GEORGE Edward Foreman au Big George ni jina kubwa katika ulimwengu wa michezo, hasa masumbwi.
Wengine hupenda kumwita ‘The Heywood Giant’ kwa sababu ya alikotokea na
ukubwa wake wa umbo, ambapo ni Mmarekani ambaye kwa sasa amefikisha
umri wa miaka 64.
Foreman anasema kwamba anakumbukia enzi
zake, na kama kuna mambo ambayo hatasahau ni ngumi ya Joe Frazier
anayosema ilimpata sikioni na kuwa kama radi.
Anasema
akiikumbuka anachukia ndondi, lakini kwamba ngumi hiyo ya kijana
aliyekuwa mdogo ndiyo ilimfanya akaongeza jitihada ili awe bondia mzuri
na kweli alifanikiwa kuwa bora kama akina Muhammad Ali.
“Hakuwa mpiganaji mkubwa lakini ndiye pekee niliyekuwa namwogopa tukiwa
ulingoni maana alijiamini sana, hata nilipompiga na kumdondosha,
alinyanyuka haraka sana na kuwa kama mbogo aliyejeruhiwa,” anasema.
Anakumbuka alivyomwangusha mara sita lakini kila baada ya kufanya hivyo
alinyanyuka na kuendelea na pambano mpaka watu wakamshauri mwamuzi
asitishe pambano, lakini naye Foreman aliondoka na majeraha makubwa ya
sikio na anasema aliogopa kwamba Frazier angemuua.
Hayo
yalikuwa ya zamani lakini sasa Foreman ameanzisha kampuni yake inayoitwa
‘Foreman Boys Promotions’ ambayo inasimamia ndondi kwa kuandaa
mapambano.
Kazi yao ya kwanza ilikuwa ni pigano la uzani wa
Feather kati ya bondia wa Puerto Rico, Juan Manuel Lopez na Mmarekani
ambaye hakupata kupigwa kabla ya hapo, Mikey Garcia.
Foreman aliwahi kupata medali za dhahabu kwenye michuano ya Olimpiki na alikuwa bingwa mara mbili wa uzani wa juu duniani.
Kwa sasa, tofauti na kufanya promosheni za ngumi, Foreman anaandika vitabu na kuendesha biashara mbalimbali. Katika utoto wake alikuwa na matatizo makubwa lakini amekuja kufanikiwa kwenye masumbwi na maisha kwa ujumla.
Alipoteza pambano lake kwa Muhammad Ali mwaka 1974 katika kile
kilichoitwa ‘The Rumble in the Jungle’. Alistaafu baada ya kupoteza
pambano dhidi ya Jimmy Young 1977.
Alipata kustaafu lakini baadaye 1994 alirudi ulingoni akapigana akiwa na umri wa miaka 45 akichapana na Michael Moorer.
Kwa sasa anashikilia rekodi ya kuwa bingwa mwenye umri mkubwa zaidi wa
uzani wa juu duniani ambapo ameshinda mapambano 76 kati ya hayo 68
yakiwa ni kwa ‘Knock Out’.
Anachukuliwa kuwa bondia namba nane
kwa umaarufu duniani kwenye uzani wa juu, ambapo mwaka 2002 alitajwa
kuwa miongoni mwa mabondia 25 bora katika miaka 80 iliyopita.
Hata hivyo, jarida la ‘The Ring’ lilimtaja kuwa bondia namba tisa kwa ubora.
Nje ya ulingo ni mjasiriamali aliyefanikiwa sana na maisha yake
yanakwenda vyema na anasifika sana huko alikozaliwa, Marshall, Texas.
Alilelewa na J.D. Foreman aliyemwoa mama yake, lakini baba yake mzazi ni Leroy Moorehead.
Foreman alikuwa anapenda zaidi soka na si ajabu leo angekuwa mmoja wa
wanasoka maarufu zaidi duniani, akifuata nyayo za Jim Brown, lakini
aliamua kuachana na mchezo huo na kujiunga na masumbwi.
Vyombo
vya habari havikumsema vizuri sana kwa sababu vilidai hakuwa na urafiki
navyo hata alipotakiwa kuongea alikuwa mkinya akivikwepa.
Foreman alipata kwenda Afrika, ambapo alikuwa akifanya mazoezi nchini
Zaire, ambapo katika mazoezi alijiumiza juu ya jicho na kulazimika
kuahirisha mechi aliyokuwa nayo kwa mwezi mmoja.
Wakati huo,
hata Ali mwenyewe alizuru Zaire kabla ya pambano lao, nchi iliyokuwa
imechanua vyema kimazingira japokuwa iliharibiwa na wanasiasa.
Katika tawasifu yake, Foreman anasema kwamba lengo lake kubwa lilikuwa
kutafuta fedha kwa ajili ya kituo cha vijana lakini pia kupambana na
Mike Tyson. .Chanzo gazeti la SPOTILEO zaidi tembelea mtandao wa http://superdboxingcoach.blogspot.com/ na kwa mahitaji mbali mbali ya dvd za mafunzo ya ngumi wasiliana na kocha kwa namba za simu
No comments:
Post a Comment