Meneja wa NMB Mlimani City Bw. Leonard Ngaya (kushoto)
akikabidhi sehemu ya madawati 55 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Makuburi Jeshini Bi. Stella Kaluse (kulia).
Wakishuhudia makabidhiano hayo ni Mwenyekiti wa Kata ya Makuburi Bw. Moshi
Kaftanyi (katikati) na Meneja wa NMB tawi la University Bw. Charles Mapunda . Hafla ya Makabidhiano haya
yalifanyika hivi karibuni katika viwanja vya shule hiyo.
Wawakilishi toka NMB pamoja na uongozi wa shule wakiwa
kwenye picha ya pamoja na wanafunzi
baada ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya kupunguza
uhaba wa madawati katika shule hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika
viwanja vya shule ya makuburi jeshini hivi karibuni.
Hivi
karibuni, Benki ya NMB imeukabidhi Uongozi wa shule ya msingi Makuburi
Jeshini jijini Dar es Salaam msaada wa madawati yenye thamani ya
shilingi million tano. Madawati ambayo yatasaidia kupunguza upungufu wa
madawati katika shule hiyo.
No comments:
Post a Comment