Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea vifaa mbali mbali vya
michezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan and Sons kwa
niaba ya wafanyabiashara wenzake Mohd Raza kusaidia mashindano ya
Kombaini za wanafunzi wa Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************************
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar imedhamiria kufufua upya vugu vugu la michezo Nchini ili
kuirejeshea hadhi yake Zanzibar katika Nyanja za Michezo Kimataifa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo katika
hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya michezo pamoja na vyakula kwa ajili
ya washiriki wa mashindano ya Kombaini za wanafunzi za Wilaya 10 za
Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla
iliyofanyika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Nje kidogo ya
Mji wa Zanzibar.
Balozi
Seif alisema heshima ya Zanzibar kimichezo lazima iwepo kwa
kuhakikisha Vijana wanaandaliwa vyema Maskulini ambako ndiko
kunakopatikana vipaji vya michezo mbali mbali vinavyoweza kuirejeshea
heshima yake Zanzibar.
Alifahamisha
kwamba jamii popote pale hapa Nchini inahitajika kuongeza ari ya
kuwaamsha vijana kwenye mitaa yao katika kupenda na hatimae kushiriki
kwenye michezo tofauti kulingana na uwezo wa vijana wenyewe.
“
Zanzibar inaweza kurejea tena katika hadhi yake ya kimichezo Kimataifa
kama mpango utakaoandaliwa wa kuamsha vugu vgugu la michezo utapokelewa
vyema katika maskuli mbali mbali hapa nchini “. Alisema Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Kampuni ya Hassan
and Son’s, Zat pamoja na ule wa Zanzibar Ocean View kwa uwamuzi wao wa
kuchangia sekta ya michezo nchini mbali ya kudumisha ushirikiano lakini
pia husaidia kutoa ajira kwa wanamichezo nchini.
Akitoa
Taarifa ya mashindano hayo ya Kombaini za wanafunzi za Wilaya 10 za
Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mkuu wa kitengo
cha michezo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mussa Abdullrabi Fadhil
alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya vijana maskulini.
Abdullrabi
Fadhil alisema tafiti zinaonyesha kwamba vipaji vingi katika sekta za
michezo mara nyingi hupatikana miongoni mwa wanafunzi katika skuli mbali
mbali hapa nchini.
Alieleza
kwamba mashindano hayo yataoshirikisha michezo tofauti ikiwemo soka,
Wavu, mchezo wa Bao, Pete pamoja na Table Tennis kwa kujumuisha
wanafunzi wa unguja na pemba yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Tarehe 29
Disemba mwaka huu wa 2013 katika uwanja wa michezo wa Uzini Wilaya ya
Kati na kumalizika tarehe 5 Januri mwaka 2014.
Mapema
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan And Sons Mohd Raza kwa niaba
ya wafanyabiashara wenzake waliochangia vifaa hivyo vya michezo pamoja
na vyakula alisema Serikal lazima iungwe mkono na wafanyabiashara pamoja
na wananachi katika kusaidia kupunguza au kuondoa kabisa kero
zinazoikabili jamii.
Alisema
utaratibu huo kwa njia moja utaiwezesha Zanzibar kurejea katika
heshima yake kimichezo iliyokuwa ikitambulikana katika sehemu mbali
mbali ulimwenguni.
Wakati
huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amepokea vifaa vya michezo
kwa ajili ya kuchangia maandalizi ya mashindano ya kombe la mapinduzi
linalotarajiwa kushirikisha Timu 12 za soka za kitaifa na kimataifa
pamoja na timu 27 za michezo mengine ya ndani.
Vifaa
hivyo vilivyojumuisha vikombe vitatu kwa washindi wa mwanzo, medani, T.
Shirts, Redio maalum kwa Mchezaji, mfungaji na Kipa bora wa mashindano
hayo vimetolewa kwa pamoja na Kampuni ya Hassan and Sons, Zat pamoja na
Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Akipokea
vifaa hivyo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza uongozi wa Makampuni hayo kwa
michango yao hiyo itayosaidia kufanikisha vyema mashindano hayo.
Balozi
Seif alisema michango ya uongozi wa Kampuni hiyo italeta changamoto
kubwa kwa wanamichezo kuweza kujikita zaidi katika hamasa ya kuendeleza
vyema mashindano hayo ya kimataifa kwa mwaka huu.
Mapema
Mwakilishi wa makampuni hayo ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini
Mohd Raza aliahidi kwamba yupo tayari wakati wowote kutoa mkopo wa
dharura endapo yatajitokeza mapungufu wakati wa maandalizi ya sherehe
hizo za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Nusu Karne.
Alisema
yeye kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake wakati wowote wataendelea
kuiunga mkono Serikali kuu katika kutoa michango na misaada itayosaidia
kupunguza matatizo yanayowasumbua wananchi.
Akipokea
vifaa hivyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kutafuta fedha kwa ajili ya
kufanikisha mashindano hayo ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Michezo Zanzibar Sharifa Khamis aliwakumbusha wafanyabiashara nchini
kuiangalia pia michezo ya ndani katika misaada wanayotoa ili kwenda
sambamba na ule mchezo uliozoelewa wa soka.
Timu
kadhaa za mchezo wa zimeshathibitisha kushiriki mashindano hayo
miongoni mwao zikiwemo timu za soka za Yanga , Simba na Azam za Tanzania
Bara, timu za Nchi jirani za Afrika Mashariki, Ikiwemo Sudan ya Kusini,
China pamoja na Vietnam.
No comments:
Post a Comment