini Marekani Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali. Picha na Freddy Maro
 Juu na chini ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba (15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowatembelea na kuwafariji  baadhi ya wagonjwa katika wodi ya Mwaisela leo.
Rais akizungumza na mtoto huyo.

FUMANIZI KRISMAS HILI HAPA


KRISMASI noma sana! Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Pendo ameiona chungu Sikukuu ya Krismasi 2013 kufuatia tukio la kufumaniwa na mkewe, Mama Pendo au Mama P ‘akibanjuka’ na mwanamke ndani ya gari.

NI MKESHA WA KRISMASI
Tukio hilo la aina yake lilijiri eneo maarufu Kijitonyama jijini Dar linalojulikana kwa jina la Miti Mirefu, usiku wa Mkesha wa Krismasi, majira ya saa 8:00 usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.
Ina maana kwamba Baba Pendo aliamua ‘kumalizia shida’ zake ndani ya gari hilo ambalo namba zake za usajili tunaziweka kapuni.


OFM YAJUZWA
Kabla ya tukio hilo, mara kadhaa Mama P aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na kulalamika juu ya mumewe kutoka nje ya ndoa na mwanamke mmoja wa mjini.
Mama P: Haloo…naongea na OFM? Jamani naombeni mnisaidie kuna mwanamke anamzuzua sana mke wangu.
OFM: Una uhakika mama?

Mama P: Nina uhakika wa asilimia mia moja. Hapa nimeona meseji wamepanga kukutana leo na ndiyo maana nikawatafuta. Ninyi mpo wapi?
OFM: Sawa, sisi tupo kikazi Mango Garden (Kinondoni, Dar) wewe upo wapi?
Mama P: Nipo Sinza A (Dar) nitawashtua mambo yakiiva maana najua lazima mume wangu atatoka muda si mrefu, nimemuona anajiandaa.

OFM: Oke lakini uwe makini sana.
Mama P: Sawa, nitawashtua.
Hiyo ilikuwa saa 5:12 usiku, hivyo OFM iliendelea na majukumu mengine ya kufichua uovu katika jamii.

BABA PENDO AAGA ANAKWENDA MKESHA
Kwa mujibu wa Mama P, majira ya saa 5:20 usiku, mumewe alimuaga anakwenda kwenye mkesha wa kumpokea mwana wa Mungu (Yesu) aliyezaliwa ambapo kwa mujibu wa mume huyo, alikuwa anakwenda kusali Kanisa la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo Mwenge, Dar.

MAMA P MZIGONI
Baada ya mumewe kuondoka, mwanamke huyo aliwasiliana na OFM na kuwapa ishu nzima ambapo walimpa mbinu ya kumfuatilia mumewe ikiwa ni pamoja na kubadili aina ya usafiri ili asishtuke.

Mama P alichukua Bajaj na kumfuatilia mumewe hadi maeneo ya Sinza-Kijiweni ambapo alimuona akipaki gari lake na kuingia kwenye ‘pabu’ moja kisha akaagiza ‘ngumu kumeza’ (mzinga wa konya) ambayo aliipiga taratibu hadi mishale ya saa 8: 05 usiku huku akipiga stori na washkaji.
Baada ya hapo, Baba Pendo aliingia garini kuondoka. Mama P naye akachukua bodaboda kumfuatilia kwa nyuma.
Alipofika maeneo ya Kijitonyama  alimuona akisimamisha gari na kuingia kwenye ‘kamtaa’ f’lani, akatoka na mwanamke kisha akaingia naye kwenye gari.
Alisema yeye akiwa bado nyuma, walipofika Miti Mirefu  mumewe alipaki gari lakini hakuna aliyeshuka.

Aliendelea kusimulia kisa mkasa mbele ya ‘kachero’ wa OFM kuwa uvumilivu ulimshinda, alihisi kuna linaloendelea ndani ya gari,  akaamua kulisogelea na ndipo hamadi! Akamkuta mumewe ‘laivu akiduu’ na mwanamke huyo na ndipo OFM walipochomoza baada ya kujulishwa kuwa ishu imetiki.
“Uzuri ni kwamba walisahau ‘kuloki’ milango ya gari ‘so’ nilipoushika ukafunguka,” alisema Mama P baada ya OFM kupiga picha za kutosha.

TIMBWILI
Katika tukio hilo kulitokea timbwili ambapo askari waliokuwa doria walitonywa na kufika eneo la tukio na kuamulia damu isimwagike.
Mwanamke aliyenaswa na mume wa mtu alikula mbata za kufa mtu huku mwanaume akitoka nduki kukwepa aibu ya kamera za OFM.

MAMA P HASIRA
OFM ilimsikia Mama P akisema: “Kumbe ndiyo wewe…nilikuwa nakufuatilia muda mrefu, badala ya kwenda kanisani unahangaika na waume za watu hata humuogopi Mungu.”

Hadi gazeti hili linaondoka eneo la tukio, wanawake hao walikuwa mikononi mwa polisi wakitakiwa kuacha ugomvi na kama kuna malalamiko wayafikishe

BALOZI IDDI APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA MICHEZO YA KOMBAINI YA WANAFUNZI


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea vifaa mbali mbali vya michezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan and Sons kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake Mohd Raza kusaidia mashindano ya Kombaini  za wanafunzi wa Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************************
 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  imedhamiria kufufua upya vugu vugu la michezo Nchini ili kuirejeshea hadhi yake Zanzibar katika Nyanja za Michezo Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa  vifaa vya michezo pamoja na vyakula kwa ajili ya washiriki wa mashindano ya Kombaini za wanafunzi za Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliyofanyika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema  heshima ya Zanzibar  kimichezo lazima  iwepo kwa kuhakikisha  Vijana wanaandaliwa vyema Maskulini ambako ndiko kunakopatikana  vipaji vya michezo mbali mbali vinavyoweza kuirejeshea heshima yake Zanzibar.
Alifahamisha kwamba jamii popote pale hapa Nchini inahitajika kuongeza ari ya kuwaamsha vijana kwenye mitaa yao katika kupenda na hatimae kushiriki kwenye michezo tofauti kulingana na uwezo wa vijana wenyewe.

“ Zanzibar inaweza kurejea tena katika hadhi yake ya kimichezo Kimataifa kama mpango utakaoandaliwa wa kuamsha vugu vgugu la michezo utapokelewa vyema katika maskuli mbali mbali hapa nchini “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  aliupongeza Uongozi wa  Kampuni ya Hassan and Son’s, Zat pamoja na ule wa Zanzibar Ocean View kwa uwamuzi wao wa kuchangia  sekta ya michezo nchini mbali ya kudumisha ushirikiano lakini pia husaidia kutoa ajira kwa wanamichezo nchini.
Akitoa Taarifa ya mashindano hayo ya Kombaini za wanafunzi za Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mkuu wa kitengo cha michezo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mussa Abdullrabi Fadhil  alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya vijana maskulini.
Abdullrabi Fadhil alisema tafiti zinaonyesha kwamba vipaji vingi katika sekta za michezo mara nyingi hupatikana miongoni mwa wanafunzi katika skuli mbali mbali hapa nchini.

Alieleza kwamba mashindano hayo yataoshirikisha michezo tofauti ikiwemo soka, Wavu, mchezo wa Bao, Pete pamoja na Table Tennis kwa kujumuisha wanafunzi wa unguja na pemba yanatarajiwa kufunguliwa rasmi  Tarehe 29 Disemba mwaka huu wa 2013 katika uwanja wa michezo wa Uzini Wilaya ya Kati na kumalizika tarehe 5 Januri mwaka 2014.
Mapema Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan And Sons Mohd Raza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake waliochangia vifaa hivyo vya michezo pamoja na vyakula alisema Serikal lazima iungwe mkono na wafanyabiashara pamoja na wananachi katika kusaidia kupunguza au kuondoa kabisa kero zinazoikabili jamii.
Alisema utaratibu huo kwa njia moja utaiwezesha Zanzibar  kurejea katika heshima yake kimichezo iliyokuwa ikitambulikana katika sehemu mbali mbali ulimwenguni.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amepokea vifaa vya michezo kwa ajili ya kuchangia maandalizi ya mashindano ya kombe la mapinduzi linalotarajiwa kushirikisha Timu 12 za soka za kitaifa na kimataifa pamoja na timu 27 za michezo mengine ya ndani.
Vifaa hivyo vilivyojumuisha vikombe vitatu kwa washindi wa mwanzo, medani, T. Shirts, Redio maalum kwa Mchezaji, mfungaji na Kipa bora wa mashindano hayo vimetolewa kwa pamoja na Kampuni ya Hassan and Sons, Zat pamoja na Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Akipokea vifaa hivyo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza uongozi wa Makampuni hayo kwa michango yao hiyo itayosaidia kufanikisha vyema mashindano hayo.
Balozi Seif alisema michango ya uongozi wa Kampuni hiyo italeta changamoto kubwa kwa wanamichezo kuweza kujikita zaidi katika hamasa ya kuendeleza vyema mashindano hayo ya kimataifa kwa mwaka huu.
Mapema Mwakilishi wa makampuni hayo ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza aliahidi kwamba yupo tayari wakati wowote kutoa mkopo wa dharura endapo yatajitokeza mapungufu wakati wa maandalizi ya sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Nusu Karne.
Alisema yeye kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake wakati wowote wataendelea kuiunga mkono Serikali kuu katika kutoa michango na misaada itayosaidia kupunguza  matatizo yanayowasumbua wananchi.

Akipokea vifaa hivyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kutafuta fedha kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Sharifa Khamis aliwakumbusha wafanyabiashara nchini kuiangalia pia michezo ya ndani katika misaada wanayotoa ili kwenda sambamba na ule mchezo uliozoelewa wa soka.
Timu kadhaa za mchezo wa zimeshathibitisha kushiriki mashindano hayo miongoni mwao zikiwemo timu za soka za Yanga , Simba na Azam za Tanzania Bara, timu za Nchi jirani za Afrika Mashariki, Ikiwemo Sudan ya Kusini, China pamoja na Vietnam.

MBUNGE FILIKUNJOMBE ATIMIZA AHADI ZAKE KWA KANISA LA ANGLIKANA ILELA LUDEWA


Waumini  wa Kanisa la  Anglikana  Ilela  Ludewa  wakimshangilia  mbunge  wao  Deo  Filikunjombe  wakati  akitolea ufafanuzi  wa misaada  anayoitoa  kanisani hapo  ,wakati  wa ibada ya Krismas
Mmoja kati ya  waumini wa kanisa  hilo akishukuru kwa  kulala  chini  wakati  mbunge  wao akitoa  misada  yake
Mbunge  wa   jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe wa pili  kulia akikabidhi msaada wa marumaru  seti  100 kwa  mchungaji wa kanisa la  Anglikana mtaa  wa  Ilele  Ludewa mchungaji Canon Ngoye
Wananchi  na  waumini  wa kanisa la Anglikana   mtaa wa Ilela  Ludewa  wakimuwekea mikono ya baraka  mbunge Deo Filikujombe baada ya  kukabidhi misaada kanisan i hapo
Waumini  wa kanisa la Anglikana  mtaa wa Ilela Ludewa akifurahi pamoja na mke  wa mbunge Deo Filikunjombe Bi Habiba Filikujombe mwenye nguo  nyekundu kati
Waumini  wa kanisa  hilo  wakimshangilia mbunge  wao
Mmoja  kati  ya  waumini  wa kanisa  hilo  akimfuta jasho mbunge  Deo Filikunjombe kama  ahsante kwa  kuwajali  wapiga kura  wake
Mbunge  Filikunjombe  akitoa neno kwa  wapiga kura  wake kanisani  hapo

STENDI YA NJOMBE JIMBONI KWA SPIKA MAKINDA YALALAMIKIWA

Abiria   wakipita kwa shida katika  stendi ya  Njombe 
Mwanahabari  wa Clouds TV na Radio Recho akitafuta  eneo la  kupita  katika  stendi  hiyo ya Njombe 
Madereva  na  abiria   wanaotumia  stendi ya Njombe mjini  ambayo ni stendi kuu ya mabasi  yaendayo mikoani  wamelalamikia  ubovu  wa stendi  hiyo na kumwomba  mbunge wa  jimbo  hilo Anne  Simamba  Makinda  kushughulikia  tatizo  hilo.

Wakizungumza na mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com  madereva hao na  wananchi  walisema  kuwa  ubovu wa stendi  hiyo umekuwa ni kero kubwa  kwao  na  kuiomba  Halmashauri  ya  mji  wa Njombe  kulishughulikia  suala   hilo

John Sanga  ni  mmoja  kati ya madereva  eneo hilo la stendi alisema kuwa  wameshangazwa na hatua ya  mbunge  wao ambae ni spika wa Bunge  kushindwa  kuwajibika kwa kusimamia utengenezaji wa  stendi hiyo.

Kwa  alisema  wakati wa jua  eneo hilo limekuwa  likiongoza kwa  kuwa na  vumbi na  wakati wa masika  linaongoza kwa kuwa na tope sana .

Hata   hivyo  alisema  kuwa uongozi  wa serikali ya  Njombe  umekuwa ukitoa ahadi ya  kutengeneza stendi  bila kutekeleza kwa wakati na pale  madereva  wanapotaka  kugoma wamekuwa  wakitumia polisi  kuwakamata  waanzilishi  wa migomo  hiyo.

Huku Sarah Ndelwa ambae  ni mmoja kati ya abiria   waliohojiwa akimtaka  mbunge Makinda  kusaidia  kuondoa aibu hiyo ya ubovu wa  stendi  nyumbani kwake

Thursday, December 26, 2013

MOHAMED MATUMLA AMGALAGAZA NASSIBU RAMADHANI KWA POINT NA KUIBUKA NA PIKIPIKI



Bondia Mohamed Matumla kushoto akimwadhibu Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao wa raundi kumi uliofanyika siku ya sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mohamed Matumla kushoto akipambana na Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao  uliofanyika siku ya sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana na Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya krismas kayage alishinda kwa k,o picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

lulu akinyooshwa mkono juu baada ya kushinda

l
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana na Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya krismas kayage alishinda kwa k,o picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Hamis Ajari kushoto akipambana na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao uriofanyika wakati wa sikukuu ya krismas cheka alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Sadiq Abdulazizi kushoto akipambana na Juma Fundi wakati wa mpambano wao uliofanyika wakati wa sikukuu ya krismas juma fundi alishinda kwa point mpambano uho picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya mashabiki waliouhulia mpambano huo uliokuwa mkali na kutoa burudani ya aina yake kwa mashabiki nchini

PACQUIAO: Mbabe anayemkuna David Beckham



pacquiao na familia yake
MARA baada ya Desemba mwaka jana kupoteza pambano lake dhidi ya mbabe Juan Manuel Marquez kwa ‘KO’ mbabe na mbunge Manny Pacquiao alionekana kama zama za utawala wake katika masumbwi zilikuwa zimefikia ukomo.
Mbabe huyo amefuta wale waliokuwa na dhana hiyo baada ya kurejesha heshima yake kwa kumchakaza kwa pointi Brandon Rios mjini Macau, katika pambano alilolifanya kwa ajili ya kusaidi waathirika wa mafuriko yaliyotokea nyumbani kwao Ufilipino na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 4000 na wengine milioni nne wakikosa makazi.
Alishinda kwa jumla ya pointi 120 kwa 109 na baada ya kumalizika kwa pambano hilo Pacquiao alitamka bayana kwamba yuko tayari kupambana na bondia yeyote akiwamo mbabe asiyepigika Floyd Mayweather.
Bob Arum ambaye ni promota wa Pacquiao ametenga kiasi cha dola milioni 300 kwa ajili ya pambano hilo lakini Mayweather ameshalitolea nje kwa kusema kuwa “sina mpango wa kufanya kazi na promota huyo, kwa sababu ni mbabaishaji amekuwa akikataa kuweka pambano hilo katika miezi ninayotaka ya May na Septemba,”.
USICHOKIJUA
Usichokijua ni kwamba mwanasoka maarufu kutoka Uingereza, David Beckham amebainisha kwamba ni shabiki mkubwa wa mbabe Manny Pacquiao na kwa kuthibitisha hilo hata katika pambano lake lililopita alisafiri hadi Macau kwenda kumshangilia.
Jambo jingine ni kwamba Manny Pacquiao amekuwa ni mpenzi wa hayati Bruce Lee na amekuwa akipenda kuuweka mwili wake kama mpambanaji huyo wa zamani aliyejipatia sifa kubwa duniani.
Kuingia katika katika medani za siasa haikuwashangaza sana Wananchi wa Ufilipino kwa kuwa alishaanza kukuzwa na rais wan chi hiyo, Arroya.
Mwaka 2012, Pacquiao aliweka rekodi ya kushika nafasi ya pili ya kuwa mwanamichezo na bondia anayelipwa zaidi duniani akilipwa dola milioni 62 huku nafasi ya kwanza ikikamatwa Floyd ‘Money’ Mayweather.
Ukiachilia masuala ya ngumi pia ni mwigizaji mzuri wa filamu akiwa amecheza tamthilia kadhaa zinazoratibiwa na ABS-CBN
UTAJIRI
Mbabe huyo anamiliki utajiri unaofikia kiasi cha dola milioni 100 (sawa na shilingi bil. 160).
Fedha hizo amekuwa akiziingiza kwa mchezo wa ngumi na kufanya matangazo mbalimbali ya kibiashara ikiwamo tangazo la bia za San Migue.
Ukiachilia hayo mbabe Manny anamiliki baada yake kubwa katika maeneo maarufu kwa starehe katika kisiwa Boracay huko Aklan akiwa ameshirikiana na mfanyabiashara mwingine, Crisostomo ‘Cris’ Aquino waliyoianzisha tangu mwaka 2006.
Baa ya wawili hawa inajulikana kwa jina la Boracay West Cove ikiwa

Manny Pacquiao Decided to Still Continue Boxing Career Despite Wife’s Plea

Manny Pacquiao was shockingly knocked out in his fight with Juan Manuel Marquez but that does not stop the Filipino boxing champ.

According to Pacquiao, he still wants to continue boxing even though his wife Jinkee requested him to retire now.

The 33-year-old Filipino boxer fell down face first on the canvas from a knock-out punch then remained unconscious for several seconds as his wife tried to enter the ring. Jinkee Pacquiao admitted that she was terrified after witnessing what happened to her husband causing her to scream and cry before promoter Bob Arum calmed her down.

"It's the first time I've seen him like that, lying on the canvas, and I was scared,'' Jinkee Pacquiao told USA TODAY Sports. "I know he is still capable of fighting but for me there is nothing to prove. He already has eight title belts. He can retire - stop - at anytime. I want him to stop now. But he is the one who has the last say. Boxers risk their lives, some end up in wheelchairs. I don't want that to happen to Manny," Jinkee further stated.

Manny Pacquiao confirmed to USA TODAY Sports that he has no intentions of retiring after his loss to Juan Manuel Marquez.

"I remember hitting the canvas. My head dropped - boom! But I feel good. He just got lucky with that one punch. It made good impact because my face was going forward. It was all timing. He threw the punch without looking and he was surprised it landed. But give him credit," Pacquiao stated.

One significant basis why Manny Pacquiao wants to continue fighting is his finances. "Pacquiao has already earned huge sums of money in the last three years which includes an estimated gross of $175 million in the ring," Bob Arum revealed to USA TODAY Sports.

The couple reportedly has an extravagant money spending habits aside from the donations given to charitable causes. Mike Koncz, business adviser and chief negotiator of Manny Pacquiao, is now a little bit concerned over the couple's unnecessary lifestyle.

"Sometimes Manny gets angry with me because I'm overprotective of his money," Koncz revealed to USA TODAY Sports.

"In a general sense, we're not in the position to sustain the same lifestyle now if he were to stop fighting tomorrow. He could quit tomorrow and live comfortably. Could he quit tomorrow and live extravagantly like we are now? No," Koncz further added.

Manny Pacquiao returned to the Philippines where his family and friends gave him a warm welcome. He will celebrate his 34th birthday on December 17 then go on a come back holiday trip to Israel with several family members from December 19-30.
inakarabatiwa kila mwaka kwa kufanya kuwa na muonekano mzuri na mpya.
NYUMBA
Mbabe huyo anamiliki mjengo mkubwa nchini mwao, ikiwa na vyumba vya kulala saba, nyumba hiyo iko kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2,300.
Paa lake limejengwa kwa vigae maalum kutoka nchini Japan ikiwa ni pamoja na geti la kufunguliwa kwa rimoti.
Jumba hilo lina bwawa la kuogelea ambalo lina sura ya glovu ya ngumi, kwa pembeni ya bwawa hilo kuna vitu kwa ajili ya waogeleaji na wageni wa nyumba hiyo. Jumba hilo pia lina gereji yenye uwezo wa kuhifadhi magari saba.
Bondia huyo ametumia gharama kubwa za fedha kwa ajili ya kulifanyia ukarabati jumba hilo na kuliwezesha kuwa na muonekano mzuri na wa kuvutia.
USAFIRI
Pamoja na kwamba mbabe huyo amekuwa na magari mengi lakini amekuwa akipenda zaidi kutumia gari aina ya Brand-new Ferrari 458 Italia.
MAHUSIANO
Jinkee Pacquiao 2006, Ara Mina aliyekuwa naye tangu mwaka 2007 na Krista Ranilo aliyedumu naye tangu mwaka 2009 hadi 2010.
Mbabe huyo anaishi na mkewe anayejulikana kama Maria Geraldine Jamora na wamefanikiwa kupata watoto wanne ambao ni Emanuel, Princess, Michael na Queen Elizabeth.
WASIFU
JINA: Emanuel  Manny Pacquiao
UMRI: Desemba 17, 1978
ENEO LA KUZALIWA: Bukidnon, Mindanao, Philippines
KIMO: Futi 5 na inchi 6
UTAIFA: Ufilipino
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...